Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Status
Not open for further replies.
Nilijua spika wenu ataahirisha bunge kabla ya muda mara baada ya Muhongo kujikanganya mwishoni, na ndivyo ilivyotokea,ilikuwa bado 30 hadi 40 hivi,

kiti kilikuwa cha moto hadi nilimuonea huruma...
ila nimeamini maneno ya Yeriko ndugai angeangusha rekali mapema mno kama angeachwa na mafisadi wangekoma!!
 
Na sasa hv sio wajiuzuru tu bali hela zetu warudishe na RIBA juu

Katika ripoti ya Zitto, escrow ilitakiwa walipwe b 306, wamelipwa b 182 tu, kwenye post namba nikuulize ziko wapi? Na ni kasema jibu "kesho" litapatikana, naam, leo jibu limepatikana, umelisikia?
 
JL ana haki ya kumpa fedha yake yoyote amtakae, mbona Zitto hajataja fedha alizowapa mabinti zake?

Unajuwaje wana biashara zao zipi? na Tanzania si haramu kufanya biashara mbunge au waziri au hata kugawa kwa yeyote umtakae.

Hoja mama ya Uzi wako inayo mantiki kwa mwenye lengo la kujifunza na kwa mwenye mtazamo chanya wa kubishana kwa hoja -Na kiukweli hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa.

Hata hivyo majibu yako kwa wanaoona kama huko sawa yanaonyesha ama umebahatisha kuja na hoja hii na pengine hukuandika mwenyewe au kusudi tu umeamua kujiwehusha na kujifanya hamnazo.

Lakini kwa kuwa tunahitaji kuvumiliana ili tuelimishane;
Tafadhali nijibu maswali yangu haya ili tuweze kwenda sawa.

Ni ukweli uliowazi kuwa watu wanaweza kuwa na biashara zao ambazo pengine wengine hazituhusu na si kazi yetu kuzijua na hivyo tungepaswa kuwaacha wenyewe.

Lakini vipi kuhusu Mama ambae ni waziri aliekiri mchana kweupe kupokea Pesa Tshs. 1.6 B iliyothibitishwa na ushahidi ambao ninaimani hata wewe umeuona lakini yeye akijitetea kuwa ilikuwa imekusudiwa kama mchango kwa taasisis yake ya shule huko kwao?
-Na vipi kwa viongozi wa kidini ambao wao bado hatujapata kauli zao lakini ushahidi upo kuwa walipokea mgao huo?

Binafsi sitaki kuamini kuwa ni-wachuuzi hawa lakini,
Tuwafanyie haki stahili sisi kama watanzania tuwajadiliwa wao pia.

Maswali yangu ya msingi kwako:
1.Kwanini pesa iliyokusudiwa kama mchango wa taasisi ipitie kwenye akaunti ya mtu binafsi badala ya akaunti ya taasisi anayoisimamia au kuiongoza?
2.Unataka kuniambia taasisi wanazoziongoza hazina akaunti?

Nawasilisha.
 
Dah wamechota helaaa na magunia mifuko ya rambo viroba mm nlikua wapi dah, wana bahati ningeenda na scania yenye tela sitak tabu
 
Huyu hawezi kuwa na uchungu kwanza si raia ni msomali huyu ndiyo maana kazi yake kusifia chin ja chinja na madudu yote
Tuondoe umimi, ubinafsi na ubaguzi kiujumla,
Hapa zinazungumzwa hoja sio watu.
Kwa taarifa tu hata hili sakata kuanza na kuendelea kwake hadi ulipo uwezekano mkubwa tu wa kuwepo kwa mkono wa inchi za mbali zizinazoitakia nchi hii mema,
Lakini huo ni mjadala mwingine kabisa.
 
Tuondoe umimi, ubinafsi na ubaguzi kiujumla,
Hapa zinazungumzwa hoja sio watu.
Kwa taarifa tu hata hili sakata kuanza na kuendelea kwake hadi upo uwezekano mkubwa tu wa kuwepo kwa mkono wa inchi za mbali zizinazoitakia nchi hii mema,
Lakini huo ni mjadala mwingine kabisa.

hakuna ubaguzi hapa this is fact,huruma yetu imetuponza sana ona Singasinga toka india anavyotuhenyesha na ni hawahawa kila siku , Angalia Richmond na kagoda kina Rostam Aziz ni walewale tu .
 
Huyu hawezi kuwa na uchungu kwanza si raia ni msomali huyu ndiyo maana kazi yake kusifia chin ja chinja na madudu yote

Nisome post namba moja niliiandika jana, halafu umemsikiliza Mhongo?

Kaachia ngazi?
 
hakuna ubaguzi hapa this is fact,huruma yetu imetuponza sana ona Singasinga toka india anavyotuhenyesha na ni hawahawa kila siku , Angalia Richmond na kagoda kina Rostam Aziz ni walewale tu .

Singa singa hakuhenyeshi unajihenyesha wewe mwenyewe kwa kuwa na mawazo duni, Singa singa kisha ahidi anaibadilisha hiyo mitambo na atashusha bei za umeme, na nnamuaminia.
 
Hoja mama ya Uzi wako inayo mantiki kwa mwenye lengo la kujifunza na kwa mwenye mtazamo chanya wa kubishana kwa hoja -Na kiukweli hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa.

Hata hivyo majibu yako kwa wanaoona kama huko sawa yanaonyesha ama umebahatisha kuja na hoja hii na pengine hukuandika mwenyewe au kusudi tu umeamua kujiwehusha na kujifanya hamnazo.

Lakini kwa kuwa tunahitaji kuvumiliana ili tuelimishane;
Tafadhali nijibu maswali yangu haya ili tuweze kwenda sawa.

Ni ukweli uliowazi kuwa watu wanaweza kuwa na biashara zao ambazo pengine wengine hazituhusu na si kazi yetu kuzijua na hivyo tungepaswa kuwaacha wenyewe.

Lakini vipi kuhusu Mama ambae ni waziri aliekiri mchana kweupe kupokea Pesa Tshs. 1.6 B iliyothibitishwa na ushahidi ambao ninaimani hata wewe umeuona lakini yeye akijitetea kuwa ilikuwa imekusudiwa kama mchango kwa taasisis yake ya shule huko kwao?
-Na vipi kwa viongozi wa kidini ambao wao bado hatujapata kauli zao lakini ushahidi upo kuwa walipokea mgao huo?

Binafsi sitaki kuamini kuwa ni-wachuuzi hawa lakini,
Tuwafanyie haki stahili sisi kama watanzania tuwajadiliwa wao pia.

Maswali yangu ya msingi kwako:
1.Kwanini pesa iliyokusudiwa kama mchango wa taasisi ipitie kwenye akaunti ya mtu binafsi badala ya akaunti ya taasisi anayoisimamia au kuiongoza?
2.Unataka kuniambia taasisi wanazoziongoza hazina akaunti?

Nawasilisha.

Nimeshaijibu hilo swali la huyo mama aliyepewa 1.6b humuhumu kwenye hii post zunguka zunguka utaliona na mimi nikiliona ntakuja kukubanduikia.

1 na 2. Convenience na prestige, huwajui Wahaya?
 
Itafikia wakati Watz wanaweza beba mitutu ili kuikomboa nchi yao. Kwani kuna nchi zilianza hivi hivi na jeshi halikufua dafu.

Kauli za mafisadi zina mwisho na mwisho wake utategemea muamko wa Wananchi wa Tanzania.

Hakika watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom