Hakuna Mgogoro wowote CHADEMA - Zitto Kabwe

Hakuna Mgogoro wowote CHADEMA - Zitto Kabwe

Status
Not open for further replies.
Ukiona kivuli ujue kuna mtu nyuma.Hii thread ni ya watu wa CCM na Vibaraka wao.

Pungunguzeni kuniandama kwa kunirushia mapovu.Kama mlivyofanya hapa chini/juu.Wahuni wachache.....!

Wewe ni kirusi
 
Acha kuandika pumba wewe!!!! Dr slaa kishafukuza wanachama wangapi ndani ya CHADEMA!!!? Watu wengine banaaa ali mradi na wao waandike pumba zao tu ili kumponda Dr slaa hata kama hawana ushahidi wowote ule!!!! Haya pita Lumumba kesho saa tatu asubuhi kachukue buku 7 zako baada ya kuandika pumba.

Zitto kwa kweli ni mkomavu wa kisiasa angekuwa Dr Slaa aone mtu anamtukana halafu unagonga Like lazima ufukuzwe chama.
 
Last edited by a moderator:
ZZK mwanasiasa kijana na msomi pia ni role model wa wengi.kinachomponza CHADEMA ni uwezo wake mkubwa alionao kuliko viongozi wake wengine.HONGERA ZZK unakubalika na kuheshimika pia.
 
Zito kuwa mkweli demokrasia CSM hamna Wewe ulivyotaka uenyekiti hukushindwa kwa kura Bali wazee wa kichaga iliwrmo mtei walikwita then ukajitoa sema Kweli unaficha nini au tonge litakuponyoka unaogopa
 
Huyu mtu kajaliwa akili sana, ni mvumilivu, mstahimilivu. Anaweza kuwa mwenyekiti wa chadema. Mungu ampe uzima
Hata mimi nampenda sana Zitto lakimi kinachonitia hofu kwake ni kupendwa sana watu waCCM na waliohama chama sasa agombee urais kwa chama gani? Chadema aliko sasa au CCM anakopendwa zaidi? Maccm mwacheni Zito vinginevo kwa kumsifia sijui kama ,wamwongezea au mwampunguzia sifa Chadema
 
zitooooooooo.........
ameeendele kuthibitish kuwa yeye ni jembe,
najua maadui zake wakiona hivyo roho zinawapasuka kwa hasira.
Mtu smart ni smart tu, hata mfanyaje. Badala ya kumbomoa ndio kwanza wanazidi kumjenga.
Upo juu sana zkk. Mweneyezimungu akuongoze uwaletee watanzania mabadiliko ya kweli.

 
ukweli umeshaanza kupatikana. Maana lema na nasari walituambia watakuja na ushahidi wao sasa naona mpaka mda huu kimya. Zitto kamanda endelea na kazi yako wanafiki wote watakaa kimya. Sisi wananchi tunaona unachokifanya.
 
bado uko chadema si ulisema umemwaga manyanga?
by the way Zito bado kuwa rais anahitaji muda kwanza
siasa zake hazijakaa imara kuongoza nchi.
Tumpe muda ajifunze zaidi

Kwa kweli Zitto ni mtu wa kutumainiwa.

Angekuwa inawezekana akagombea urais angekonga nyoyo za watz
 
Akiwahutubia Wananchi wa Kaliua leo Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Zitto Kabwe ameonyesha kushangazwa kwake na kusikitishwa na uongo na uzushi unaofanywa dhidi yake na zaidi na watu wanaojidai kuwa ni Wanachadema pia.

Zitto amesema wakati huu ambao yeye amekuwa akihangaika kufuatilia watu na makampuni yaliyoficha fedha nje ya nchi vita ya kisiasa dhidi yake imezidi kuwa kubwa ambapo CCM, Matajiri hao na hata wanaCHADEMA wamekuwa wakimpiga mishale mingi ili kummaliza nguvu. "Mimi ni binadamu nikifinywa naumia, nikipigwa mishale pia naumia tusiruhusu watu waturudishe nyuma katika mapambano kwasababu ya maslahi yao" Alisema Zitto

Zitto aliongeza demokrasia ndani ya CHADEMA iko tangu siku nyingi ambapo mwaka 1995 Mzee Mtei alishindana na Mzee Bob Makani katika kinyang'anyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA lakini baadae waliamua kumuunga mkono Mrema. Mwaka 2000 Mzee Makani aligombea Uenyekiti akichuana na Mzee Ndesamburo na Makani kushinda lakini Chama kilikuwa pamoja. Kwanini yeye kugombea Uenyekiti 2009 iwe nongwa?? Alihoji!

Mnakumbuka Marando alivyoitwa Shushushu? Marando alinuka nchi nzima lakini leo Marando yuko wapi? si CHADEMA? Na ni Mwanasheria wetu kwa sasa.

Kama kweli kayaongea haya hapo kwenye BLUE ni ujinga uliopitiliza kwani sidhani kama ilikuwa ni mahara pake na napata shida kuelewa lengo la ziara yake ilikuwa ni nini, je ilikuwa ni kuimalisha chama au kubomoa chama? Zitto marumbano yaliyotokea yamefanyika kupitia mitandao ya kijamii inamaanisha alishindwa kujibu kupitia mitandao hiyo hadi leo hii atumie marumbano yale kwenye mikutano ya hadhara. Kwa hiki alichokifanya amezidi kujiweka mbali na Chama na kuonyesha wazi chanzo cha migogolo ndani ya CHADEMA ni yeye.
 
Kwa kweli Zitto ni mtu wa kutumainiwa.

Angekuwa inawezekana akagombea urais angekonga nyoyo za watz

2015 atagombea urais kupitia CCM chama ulichohamia kwani umeishajiondoa CDM baada ya kujiona mjinga na hoja yako ya masaa 24
 
kma mtu ana contacts na Rama Ighondu na Jack Zoka,Chadema bado mnamwamini?
 
Nna uhakika kati ya wanaopiga. "Hekaya za Abunuwasi" aliowaongelea Zitto ni Lema na vikaragosi vyake viwili maarufu humu JF.

Ni vipi hivyo vikaragosi vya hekaya za Abunuwasi?
 
Last edited by a moderator:
bado uko chadema si ulisema umemwaga manyanga?
by the way Zito bado kuwa rais anahitaji muda kwanza
siasa zake hazijakaa imara kuongoza nchi.
Tumpe muda ajifunze zaidi

Zitto yupo tayari ila chama bado hakimuamini. Na yote hii inaletwa na hawa vifaranga wa bavicha. Wanatunga hekaya wanazisambaza kumchafua naibu bila kujua hata wao wataathirika chama kikiyumba.
 
Kama kweli kayaongea haya hapo kwenye BLUE ni ujinga uliopitiliza kwani sidhani kama ilikuwa ni mahara pake na napata shida kuelewa lengo la ziara yake ilikuwa ni nini, je ilikuwa ni kuimalisha chama au kubomoa chama? Zitto marumbano yaliyotokea yamefanyika kupitia mitandao ya kijamii inamaanisha alishindwa kujibu kupitia mitandao hiyo hadi leo hii atumie marumbano yale kwenye mikutano ya hadhara. Kwa hiki alichokifanya amezidi kujiweka mbali na Chama na kuonyesha wazi chanzo cha migogolo ndani ya CHADEMA ni yeye.

Shule za kata tabu sana,hata kuandika hujui leo unamuona mh Zitto mjinga eti wewe una akili
 
Last edited by a moderator:
Ukiona kivuli ujue kuna mtu nyuma.Hii thread ni ya watu wa CCM na Vibaraka wao.!

Kuna tatizo gani shujaa wangu??? huoni kama kuna juhudi za watu kujenga chama? kwanini mnawachanganya wananchi? mnaacha mianya mingi wananchi kuichagua CCM 2015 tena.

Tuelewesheni mambo!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom