Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)
a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa). Aidha Spika Sitta ni mwongo au hajui anenayo
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?) Aidha hakuonekana mtu, au kama alionekana mtu, basi hakuonekana kufanya kitendo anachotuhumiwa kufanya
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika. Kwa maana kwamba, kwanza kulikuwa na vumbi. Pili, vumbi hilo linaweza likawa ni sumu au si sumu. Tatu, linaweza likawa sumu isiyotambulika kwa vifaa na utaalamu uliopo Tanzania kwa sasa.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.Kwa maana kwamba, kuna kitendo kimefanyika bali si cha kishirikina. Hii inakwazana sana na (b).
case closed.