Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Hapo ndio tunatofautiana kuelewa mambo. kazi ya kuhakiki watumishi hewa kwa vyovyote vile ilifanywa na kamati maalumu ambao ni wasaidizi wa mkuu wa mkoa. sasa kama kamati uliyo iteua hujawaamin ukaenda kuhakiki mwenyewe sasa kuna sababu gani ya kuwa na RAS, Wakurugenzi wa Halmashauri na wengineo? Ni sawa na kusema Rais akipewa taarifa say na TAKUKURU AU CAG aende tena kuhakiki taarifa zile. mimi ninge muelewa kama angewafukuza wasaidizi wa mkuu wa mkoa wote kwa kumpelekea taarifa za uongo.

Mkuu suala hapa ni content ya taarifa unayopewa. Kabla hujapewa taarifa huwa kuna mategemeo fulani ambayo wewe uliyeunda hiyo tume unategemea, sasa pale inapokuja taarifa unakuta mategemeo yale ni 0%, lazima kengere igonge kichwani na hapo ndo inakupasa ufanye uhakiki, ndicho Magufuli alichofanya na ndicho Mkuu wa mkoa alitakiwa kufanya.

Huwezi kua unafanya uhakiki kwa kila taarifa.
 
siku moja uwe kiongozi halafu uige staili hii uone utakavyo baki peke yako. kimsingi wote hatupendi uzembe kazi, lakini je, inawezekana mkuu wa mkoa kupita kuhakiki taarifa alizo pewa na wasaidizi wake? mimi ninge muelewa kama angewaadhibu wakurugenzi na wakuu wa idara walio mpa Mkuu wa mkoa taarifa za uongo.
Nina hofu na thinking capacity yako. Kwahiyo ukiwa boss kaziyako nikupokea report tu bila kuzifanyia uhakiku?
 
Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Gazeti la Habari Leo: 15 Machi 2016

RAIS Dk John Pombe Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni na kuwapa maagizo mazito. Rais amewaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za wananchi na sio kwenda kufanya siasa. Katika hotuba yake fupi kwao, Rais amewapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.

Ameonya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi mwenyewe. Vilevile Rais amewaagiza mawaziri wotw kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.

Rais ameeleza matumaini yake kuwa kupitia kwa wakuu hao wa mikoa, kero nyingi zitamalizwa na wananchi watakuwa huru katika nchi yao. Baadhi ya kero ambazo Rais amezigusia ni migogoro ya wafugaji na wakulima, ukosefu wa usalama barabarani hadi mabasi kusindikizwa na polisi pamoja na tatizo la njaa.​

Pia kupitia blog ya ikulu, imewekwa video yenye hotuba yote ya Mh. Rais pindi akiwaapisha wakuu wa mikoa. Kama hukuiona basi itazame hapa chini na uisikilize uielewe.

​


Sasa kama utakaa chini na kuitafakari hotuba ya mheshimiwa Rais basi hutakuja na post yako ya kijinga kama hii uliyoileta. Ieleweke wazi kwamba Mh. Rais akisema kitu anamaanisha, na akitoa maagizo yanatakiwa kutekelezwa. Hii si awamu ya kutafuta visingizio, bali ni awamu ya kufanya kazi.
 
Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza kifamilia au kikampuni kiwe cha serikali au binafsi.
Magufuli ni mkali kupindukia kwa majipu,wezi,wavivu, watu wasiowajibika,wasio wabunifu na ambao kazi zao ni kumpelekea raisi taarifa za uongo ambazo hawajazihakiki wenyewe kabla ya kuzipeleka.

Siku njema huonekana asubuhi.Sasa mtu kama kamteua siku chache tu keshaanza kumpelekea taarifa za uongo unategemea amleee?

Ukipewa kazi yoyote kuna kipindi cha matazamio (probation period) Ukileta uzembe katika siku hizo uwe umekaa siku moja ,mbili au 20 utatolewa mkuku kama mbwa.

Mtu akiona stahili ya Magufuli hawezi keshasema ajiondoe mwenyewe kabla hajamng`oa
Naunga mkono hoja ya Magufuli 100%, lkn napinga kusema kuendesha nchi sio kama ku run a company. Waziri Mkuu wa MALAYSIA alifanikiwa kuinyanyua nchi yake mpk pale ilipo kwa sababu hii "HE WAS RUNNING THE COUNTRY LIKE CEO" nadhani umeona MALAYSIA ilipo Sasa. So MH.JPM go go go
 
Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show

Wewe uliwahi kuongoza nini ili hili bandiko lako tulichukulie kama case study?! Mbona hutupi tathmini yako ya athari ya aina ya kiongozi mpole; anayejitekenya na kuchekacheka kama zuzu na vijembe, mipasho na kejeli kibao?!
Nchi inahitaji mabadiliko ya mindsets; JPM is the right man for that role, asiyetaka tutambomoa au aache kazi. RC kumdanganya mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu wewe unaita kosa dogo?! You must have taken leave of your faculties! Muone daktari wa afya ya ubongo! Bs
 
Gazeti la Habari Leo: 15 Machi 2016
RAIS Dk John Pombe Magufuli amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni na kuwapa maagizo mazito. Rais amewaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za wananchi na sio kwenda kufanya siasa. Katika hotuba yake fupi kwao, Rais amewapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.

Ameonya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi mwenyewe. Vilevile Rais amewaagiza mawaziri wotw kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.

Rais ameeleza matumaini yake kuwa kupitia kwa wakuu hao wa mikoa, kero nyingi zitamalizwa na wananchi watakuwa huru katika nchi yao. Baadhi ya kero ambazo Rais amezigusia ni migogoro ya wafugaji na wakulima, ukosefu wa usalama barabarani hadi mabasi kusindikizwa na polisi pamoja na tatizo la njaa.​

Pia kupitia blog ya ikulu, imewekwa video yenye hotuba yote ya Mh. Rais pindi akiwaapisha wakuu wa mikoa. Kama hukuiona basi itazame hapa chini na uisikilize uielewe.

​


Sasa kama utakaa chini na kuitafakari hotuba ya mheshimiwa Rais basi hutakuja na post yako ya kijinga kama hii uliyoileta. Ieleweke wazi kwamba Mh. Rais akisema kitu anamaanisha, na akitoa maagizo yanatakiwa kutekelezwa. Hii si awamu ya kutafuta visingizio, bali ni awamu ya kufanya kazi.

Mleta mada ni mpenzi wa mkwere; mzee wa kujitekenya na kuchekacheka mwenyewe; na mnufaika wa mitandao ya kifisadi ya enzi hizo!
 
Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza kifamilia au kikampuni kiwe cha serikali au binafsi.
Magufuli ni mkali kupindukia kwa majipu,wezi,wavivu, watu wasiowajibika,wasio wabunifu na ambao kazi zao ni kumpelekea raisi taarifa za uongo ambazo hawajazihakiki wenyewe kabla ya kuzipeleka.

Siku njema huonekana asubuhi.Sasa mtu kama kamteua siku chache tu keshaanza kumpelekea taarifa za uongo unategemea amleee?

Ukipewa kazi yoyote kuna kipindi cha matazamio (probation period) Ukileta uzembe katika siku hizo uwe umekaa siku moja ,mbili au 20 utatolewa mkuku kama mbwa.

Mtu akiona stahili ya Magufuli hawezi keshasema ajiondoe mwenyewe kabla hajamng`oa
Serikali ya JPM haina probation period ......!!!!
 
Kuna siku atajikuta yuko peke yake. Dalili zinaonesha mawaziri wake wengi wameingiwa uoga fulani na ndio maana siku hizi siwasikii sana kama mwanzo. Juzi nilijiuliza hivi Makamba JR yupo? Jenista Mhagama? Zaidi ya nusu ya mawaziri wake wako kimya wanaogopa kutumbuliwa, wanasubiri watumwe tu na bosi wao.
Bwana lemutuz hebu tulia Rais afanye kazi tuliyomtuma
 
Mtoa hoja kosa la kusema URONGO si kosa dogo, tena mbaya zaidi unamdanganya Rais wa nchi, Kheri umdanganye mumeo or mkeo. JPM upo sahihi wanyooshe ili mindset zao zikae sawa, walizoea kufanya kazi kwa mazoea, na mazoea yana madhara yake. Kama mtu hawazi akae pembeni tupo wengi tu huku uswazi tunazihitaji hizo positions. Ndugu kama unasubiri anguko la JPM kama ramri zako zilivyosoma basi utazeeka na usilione.
 
JPM anasema Nchi ilikuwa imeoza kila siku, na yeye akiwemo kwa serikali hiyo hiyo, sasa kumbe muongo mmoja uliyopita ulikuwa wa kula na kusaza na kutumbua pamoja na kuzuru kaburi la Bob Maley na kumbembea. JPM kwa sasa anafanya propaganda, na kujaribu kutawala so mimi nitamkosoa, kumpinga na kumpongeza. Na mimi kumwamini kuwa ndiye kiongozi au mtawala ninayemtaka na kujifunza kwake, Nampa uangalizi binafsi wa miaka 3.
 
Bwana lemutuz hebu tulia Rais afanye kazi tuliyomtuma
Mimi siyo Le mutuzkama unavyofikiria, bali ni mtanzania ninae tetea walionewa. Hivi karibuni nilitoa post iliyo kuwa inatetea utendaji kazi wa Mheshimiwa Mwantumu Mhiza wala sina uhusiano na yeyote bali tunataka kuona haki inatamalaki.
 
Umenena vema lakini kuna mahali you are not right.Kila mtu anachukia uzembe iwe kazini au nyumbani. uzembe una madhara makubwa sana kwa ustawi wa familia au Nchi. Kuna ubaya gani kutumia kutumia leadership stile ya great leaders kama Washington au Churchill au Mandela? mimi najua kwa vyovyote vile RC aliunda kamati ya kufuatilia wafanyakazi hewa na ndio walio mpa taarifa ile. katika kamati ile kwa vyovyote vile ras alikuwemo, RSO alikuwemo pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote. kwanini asiwaadhibu wote walio mfikisha RC pale?
Sikiliza vizur alichokinena mkuu Magufuli. Alisema angemwelewa endapo angewawajibisha waliochini yake kwa kumdanganya. Sasa wewe unapewa ripot right on time unaita media kutangaza?? [emoji22] [emoji22] Nidhamu, nidhamu, nidhamu ya kazi!!!!! Japo nawahurumia wanaotumbuliwa maana hao ndo wanafanya ZEMBE type kuwajibika.
 
Back
Top Bottom