Hakuna mamlaka Duniani isiyowekewa mkono na Mungu

mtarimbo

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,529
3,919
Ni kweli tunajiuliza kama mamlaka zinawekewa mkono na Mungu, je wanaoiba kura halafu wanashinda huwa mkono wa Mungu unakua na hiyo serikali?

Mimi labda nitowe wazo langu. Labda hao wanaoibiwa kura na wakashindwa, MUNGU hajawakubali ndio maana akaruhusu waliopo waendelee hata kwa kutenda ulaghai.

Upinzani wa Bongo unahitaji maarifa makubwa sana ili kubeba dola maana walianza vizuri kupingana na mambo ya kifisadi na uzembe kwa watumishi wa umma sasa hivi wamegeuka kupinga maendeleo na kutetea watumishi wazembe, aiseeee! Alafu Mungu asaini mpewe dola?

Please Mbowe, jipange tafuta ulipokosea maana CHADEMA inaweza ikapata kibali mbele za Mungu.
 
Magufuli anataka kubadili katiba kuondoa ukomo wa Rais.

Dalili ndio hizi za kupitisha wabunge wa CCM bila kupingwa.
Kujenga uwanja wa ndege na Ikulu Chato.

Asante Thinktank
Asante PENTAGON
Quote ReplyReport
 
Magufuli anataka kubadili katiba kuondoa ukomo wa Rais.

Dalili ndio hizi za kupitisha wabunge wa CCM bila kupingwa...
Mkuuu ni wasiwasi wako tuu hilo haliwezi tokea wanaotaka afanye hivyo ni ugali wanalinda au wanatafuta kwa Magu maana mpango wa magu ni kuboresha viwanja vya ndefu 15 na kufanya 6 viwe vya kimataifa chato kajipendelea tuu .ili asisahau kwao .
 
Kwa hiyo Magufuli amewekewa mkono Mungu ili ajenge uwanja wa ndege Chato!?
Usilete masihara we kiumbe.
Uwanja siyo tatizo mkuu wengine waliiba kabisa pesa taslimu wakahamishia kwenye account zao je huyu Si bora kaifanyia kitu cha kuacha alama ya utumishi wake kwa ndugu zetu wa chato 😀😀😀😀 nyumbani ni nyumbani....
 
😀😀😀😀😀😀😀mkuu usipaniki sana ndio ukweli huo
Ninachokueleza ndio ukweli, serikali zote za dunia hii ni za shetani. Hata waingie CDM madarakani kesho bado haitobadili ukweli huo, labda kama wewe ni mgeni kwenye mambo haya ya kiroho, nenda kamuulize kiongozi wako atakupa ufafanuzi.
 
Mkuu hamna hiko kitu ilikua enzi hizo Mungu anachagua wafalme directly. Ila kwa hawa wanaotegemea tume na waganga kubaki madarakani Siku kweli Mungu akiamua achague kuna watu watapigwa na radi jukwaani tena mchana kweupe!
 
Ninachokueleza ndio ukweli, serikali zote za dunia hii ni za shetani. Hata waingie CDM madarakani kesho bado haitobadili ukweli huo, labda kama wewe ni mgeni kwenye mambo haya ya kiroho, nenda kamuulize kiongozi wako atakupa ufafanuzi.
Ok ngoja nichimbe zaid...
 
Mwambieni kuwa makaburu wa Afrika kusini waliijenga S.A kama ULAYA, lakini haikuwafanya "WASAUZI" wawapende makaburu kwa UKATILI wao.

Mnamo mwaka 1994 makaburu waliondolewa madarakani, kwahiyo TUDARAJA 'twake' tusimpe uhalali wa kulazimisha KUTAWALA watu kwa MKONO WA CHUMA.
 
Mathayo 4:8,9
Tena Ibilisi akampeleka Yesu kwenye mlima mrefu sana, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wazo.9 Naye akamwambia: “Nitakupa vitu hivi vyote ukianguka chini na kunifanyia tendo la ibada.”
 
MUNGU hawezi weka mamlaka yenye dhulma mfano kuwanyima watumishi Haki ya kupanda madaraja, mishahara Hadi wamekuwa wakopaji wakubwa Kadi zao za Benki zinashikiliwa mitaani ili waweze kuishi.
 
Back
Top Bottom