Hakimu mwakenjwa kukumbukwa daima!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakimu mwakenjwa kukumbukwa daima!!!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Dec 2, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  huyu ni yule hakimu aliewaduwaza mawaziri wetu sijui tuite wastaafu maana walinyofolewa kutok uongozini!!!pongezi hakimu mwakenja kwa kuheshimu sheria ,nimeona kamam mmoja wa wadau wa sheria ni vyema kuwaheshimu wale wanaoheshimusheria za nchi bila kufwata wala kuendekeza nidhamu ya uoga haswa pale kwenye kutenda haki kwa biinadamu!!!
  aluta kontinua na nyie wakina hakimu eugne mingi na wengineo waambie watu wafwate sheria kurudi kijijini ni mapenzi ya mungu msiwaumize wananchi wa kawaida kwa kuwaomba pesa !!!
  haki bila pesa inawezekana:::
  Hakimu awaduwaza Mramba na Yona  Na Grace Michael

  MAWAZIRI waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambao wanakabiliwa na kesi ya kuliingizia Taifa hasara, Bw. Basil Mramba na Bw. Daniel Yona jana walikumbwa na bumbuwazi baada ya matarajio yao ya kutoka nje kwa dhamana baada ya wiki moja ya kukaa gereza la Keko kutoweka baada ya Hakimu kukataa kushughulikia suala lao.

  Hali hiyo iliyowaduwaza ndugu, jamaa na marafiki wa mawaziri hao waliofurika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamejiandaa kuwalaki wapendwa wao, ilitokea katika mazingi yaliyowafanya wengi kutoamini-ilikuwa bayana kuwa baada ya kupunguziwa mashrti ya dhamana na Mahakama Kuu Ijumaa, watuhumiwa hao jana wangekuwa nje.

  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Hezron Mwankenja alifikia uamuzi wa kugoma kuingia mahakamani kuanza kushughulikia mchakato wa dhamana ya washitakiwa hao, baada ya kubaini kuwa Mramba na Yona walifikishwa mahakamani hapo kutoka gereza la Keko bila kuwepo hati ya kisheria ya kuwatoa watuhumkiwa walioko mahabusu kabla ya tarehe yao rasmi (removal order).

  Baada ya kubainika kasoro hiyo Majira lilishuhudia vuta nikuvute kati ya mawakili wa washitakiwa na Hakimu huyo kujaribu kumshawashi akubali kuendelea kuisikiliza kesi hiyo bila mafanikio.

  Habari zinasema kuwa baadaye Hakimu huyo alikubali kusikiliza kesi hiyo iwapo pamoja na kukosekana hati hiyo ya kuwatoa washitakiwa gerezani, kwenye jalada hilo la kesi kungekuwa na amri ya Jaji inayomtaka kusikiliza kesi hiyo, amri ambayo nayo ilikosekana lilipofunguliwa jalada la kesi hiyo lililitoka Mahakama Kuu.

  Hakimu Mwankenja alionekana kushikilia msimamo wake huo na hivyo washitakiwa hao wakalazimika kupanda karandinga kurejea gereza la Keko, huku gari walimopanda vigogo wakiwa pia wamepanda watuhumiwa wa ujambazi ambao ulitokea kwenye taa za kuongozea magari za Ubungo, Dar es Salaam.

  Akifafanua kuhusu kilichotokea hadi akafikia kuchukua uamuzi huo, Bw. Mwankenja alisema asingeweza kupindisha taratibu za kisheria kwa kuendesha kesi bila kuwepo hati hiyo ambayo alisema ndiyo inayomwongoza kutambua kuwa ana kesi kama hiyo kwa siku hiyo.

  "Bila kufuata utaratibu unaotakiwa hatutaweza kufanya kazi, kitu kilichotakiwa ni wao kuandika barua ya maombi ya kuwaleta washitakiwa hao leo mahakamani na ikasainiwa, lakini bila hivyo tutakuwa tumevunja utaratibu na mbali na hilo pia hata jalada halioneshi elekezo lolote," alisisitiza Hakimu Mwankenja.

  Aidha alisema kuwa hata mawakili wa upande wa utetezi walikiri kuwepo upungufu huo katika kufuata utaratibu wa kuwaleta washitakiwa hao mahakamani hapo.

  Uchunguzi uliofanywa na Majira mahakamani hapo ulionesha kuwa mawakili wa Mramba na Yona walimsihi sana Hakimu huyo akubali kushughulikia dhamana hiyo bila mafanikio.

  Hakimu Mwankenja alisisitiza kuwa kisheria hakuweza kutambua uhalali au sababu za washitakiwa hao kuwepo bila hati hiyo.

  "Kama hao washitakiwa wapo basi watakuwa na mambo mengine sijapokea maombi yoyote yakiomba kuletwa kwao hapa lakini pia hakuna maelekezo yoyote kwa maandishi ambayo yananitaka kufanya hivyo kwa hiyo haitawezekana, kinachotakiwa ni taratibu kufuatwa kwa mujibu wa sheria," alisema Bw. Mwankenja.

  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja bila kuwepo hati hiyo watuhumiwa waliruhusiwa vipi kutoka gereza la Keko, kwani kiutaratibu, kanuni za magereza haziruhusu kutolewa mahabusu aliyeko gerezani kabla ya tarehe yake rasmi bila kuwepo hati hiyo.Swali ni je, washitakiwa hao jana walitolewa vipi gerezani hapo?

  Akitotoa ufafanuzi wa kisheria kwa gazeti hili katika mahojiano kwa njia ya simu jana, wakili mashuhuri jijini Dar es Salaam, Bw. Damas Ndumbaro alisema kimsingi hati hiyo ya kuruhusu mahabusu atolewe gerezani haipo katika tamko lolote la kisheria za Tanzania bali ni utaratibu uliowekwa kwa siku nyingi na mahakama.

  "Utaratibu huo haujatajwa katika CPA (Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai) ila ni utamaduni wa muda mrefu wa kuomba mshitakiwa aliye mahabusu kufikishwa mahakamani kabla au nje ya tarehe ambayo kesi yake imepangwa katika kalenda ya kawaida ya mahakama.

  "Ni hati ya muhimu sana kisheria kwa sababu inawasaidia hata watu wa magereza kwa kuwa inasainiwa na Hakimu husika au Jaji, kufahamu kuwa mahabusu fulani anatakiwa mahakamani kihalali.

  Kwa kweli bila hiyo kiutaratibu huwa magereza hawaruhusu mtu kutolewa, sasa nani aliwatoa bila ruhusa, hiyo ni kashifa. Ila Hakimu alikuwa sahihi kiutaratibu," alisema Bw. Ndumbaro ambaye amekuwa kwenye jopo la utetezi katika mashitaka kadhaa mashuhuriu ya jinai nchini.

  Kufuatia dhamana hiyo kushindikana na watuhumiwa kurejeshwa gereza la Keko nyuso za huzuni zilitawala tena mahakamani hapo, ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao wakiendelea kutoamini makali ya taratibu za kisheria.

  Washitakiwa watafikishwa tena leo mahakamani hapo wakati kesi yao itakapokuwa ikitajwa kwa ajili ya h
   
 2. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Good start, lakini asiishie kwenye kudai removal order tu. Kama itathibitika kuwa hao Mramba na Yona wana kesi ya kujibu awalambe mvua za kutosha tu sio kufanya usaniii...
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sheria ni msumeno.......!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Haswaaaaaa!!!!!!!!!!tuombe mungu hakimu asibadilishwe!!
   
 5. share

  share JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Huu ni wakati wa kuvuna kwa mahakimu who do not respect their judicial profession. Watatengeneza ka-EPA kao nao. Hakimu asiyeikubali hako kaEPA ataanza kupata vimemo vya vitisho. Let's pray that Mwakenjwa may not become corrupt ili atutendee haki kwa wezi wetu. Kula nyasi tumechoka. The national cake is for us all.
   
 6. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kazi kweli kweli
   
 7. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #7
  Dec 3, 2008
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  washitakiwe walihusika kuwatoa gerezani na walipe gharama au?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Katika mahakimu wanaoheshimiwa katika TZ hii Mwankenja yumo tena no 1......hapindishi sheria na hana kashfa kupokea hata sh 1 ya mtu....hata PCCB wanamtambua na wanamjuaa sana ....na serikali pia inamtambua.....kwa taarifa tu vilaza...wote waliokuwepo hapo kisutu kabsa kesi ufisadi kuanza wamehamishwa.......wote wameletwa wenye profile nzuri na wachapakazi......
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  .....Naomba Mwankenja usisite kuwafunga hawa......................
  Wasije na janja janja yao. Kama walileta kesi kutupiga changa la macho wewe tafuta kakifungu kengine ka kuwabamiza ukonga.
  Angalau rufaa ndio iwanyofoe huko....Unasikia mkuu????????
   
 10. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa nini hawakushtakiwa na sheria ya sokoine ( Kuhujumu Uchumi-1984). Hili wakae ndani under unbailable offense. Au hiyo sheria( kifungu cha dhamana) kilishatangazwa kuwa kinasigina katiba? Mama mia ebu niabarishe kidogo katika hili.

  Shadow
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Keep it up Mwankenja mungu atakulinda na hila mbaya za mafisadi as sheria ni msumeno.
   
 12. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Fisadiz wakishakula mvua hapo ndipo tunaweza kutoa pongezi. Tofauti na hapo hii naona kama ni movie tu kama zingine ambazo sterling mara nyingi hauawi wala kufungwa mwishoni mwa SINEMA. Nyie subirini mtakachosikia baada ya uchaguzi Mkuu ujao. Watch.
   
 13. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakati mnamsifu Hakimu mwakenjwa, pia tumkumbuke Jaji Lusekelo Kyando (RIP) ambaye alifariki ghafla baada ya kuamua kesi ya uchaguzi wa mufti wa Tanzania.

  Jaji Kyando alitoa maamuzi ya haki bila kujua kuwa wale watakaoshindwa watammaliza.

  RIP Jaji Lusekelo Kyando
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Leo hii wamekubaliwa kwenda kuchukua pesa zao walizopeleka na kudai dhamana ilikuwa kubwa mno,,mnayajua haya
   
 15. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwakenja mwakenja mwakenja......Mzee wa makamo, nafikiri uta act kisheria zaidi,usijekuwa mwana mtandao!
   
Loading...