Baba ashukuru mwanaye kufariki

Baba ashukuru mwanaye kufariki

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
156
Reaction score
191
Baba Mdogo wa Kijana anayefahamika kwa jina la Ndesa, anayedaiwa kuhusishwa na matukio ya uhalifu Jijini Arusha, amesema familia yao inashukuru kufuatia kifo cha kijana huyo kutokana na tabia zake zilizokuwa zikiwasumbua. Anazungumza katika msiba wa Kijana huyo aliyezikwa leo, Oktoba 27, 2026, Baba Mdogo huyo amedai kuwa familia ilikuwa imechoshwa na tabia za Ndesa, akieleza kuwa alikuwa akijihusisha na vitendo vya wizi, ikiwemo kuwaibia Ndugu, Wazazi na Wanafamilia wengine. “Tumemchoka, anaibia hadi familia, apumzike,” amesema Baba Mdogo wa Kijana huyo.

Mh!!! Hii ikoje wakuu 🤔 🤔 yani huu mwaka mpaka kufika hii Oktoba mwishoni huku, binafsi nimeona mengi aiseee khaaa! Sasa hata kama mtu alikua na tabia mbaya akiwa hai ndo inakua sahihi kuongea maneno kama hayo pindi anapofariki au mimi ndo nayakuza? Aah! ila hapana aiseee


​
 
Arusha huko kwa kina Yoda

Uko kwa mujibu wa Yoda ni sehemu zenye maadili kuliko pwani na dini yao ya ukristo imewasaidia.
 
Back
Top Bottom