PostGE2025 Jaji Chande: Madai ya kuwepo kwa makaburi ya Kondo hayakuweza kuthibitishwa

PostGE2025 Jaji Chande: Madai ya kuwepo kwa makaburi ya Kondo hayakuweza kuthibitishwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,939
"Lakini pia, Mheshimiwa Rais, kulikuwa na madai ya kuwepo makaburi ya halaiki. Kulikuwa na madai hayo kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao ya kijamii kuhusu uwepo kwa makaburi ya halaiki eneo la makaburi ya Kondo, Kunduchi, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Tume imefanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kutembelea na kukagua eneo la makaburi, kufanya mahojiano na kupata taarifa ya afisa msimamizi wa makaburi hayo kutoka Manispaa ya Kinondoni na kuchukua ushahidi wa wasimamizi wa makaburi ya Kondo.

Tume pia imeshirikisha wataalamu mbalimbali ili kufanya uchunguzi wa kisayansi kuhusu madai hayo ikiwa pamoja na picha za satellite zilizotumika kuleta madai hayo. Maoni ya wataalamu hao wakiwemo wachambuzi wa mbalimbali wa mifumo ya taarifa za kijiografia, Remote Sensing and Geographical Information System, ni kwamba madai hayo hayakuweza kudhibitishwa.

Soma Pia Uchunguzi wa CNN wasema huenda kaburi la halaiki lipo katika Makaburi ya Kondo, Dar es Salaam

Lakini Tume pia ilifanya ukaguzi na kubaini kuwa eneo la makaburi ya Kondo limezungukwa na makazi ya watu na ambayo bado linatumika kwa shughuli za kilimo cha msimu na lina ulinzi muda wote.

Kwa upande wa ushahidi na uchunguzi wa Tume wa uandani na kuzingatia hali ilivyoonekana katika eneo la makaburi hayo pamoja na taarifa za wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi, Tume imebaini kuwa madai ya kuwepo kwa makaburi halaiki eneo la Kondo hayakuweza kuthibitishwa." - Jaji Chande

Walishondwa nini kuthibitisha siku zote hizo walikuwa wanafanya nini!!
 
Tume ya uchunguzi wa ghasia wakati na baada ya uchaguzi, imesema hakuna ushahidi uliothibitisha kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la Kondo, jijini Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande alipozungumza wakati wa halfa ya kukabiri ripoti yake mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Kutokana na ushahidi na uchunguzi wa tume wa uwandani na kuzingatia hali ilivyoonekana katika makaburi hayo, pamoja na taarifa za wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi, tume imebaini kuwa madai ya kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la kondo hayakuweza kuthibitika,” amesema.
 
Kwa hiyo hao 500 mnaosema walikufa, walizikwa wapi? Nikweli walipelekwa viwanda vya cement kuchomwa moto?

Kama Tume ingekuwa na watu wenye akili angalau kidogo, basi ingetudanganya kwamba hao 500 inaosema waliuwawa wote walizikwa na familia zao
 
Sasa km tume ni ya rais sisi inatuhusu nini si wangeitana uko mafichoni wakapeana kitu kiwe mali yake halafu kije na majibu machachu kuhusu yeye?
 
Ukisoma vizuri hayo maelezo ni kwamba hata hawakufukua hilo eneo kujiridhisha.
 
Back
Top Bottom