Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,492
Jeshi la Polisi limetoa ripoti yake kuhusu uchunguzi wa kile kilichodaiwa vitendo vya kishirikina Bungeni karibu mwezi mmoja uliopita ambapo ilidaiwa mmojawapo wa wabunge alionekana akimwaga unga kwenye viti mbalimbali. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa (kati ya niliyoyanasa kwa haraka)
a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.
Hayo yamesemwa na Kamanda huyo wa Mkoa Bw. Omar Mganga alipotoa taarifa kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge kuhusu uchunguzi huo uliofuatia matukio ya wiki chache zilizopita. Vyanzo vingine vinasema kuwa kati ya mambo yaligundulika katika uchunguzi huo ni pamoja:
a. Kamera mbili kuwa mbovu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa matengenezo na nyuingine mbili zilikuwa zimegeuzwa (tilted) ingawa sijui zilikuwa zinaangalia upande gani!
b. Na mojawapo ya madai ya kushtua kabisa ambayo wenu mtiifu ameyasikia ni kuwa baadhi ya watu wanaolipwa kuzikodolea macho hizo kamera walikuwa wameuchapa!

Last edited by a moderator: