Hakuna cha Kamera, wala ushirikina - Polisi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)

a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.

Hayo yamesemwa na Kamanda huyo wa Mkoa Bw. Omar Mganga alipotoa taarifa kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge kuhusu uchunguzi huo uliofuatia matukio ya wiki chache zilizopita. Vyanzo vingine vinasema kuwa kati ya mambo yaligundulika katika uchunguzi huo ni pamoja:

a. Kamera mbili kuwa mbovu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa matengenezo na nyuingine mbili zilikuwa zimegeuzwa (tilted) ingawa sijui zilikuwa zinaangalia upande gani!
b. Na mojawapo ya madai ya kushtua kabisa ambayo wenu mtiifu ameyasikia ni kuwa baadhi ya watu wanaolipwa kuzikodolea macho hizo kamera walikuwa wameuchapa!
 
Last edited by a moderator:
Kwa mwenendo huu mafisadi hawaishi, spin six times......

-Wakapeleka mkanda mtupu, okay, kwa hilo si rahisi kuona mtu hapo.

-Walivyoanalyse vumbi walikuwa na lengo la kuona nini....sumu, sumu gani?

- Ni test gani hiyo waliyofanya na kugundua hakuna sumu ilhali hawajaweka target ni sumu gani walikuwa wakitafuta?

-Je vumbi, limeanalysiwa kwa method gani HPLC, distillation, evapotaration au?

-Je uchawi unaweza kuwa analysed scientifically?

-Mkemia mkuu anajua ushirikina unavyokuwa tested na test zimeprove hakuna ushirikina!
 
Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)

a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.

case closed.

Nani alimwaga huo unga?na maneno ya spika kwamba kuna watu wawili walionekana wakiingia ndani,hii ni ngoma nzito na ya kikubwa
 
Sasa Sitta alisemaje vile ? kuna kamera imenasa jamaa akiwanga ,sasa nani alipeleka mikanda ya kideo , apo inaonyesha jamaa wameshacheza gemu ,wamepeleka mikanda mipya.
 
...hakuna ufisadi, hakuna wizi, hakuna unga, hakuna uchawi, hakuna mkanda, hakuna nia mbaya, hakuna nia ya kuchunguza mambo kikamilifu

...hakuna hakuna hakuna hakuna x 100000000000000000000000000000

...ndiyo maana hakuna maendeleo....kazi kujiombeleza kutoka nchi matajiri zenye kuchukulia serious kila kitu!!!
 
mikanda mitupu, hakuna cha unga, hakuna aliyeonakana akiingia na kuruka ruka kwenye viti; hata maneno ya Chiligati kuwa kulikuwa na Mbunge anatafuta mahali pa kuweka makalio yake, hakuna, hata vumbi linalodaiwa kuchukuliwa Bungeni halina dalili yoyote ya kuongezwa, ni tujivumbi tule tule... put in technical terms... there is no evidence whatsoever of anything improper that warrants any further investigations.

Kesho Spika anatarajiwa kufunga mjadala huu rasmi Bungeni. No questions asked. Kama ingekuwa ni kulikimbilia daladala.. hapa ndipo unasikia konda anabamiza pembeni na kulia...."........" you know what..

halafu tunaambiwa hakuna uchawi!
 
Sasa yule mtu mweupe aliyekuwa anatafuta kiti naye pia hakuonekana?
polisi ripoti ya polisi imeonyesha jinsi walivyowataalamu kweli.
 
Maswali ni mengi kuliko majibu labda hiyo kesho ikitolewa taarifa ya kina tunaweza kujua kulikoni na kilichojiri .....hapa kuna kitu kinaweza kmutokea kikubwa na cha msikitiko.
 
Chenge ameonakana akicheka akicheka pembeni, kwani sasa hivi wakati wengine wote mmeshikilia magalasha/sa yeye kashikilia majembe kwenye karata zake... aamue tu acheze vipi.. nani awe wa kwanza kushtakiwa? Sitta, Magazeti, ...
 
Dhumuni lake liwekwe wazi maana kama ni unga wa SEMBE LA KUWATOSHA WABUNGE AMBAO WENGI WAO NI OVERWEIGHTS...Basi alitakiwa aje na Gunia kama mbili hivi na si tu unga unga!
 
Maswali ni mengi kuliko majibu labda hiyo kesho ikitolewa taarifa ya kina tunaweza kujua kulikoni na kilichojiri .....hapa kuna kitu kinaweza kmutokea kikubwa na cha msikitiko.

Kama polisi na taasisi 'zilizochunguza' unga unga na mikanda hawakuona kitu, nani mwingine atatoa ripoti ya kina?
 
Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)

a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa). Aidha Spika Sitta ni mwongo au hajui anenayo
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?) Aidha hakuonekana mtu, au kama alionekana mtu, basi hakuonekana kufanya kitendo anachotuhumiwa kufanya
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika. Kwa maana kwamba, kwanza kulikuwa na vumbi. Pili, vumbi hilo linaweza likawa ni sumu au si sumu. Tatu, linaweza likawa sumu isiyotambulika kwa vifaa na utaalamu uliopo Tanzania kwa sasa.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.Kwa maana kwamba, kuna kitendo kimefanyika bali si cha kishirikina. Hii inakwazana sana na (b).

case closed.

MM, interesting. Lakini yatafumuka tu muda si mrefu, kaa chonjo. Huyu AC kakanyaga sana vidole vya watu on his way up, wapo wengi wanamsubiri on his way down. Waliomshauri aingie siasa through ubunge walitaka atoke pale AG office maana alikuwa na nguvu za ajabu, na si kuwa walimtakia mema.
 
Nawashauri kuachana na mada hii, mtaumia vichwa bure. Tukubali tu yaishe. Tusonge mbele. Bao jingine hilo tena la kisigino.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom