Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
19,371
Reaction score
14,481
Waheshimiwa Sana Wana JF, Hbr za jioni? Kama kichwa kinavyosema katika mapito niliyopitia nimegundua kuwa hakuna Binadamu "ANAYEKUPENDA KWA DHATI',. Mwenye upendo wa dhati nawe ni Mwenyezi MUNGU aliyekuumba na kukupa Pumzi na riziki na Wazazi wako tu waliokuzaa na kukulea vema.

Fuatilia visa hivi.
Mimi Nilikuwa na rafiki yangu mkubwa ambaye tulikuwa tunasaidiana ktk shida na raha, Lakini kuna wakati nilikuja kuyumba Sana kimaisha jamaa alikuwa vizuri, Siku moja nikaomba anikopeshe 50,000/= (Elfu hamsini tu),jamaa alikataa kunikopesha kuwa hana Hela wakati huo Mimi najua jamaa ana pesa kwasababu yeye mwenyewe alikuwa anasema kuhusu mipango yake na baada ya hapo akaanza kupunguza mawasiliano na ukaribu.

Rafiki zangu wengine waliacha kabisa kuwasiliana na Mimi, wakati nilipokuwa na hali nzuri kiuchumi walikuwa ni watu safi sana wakionyesha kuwa Wana upendo wa dhati kwangu, Kumbe sivyo.

Kisa kingine ni Cha mdogo wangu,huyu alipatwa na matatizo makubwa hadi kufungwa jera,aisee marafiki zake aliokuwa akijidai nao kuwa oh!, Mimi Nina rafiki wengi tulioshibana, aisee walijiweka mbali sana na shida hiyo hata kwenda gerezani hawakwenda,hata kuulizia tu maendeleo yake hawakuthubutu kabisa.Alipotoka ndio wakawa wanakuja kwa aibu wanasema eti "Tuliogopa kuja gerezani", Wengine wakasema "Tulikuwa na mpango wa kuja baadaye", wakati mtu amekaa jera miezi minne.

Hitimisho
Ndugu yangu/zangu ukiwa vizuri kimaisha,kwa maana ya kazi nzuri, biashara nzuri,cheo kizuri,n.k.Usije ukalewa sifa kutoka kwa rafiki zako hao wanakupendea nafasi uliyonayo na si wewe, ukitaka kuthibitisha hilo hebu pata msukosuko kidogo uone jinsi jamaa zako watakavyotoka nduki.

Hivyo ushauri wangu ukiwa na nafasi nzuri jari kwanza Wazazi wako,Famili Yako,Bila kumsahau Mwenyezi MUNGU;Km unataka kumsaidia mtu msaidie tu km Ibada tu na si kutegemea kurudishiwa fadhila. Kuwa na Marafiki ni kitu kizuri lakini uwe mwangalifu,ishi nao huku ukijua wazi kuwa siku mambo yakikuendea mrama lazima hao marafiki zako wakukimbie au wakusaliti.Tujifunze pia kupitia kwa Yesu namna Wanafunzi wake walivyomkwepa wakati wa Mateso yake.
 
huwa naamini katika mimi mwenyewe hakuna wa kunipa msaada zaidi yangu mimi mwenyewe na aliyeniumba
Mkuu kuna wakati hata uwe na kila kitu au uwe na uwezo vipi,lkn utahitaji tu msaada kutoka kwa mtu mwingine.Fikiri mfano upo gerezani utawezaje kutoka bila kumtegemea ndugu yako wa Karibu au mzazi wako au mkeo?.
 
Tumesha sema na tunarudia kusema marafiki unaokutana nao ukiwa umeshafanikiwa au mmekutana nao kazini hao kuwa nao Makin wengi wao siyo marafiki maana siku ukianguka au ukapoteza kazi Basi na urafiki wenu utakua umeishia hapo na mazoea hatataka kabisa.

Jaribu kufikiria kipindi ukiwa haujafanikiwa au ulipokua hauna kazi kuna marafiki hata kama siyo wengi basi Kuna rafiki ambae alikua mtu wako wa karibu na alishakusaidia mambo flanflan hata kama siyo ya kipesa lakin hata ushauri wake au alikupa moyo ukiwa kwenye majaribu fulani , hao ndo wanakuaga marafiki wa kweli lakin kwa bahat mbaya huwa tukifanikiwa kidogo huwa tunawatupa hata Salam tunakata na badae tunaanzisha urafiki na watu fake.

Marafiki weng wa kazn urafiki wao huwa unakuzwa sana nyakati za starehe na pombe, ukiweza kujitenga na pombe au mambo ya starehe hapo kazin kwenu hautakua na rafiki wa karibu hata mmoja isipokua utabak urafiki wa kukutana ofisin tu.
 
Back
Top Bottom