Nakuomba Rais Samia achana na mpango wa kuibinafsisha bandari wacha Watanzania wafe na umasikini wao

dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
9,404
15,985
Nimeona nije kivingine kbsa kuhusu hili la bandari kupewa dp world

Mwanzo nilielewa dhamira ya serekali yako juu ya kuwekeza bandari kwa dp world lkn kutokana na kelele zilizojitokeza na yanayo endelea kusemwa juu ya suala Hilo.

Nimesikiliza mjadala wa bunge na kuwasikiliza baadhi ya watu wasomi Kama prof ,kitila akisisitiza kuwa tusiogope kuwekeza bandari kwa waarabu wa dp world kwamba Ni mkataba mzuri na Ni Jambo jema Sana Hilo .

Lkn ajabu ukimsikiliza lisuu anasema Ni mkataba wa hovyo ambao hawajawai kuona tokea kusaliwa kwake kwamba Ni mkataba mmbovu na wa hovyo yake ,lema anasema yake kuwa Ni jambo jema,askofu pengo naye yake ,mbowe nae anasema yake ,Prof tibaijuka nae anasema yake ,yaani Ni vvurugu tupu tunashindwaa ss wananchi wa namanyere tumsikilize Nani ktk hili Jambo ...napatwa na wasiwasi Sana.

Lisu amefika mbali akasema wew na mbarawa na katibu mkuu uchukuzi mnauza Mali ya watanganyika huku mkiacha bandari yenu ya Zanzibar salama

Hili linatupa hofu Sana, mimi nakushauri achana na huu mpango wako wacha watanzania wafe na umasikini wao fanya mambo mengine hili la bandari kuu litagawa inchi Sana ,na tayari unapingwa Sana mbaya Zaid wote mnaofanya Hilo Jambo ni wanzanzibari

Kama mkapa, kikwete, JPM, Mwinyi hawakuweza kuuza kwanini wewe uangaike na Jambo hili la hatari linalotaka kugawa nchi yetu?

Rasilimali ni za Watanganyika na watanganyika tumeridhika na uendeshaji huu uliopo HV Sasa .Kama kuliwa acha eendelee kuliwa tu kuliko kuwapa hao watu wa dp world . bandarii hii tuliyopewa na mwenyezi mungu Ni heri tubaki HV HV kuliko kuwapa hao watu wanakuja kuleta usultani
 
Ingekuwa ni mkataba wa miaka kumi ingekuwa fresh tu, wakifanya vizuri wana renew, wakiboronga hawaongezewi mwingine. Huu mkataba usio na ukomo wa kueleweka ni kizingimkuti kilichowachanganya wananchi
 
Kiukweli watanganyika wapo kwenye mshtuko mkubwa kwa takribani mwezi sasa
Wanajadili kwa hasira sana huu mkataba wa nchi kupigwa mnada

Samia umekalia kiti kilochobeba ndoto za watanganyika milion 59

Achana na wazo la kuuza nchi utajiepusha na mengi
 
Kuna vitu vina ukakasi, kwamba Mbarawa, SHS wanaopenda Tanganyika kuliko Zbr?? Kwa nini za Zbr hazijaguswa km ni kwa nia njema? Tukumbuke huu ni mzigo wa watanganyika, tukishakuwa kitanzini watarudi pemba na kizmkz hawatakuwa na habari tena na upande wa ng'ambo. Tusitangulize ushabiki
 
Una hoja ila unavyosema tubaki na umaskini wetu ndo unapoleta ukakasi. Haiwezekani tuwe na bandari zaidi ya moja halafu tuendelee kuwa maskini. Kwa sasa bandari ina ufanisi mdogo na kibaya zaidi hicho kinachopatikana kinaliwa na wachache. Watu wote wanaohusika na bandari wana utajiri wa kufuru kwasababu ya upigaji. JPM alipambana nao ila hakuwaweza. Kama DP World watafanya wanachosema bàsi tutanufaika pakubwa. Ule uhuni wa watu wa bandari utamalizwa kabisa.
 
bandarii hii tuliyopewa na mwenyezi mungu Ni heri tubaki HV HV kuliko kuwapa hao watu wanakuja kuleta usultani
Unafikiri ni bandari moja inahusika?
Wanakabidhiwa bandari zote za Tanganyika zilizopo sasa na zitakazokuwepo baadaye, za bahari, maziwa, mito, nk
 
Umetoa hoja nzur sana, mwenye masikio asikie.Bandari zote za Tanganyika apewe Dp world,MAPATO yagawanywe kote,wakati ya kwao ipo pale pale.
 
Back
Top Bottom