Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,339
- 3,674
Habarini wapendwa
Ni siku nyingine tena ya wana mmu kuwepo ndani ya jukwaa letu pendwa kupeana habari mbalimbali zinazotuelimisha na kutuburudisha.
Leo ninalo hili wana MMU,ni hili suala la mwonekano mzuri na mwaonekano mbaya wa mtu mmoja mmoja,kiukweli kuna mionekano tofauti tofauti hapa duniani na kila mmoja na mwonekano wake aliopewa na muumba wetu Mungu.
Kuna wale ambao kwa kweli ni mashalaahh yaani wamejaaliwa na mungu na kwa kweli wana mwonekano mzuri sana na wala huwezi kusita kukubali kuwa mtu huyo ni mzuri mara tu umtiapo machoni,hongera kama uko kundi hili na umshukuru muumba wako.
Na wapo pia wenye mwonekano mzuri wa wastani na pia wapo wale ambao labda hawakujaaliwa kuwa na mwonekano mzuri sana na hivyo kutokana na mapungufu tuliyonayo wandamu huishia kuponda au kusema ni wabaya au wana sura mbaya.
Swala linakuja hapa kuna baadhi ya watu waliojaaliwa mwonekano mzuri sana au hata wa wastani au wenye dharau tu kiasili kuwa na tabia ya kuwadharau na kuwashusha kabisa wale ambao hawakujaaliwa mwonekano mzuri wa kutukuka,kazi zao ni kuwasema,kuwanyanyapaa kuwaepuka na kuwakosoa kila wakati na kuwaona kama sio binadamu wanaostahili kupendwa na kuthaminiwa,mpaka kuna baadhi yao wakiona watu wa namna hiyo wamepata wapenzi wao huanza kuwakosoa wale wapenzi wao kwa maneno ya kejeli kama:
"hivi ulikosa nini mpaka ukaamua kuwa na huyo mtu"?au "umezunguka hapo ndo ukafika mwisho"?
jambo ambalo limekuwa likiwakosesha raha watu wa namna hiyo na kujiona wasiofaa kitu na kukaa kwa kujihisi mara kwa mara na kukosa kujiamini.
Sasa kwako wewe uliye na tabia kama hiyo em tua kidogo ujiulize haya:
1.wewe ulijiumba ukajipa huo uzuri ulio nao?
2.hao unaowaona wewe kuwa ni wabaya walijiumba,walipenda kuwa hivyo walivyo?
3.wewe una mapungufu mangapi kwenye mwili wako ambayo huyapendi?vipi ulipenda kuwa nayo au ulijiumbia wewe?ungekuwa umejiumba si ungeyatoa basi?
4.unajua kuwa uwezekano wa wewe pia kuwa na mwonekano mbaya ulikuwepo kwa kuwa sio wewe uliyejiumba? muumbaji wa watu wote angeweza na anaweza hata sasa akaamua ukawa na mwonekano wa huyo unayemwona kuwa mbaya?
5.assume wewe ndo huyo unayemwona mbaya ungejisikiaje kama ungekuwa unanyanyapaliwa na kudharaulika na kuepukwa kwa jambo ambalo hata wewe hukupenda liwepo?
6.ukoo wenu mzima wamejaaliwa kuwa mashaalaaahh?
ikiwa sio pengine hata mama au baba yako hana mwonekano mzuri ni wewe tu umeangukiwa na hiyo ngekewa pengine dada kaka mjomba bibi binamu au shangazi hana mwonekano mzuri,je hao pia utawadharau,utawanyanyapaa utawaepuka?
ikiwa hutawadharau kwa kuwa ni ndugu zako,utajisikiaje ikiwa utajua kuwa wanatendewa vibaya na watu wengine kwa ajili ya mwonekano wao?
utawaonaje watu wanaowatendea vibaya ndugu zako vibaya kwa ajili tu ya mwonekano wao?
7.pengine kwa sasa wewe ni bachela hujazaa,haya umekuja kuzaa mtoto huyo mwonekano kama wa huyo unayemwona kuwa ni mbaya,je utamtupa?
utamnynyapaa?
utamtenga?
utapenda wengine pia wamtenge?
utapenda akipata mume/mke au mpenzi wamkejeli Yule aliye naye kwa ajili ya mwonekano wake?
Nadhani kila mmoja ana majibu yake kichwani
Kwa kuhitimisha,ukweli ni kwamba hakuna aliyejiumba hakuna aliyejipa ubaya au uzuri hakuna aliyejipa kasoro za mwili alizonazo,sote tumeumbwa na Mungu yeye ndiye aliyetuumba na kama ni ubaya au uzuri basi jua Mungu ndivyo alivyokuumba.
Kwa hiyo basi somo hapa ni:
Tuache hizi tabia za kuwadharau na kuwashusha watu kwa ajili ya mionekano yao na kwa:
wewe uliyejaaliwa uzuri wa kutukuka na muumba mshukuru muumba wako kwa kukujaalia mwonekano mzuri na uwaonee huruma wale ambao hakujaaliwa kama wewe ulivyojaaliwa na sio kutumia uzuri wako kuwadharau wengine na kuwaona wasiofaa kitu,hata wao hawakupenda kuwa hivyo walivyo kama kungekuwa na aliyejiumba nadhani kila mmoja wetu angeondoa kasoro zote alizonazo mwilini mwake kama vile ufupi wa kupita kiasi,urefu wa kupita kiasi,unene,wembemba,weusi,weupe na kasoro nyingine nyingi tulizonazo miilini mwetu.lakini kwa kuwa hatujiumbi basi tunakaa tu na kasoro zetu za mwili hata ikiwa hatuzipendi.
Kila mmoja ana haki ya kupendwa kupenda na kuthaminiwa ukimdharau huyo unayemwona mbaya na ukitaka wengine pia wamwone kama wewe unavyomwona unataka akajifiche wapi?je hastahili kuishi?
Si vibaya kuwasifu wenzetu waliojaaliwa na muumba na wala hulazimishwi kukubaliana kuwa kila mmoja ana mwonekano mzuri,ruksa kuona huyu mzuri huyu si mzuri kwa mtazamo wako lakini jambo baya hapa ni kuanza kuwabagua,kuwanyanyapaa,kuwatenga na hata kuwashawishi wengine wamwone mbaya kama wewe unavyomwona,kama wewe unamwona mbaya basi kaa nalo moyoni mwako usiwashawishi wengine wamwone hivyo pia wapo wanaomwona kuwa ana mwonekano mzuri.
Samahanini kwa hotuba ndefu sana lakini ilinibidi kuandika yote niliyoyaandika,karibuni nawasilisha wana MMU.
copy😡Himidini TetraPetCashKaunga @FixedPoint BAK @MrRocky AshaDiiSnowBallgfsonwinMwanajamiiOnesaudariMamdenyi nyumbakubwa KOKUTONAladyfurahiapassionlady grafani11@Eiyer ExcelTamatheomwekunduTaiJike na wengine wote karibuni.