Biashara ni jambo la kiroho(spiritual)

Biashara ni jambo la kiroho(spiritual)

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
561
Reaction score
991
Biashara ni jambo la kiroho(spiritual)

Binadamu ni roho ambayo ipo ndani ya mwili na nafsi.Roho ndio sehemu ambayo inaunganishwa na Mungu.

Maisha ya nje yaani kwenye mwili yana anzia ndani, ili uweze kufanikiwa nje lazima pia ndani utakuwa umefanikiwa.

Imani yako na mtazamo wako kwa kile unachokifanya una mchango mkubwa wa mafanikio ya kile unachofanya.

Ili uweze kufanikiwa nje yaani maisha yanayo onekana ata kwa watu anza kufanikiwa ndani, kuwa na amani ndani yako , ondoa vinyongo, samehe walikukosea, kuwa na shukrani, upendo.

Moyo uliokuwa na amani pia utulivu wa akili unavuta mafanikio kwenye maisha yako,
auta tumia nguvu kuvuta wateja kwenye biashara yako, watu wataku amini na kukupa fursa, kifupi nyota(aura) inakuwa ina ng'aa kwa mtu mwenye amani na utulivu wa akili ndani yake.

Ukiwa na moyo wa amani na utulivu wa akili ndani yako utakuwa unafanya maamuzi sahihi, kile utachofanya kitafanikiwa sababu akuna shinikizo ndani yako, haufanyi mambo kwa hisia bali kwa utulivu wa akili.

Watu wengi wanaingia kwenye fursa za kitapeli, pesa kupotea kwenye biashara, au miradi sababu walifanya maamuzi yao kwa hisia na sio utulivu wa akili.

Imani na juhudi, ili uweze kufanikiwa ni lazima pia uwe na imani kwa kile unachofanya, amini kwamba hichi ninachokifanya Mungu atasaidia nitafanikiwa atakama kuna changamoto kiasi gani.

Unapokuwa na imani , juhudi na nidhamu basi mafanikio yatakufuata, Yesu alisema ukiwa na imani unaweza kuamisha mlima kwa kusema na ukaama, hivyo kila kitu kinaanza na imani.

Kitu chengine ni uvumilivu na kujifunza, lazima ukubali kuvumilia kile unachokifanya, biashara inaitaji muda, kujifunza, kuongeza ubunifu na hii itapelekea kufanikiwa kwenye biashara yako.

Mafanikio yanaanza ndani yako kabla ajatokea nje na kuonekana kwa watu wengine, moyo wa amani, utulivu wa akili, imani kwa Mungu, uvumilivu, juhudi na nidhamu zitakufikisha kufanikiwa kwenye ndoto zako.

Kuna watu watasema mbona wengine awafanya hivyo vitu na wanafanikiwa,

Mafanikio yapo ya njia ya nuru na giza, hizo njia nilizotoa ni njia za Mungu au nuru,

Mafanikio ya Mungu yanakuwa na amani, unyenyekevu, msaada, upendo na kudumu muda mrefu.

Mafanikio ya njia za giza hayakupi amani,utulivu, hayadumu, watu waliopitia njia hizi maisha yanakuwa ayaeleweki, wamefanikiwa lakini akuna amani ndani yao.
 
Back
Top Bottom