Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Pia hata sisi kama tunao uwezo wa kuwapiga tafu watoto wetu sio mbaya
Hata kwa wajukuu zetu kama tutakuwa na huo uwezo

Na kama ukifikiri kwa makini utagundua hata wazazi wetu walitamani sana na kujitahidi ili hata tukija kukwama kimaisha watusaidie


Kweli wapo waliotamani na kujitahidi kufanya wajibu wao. Ila wapo pia waliokimbia majukumu yao, wapo waliotegea majukumu yao na kukimbizana na ulimwengu
 
Utapinga lakini ukweli uko palepale kwamba Afrika kwa ujumla kuna kundi kubwa la vijana wanakua ilihali serikali karibia zote wala hazioni hili


Si kweli na nina pinga vikali!
Kila kitu kinakuja na mbinu zake, acha uvivu wa ubunifu wa mbinu mbali mbali za maendeleo walahi!
Aamka kijana mdogo na ujue kila unacho kiwaza kitakupata wewe na uzao wako tu walahi!
 
Haya masuala ya extended family yanaleta sana umaskini. Umepata kikazi utaona ndugu, jamaa .mpaka wazazi wanakutegemea. Unahangaika nao ukija kushtuka huna ulichofanya. Baadae wanaanza kukucheka .mara jamaa alikua na kazi nzuri hana kitu. Shida sana
Hii inatokea sana. Hasa hapo kwenye kukucheka ama kucheka wanao unapokuwa umetangulia mbele ya haki mapema.
 
Huna lolote zaidi ya roho MBAYA tu. Mzee asiyejiweza kule kijijini aliyewekeza kila kitu cha thamani maishani mwake kulea toto lenye majivuno na jeuri dizaini yako anakuwa na msaada gani zaidi ya wale aliowakuza? Kumbuka sio Ulaya hapa ambapo wazee wanatunzwa na gharama za serikali.
 
Mtoa mada asante mkuu uko vzr..! Kupitia hii mada nimegundua kuna watu wako smart sana... Nasikitika baadhi wana ufikiri hafifu.... Thnx to God Ujumbe umefika panapohusika


Mkuu Kuna watu wanadhani siwapendi wazazi wangu, wengine wanadhani huenda mapembe yamekuwa baada ya mimi kukua. Jambo ambalo si kweli. Mada hii inatuasa sisi kama vijana tuwe chachu na role model wa watoto wetu. Watoto kwa sehemu kubwa huiga wazazi wao. Endapo Baba/Mama utakuwa mvivu ukiwa kijana hii itapelekea na watoto warithi tabia hiyo hiyo.

Siku hizi kuna mashamba ya laki mbili, tatu na kuendelea. Lakini mtu mpaka anafikisha miaka 30 hana hata shamba wakati huo huo amewahi kumiliki simu zaidi ya kumi zenye thamani ya laki nane mpaka milioni moja. Akifikisha miaka 50 hana hata cha kusimulia zaidi ya kusimulia ujinga. Mara enzi hizo wadada walinikoma, sijui wanaume nilikuwa nabadilisha. Upuuzi mtupu. Mara Bar zote zilikuwa zinanijua.

Sijui kama naeleweka lakini
 
Kusaidia wazazi ni jambo jema. Lakini mzazi kutotayarisha maisha yake akitegemea kusaidiwa na watoto siku moja ni ujinga pia. Namwomba Mungu anisaidie nijitegemee wakati wa uzee wangu. Kama ni msaada uwe wa kunibeba toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kama hali ya mwili itakuwa hainiruhusu siyo msaada wa kunipa pesa ya chakula.
 


Ushasema kawekeza kwangu kwa nini asile alichowekeza. Huwezi vuna usipopanda hiyo ni kanuni katika mfumo wa maisha. Asiyefanya kazi na asile.

Kama umefika kidato cha nne huwezi shindwa elewa mantiki ya mada hii. Lakini kama madarasa ni machache huwezi kunielewa.
 
. Wakati wewe ukifanya hayo ukifikiri ndio maisha wenzako wananunua hekari tatu kwa laki tisa. Baada ya miaka ishirini unashangaa wanamiliki si chini ya heka 50 unaona kama waliiba pesa kumbe ni akili.

wapi huku mkuu hekari3 kwa laki 9
 


Mkuu umeongea vizuri sana. Mungu hawezi kujipinga hata siku moja. Biblia inasema "Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku mbaya ukasema sina raha katika haya". Kumkumbuka Mungu siku za ujana ni kushika sheria zake moja wapo ni kufanya kazi kwa bidii ukimcha Mungu. Ukimkosea Mungu Ujanani subiri uzeeni utamuelewa vizuri.

Lazima watu tufanye kazi jamani
 
. Wakati wewe ukifanya hayo ukifikiri ndio maisha wenzako wananunua hekari tatu kwa laki tisa. Baada ya miaka ishirini unashangaa wanamiliki si chini ya heka 50 unaona kama waliiba pesa kumbe ni akili.

wapi huku mkuu hekari3 kwa laki 9


Mkuu mbona sehemu nyingi tuu Hapa Tanzania. Nenda Morogoro ndani ndani. Nenda Songea huko, Sehemu ni Nyingi sana.
 
kama ndiyo tayari imeshatokea wazazi wanakutegemea utafanyaje??
Kama wazazi tayari wanakutegemea, endelea kuwasaidia. Lakini hakikisha kuwa unajiandaa wewe mwenyewe kukata mnyororo wa utegemezi kwa watoto wako. Usipowategemea watoto watoto wako na wao hawatawategemea watoto wao.
 
Sio kwa maisha haya ya kibongo maana wazazi wengi wangefata hayo wengine tusingezaliwa.

Wazazi wengi walichojitahidi ni kuwaachia watoto nyumba na elimu basi. Na wazazi wakibakia na Maisha duni ya uzeeni kutokana na nguvu nyingi wametumia kusomesha watoto na ujenzi wa nyumba
 
Umeongea bonge la point mkuu.kingine mzazi kumlea mtoto ni lazima sio ombi
 
Kk yangu jamaa kamuongelea baba kwani wababa wengi wanajisahau sana.Mama ana special respect na itabaki hivyo.Nani kama mama?
 
Sio kwa maisha haya ya kibongo maana wazazi wengi wangefata hayo wengine tusingezaliwa.


Ndio hivyo mimi mwenyewe nimezaliwa kwa mfumo huo. Silaumu. Napambana kuhakikisha sina wakumlaumu isipokuwa anayejua kusudi langu la kuwepo Duniani.

Lakini lazima nitimize wajibu wangu kama kijana, nifanye kazi kwa bidii kwani tayari Mungu ameniahidi Baraka. Jukumu langu ni kufanya kazi kwa bidii. Kuwa na nidhamu ya pesa na kila kitu, Kuulinda muda alafu Mungu yeye anaweka baraka zake. Mungu ananitegemea sana kutimiza mipango yake katika maisha yangu. Ananitaka nishike tuu sheria zake Basi.

Nikiwa kama Joka kiumbe wa zama zangu, najitahidi kumuiga Baba yangu aliyembinguni kwa kufanya katika familia yangu.
Lazima tujitahidi, tusiwe watu wakukata tamaa kwa mambo madogo. Mwanaume lazima upambane
 
Jiwe anasema tufyatue watoto.... akili za kuambiwa changanya na za kwako. Ukipata mzazi wa kukujengea nyumba na kukupa elimu bila shaka huyo anajitambua sana. Na aina ya wazazi hao hawahitaji msaada wa kununuliwa chakula na watoto wao. Wanahitaji msaada wa kupelekwa hospitali kama ni wagonjwa, ama kuvalishwa nguo kama wanakiharusi nk.
 
Kk yangu jamaa kamuongelea baba kwani wababa wengi wanajisahau sana.Mama ana special respect na itabaki hivyo.Nani kama mama?


Na nimemuongelea Baba kwani yeye ndiye aliyekabidhiwa huu ulimwengu akiwepo na Mwanamke. Sasa kufeli kwingi katika huu ulimwengu chanzo ni mwanaume. Wanaume wakiamua jambo fulani liwe linakuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…