Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Lazima watu wanatofautiana hata mkiwa Chama kimoja siyo kuwalazimisha wawe kama yeye alivyo haiwezekani
 
Magufuli anachoonyesha ni kuwa wa;le walikuwa wanafikiri ukuu wa mkoa ni cheo wamekosea.Ukuu wa mkoa ni kazi,kuna kazi anazobidi mkuu wa mkoa afanye si kusubiri kupokea ripoti na kumpelekea raisi kama zilivyo bila kuhakiki.

Magufuli kaonyesha kuwa ukuu wa mkoa si kupanda gari zuri lenye bendera ya mkuu wa mkoa na kupigiwa saluti na polisi.Kuna kazi ya kufanya.

MAGUFULI KANYAGA MOTO GARI ONGEZA SPIDI WANANCHI TUNATAKA UENDESHE NCHI KWA SPIDI YA KILOMITA 1000 KWA SAA.TUMECHELEWA MIAKA 55 YA UHURU TUKO MBALI ONGEZA MOTO ONGEZA MOTO
Mbona unakata mauno hapa kama umekalia kibao kata ?
 
Just imagine viongozi walio tangulia kama siyo uvumilivu leo Magufuli angekuwa hapo alipo? kule tu kuwakejeli wakazi wa kigamboni kungetosha kumaliza ndoto zake za kisiasa. hakika anatakiwa apime mambo, na wakati mwingine atoe fursa ya mtuhumiwa kujieleza ili ajue makosa yake ndi umtumbue. haraka ya nini? Nyerere enzi zake alikuwa anakuita anakuhoji anakuonesha wapi umekosea ndio anakustaafisha kwa manufaa ya umma. Mazuri yote ya Anne Kilango ameishia kufedheheshwa hadharani daah siasa bwana!
Unawezaje kututhibitishia hilo halikufanyika?
 
Mlilia tumpate Rais Dictator , leo mnamuita majina ya ajabui ajabu eti Hitla mara Idd Amin , watanzania acheni unafik ndio kwanzaq miezi 6 subirini dawa iigie 5 years to go... mtaimba Haleluya
 
W

wanadamu wamezaliwa wanasema,

hii ni falsafa ya hali ya juu sana kwa wale wenye uwezo wa kudadavua kwa umakini blia ulimbwendende wala mapambo, mimi binafsi nadhani ni sahihi nikisema kila mtu ana ubongo wake wa kufikiri, mitazamo tuko tofauti sana tena sana, hii ni changamoto aliyoitoa Mungu ili kuleta radha fulani katika maisha yetu ya kila siku,

tukirudi kwa huyu mtoa mada, nadhan kwa kufikiria kwake anaweza kuhisi yuko sahihi sana na ndo maana katumia muda wake kuyanaadika haya lakini labda huyu mtu atakuwa yuko ughaibuni au amekosa uzalendo wa hii nchi,

wote ni mashahidi kuwa nchi hii imokosa dira sababu ya kushindwa au kucheleweshwa kufanyika kwa maamuzi, hii imeighalimu taifa kwa kiasi kikubwa (MULTPLIER EFFECT) kwa kitendo cha JPM kutengua iuteuzi huu imepeleka ujumbe mkubwa c Tanzania tu hata nje ya nchi, sasa hivi kila mtu anajua ukubwa wa kosa la kudanganya, inabidi kiongozi awe mfano na akisema jambo liwe hivyo, mkuu akisema jambo linasimama kama sheria, haya mambo ya kuchanganya sympathy na kazi ndo yanatufikisha hapa, mnakaa vijiweni na kuisifia China, je ulishawahi kukaa na kujiuliza namna ambayo china wameitumia kufika hapo walipo? ni maamuzi magumu.

Najua itawapa shida sana sababu hamkozoea, mlishakariri kila mkiharibu mnaitwa hoteli na kununuliwa juice alafu ndo mnaabiwa kistarabu mara unajua pale ulikosea, these time are not the same as those time, things are already changed, tupo na mtu anayejua kazi yake kama mkuu wa nchi, hii nchi ni kubwa na ina watu wengi, lazima mkuu wa nchi aoneshe anchukia nini.

nakushukuru kwa kuleta mada yako lakini nimesikitika sana kwa namna unavyotetea maovu.
Umenena vema lakini kuna mahali you are not right.Kila mtu anachukia uzembe iwe kazini au nyumbani. uzembe una madhara makubwa sana kwa ustawi wa familia au Nchi. Kuna ubaya gani kutumia kutumia leadership stile ya great leaders kama Washington au Churchill au Mandela? mimi najua kwa vyovyote vile RC aliunda kamati ya kufuatilia wafanyakazi hewa na ndio walio mpa taarifa ile. katika kamati ile kwa vyovyote vile ras alikuwemo, RSO alikuwemo pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote. kwanini asiwaadhibu wote walio mfikisha RC pale?
 
Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show
kuna mambo 2 ambayo naweza kuyasema,
1:kama hukupowe pesa au umaumizwa na kufukuzwa na hyo mama basa umesahau kuwa magu si digiteta bali ni Mtendaji, tafuta uzi hum ndani wakati wanawalinganisha magu na edo, watu wengi wanajua yy ni mtendaji, sasa ktk utendaji wake ndiyo stail yake, tatzo watu wamezoea ule mfumo wa lelemamaa,

2; kama huo ubabe upo kwa aina ya watendaji kama kilango na uendelee hko mliko serikalin mtajijua, sisi huku mtaani shwariiii mwendo mdundo, ninachoona ni kuwa nidham ya kazi imeanza kurudi

mwisho polen kwa yote yaliyo wakuta jifunzen kukimbia kama hamuwezi kaa pembeni wanaoweza watakimbia[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kuna siku atajikuta yuko peke yake. Dalili zinaonesha mawaziri wake wengi wameingiwa uoga fulani na ndio maana siku hizi siwasikii sana kama mwanzo. Juzi nilijiuliza hivi Makamba JR yupo? Jenista Mhagama? Zaidi ya nusu ya mawaziri wake wako kimya wanaogopa kutumbuliwa, wanasubiri watumwe tu na bosi wao.
 
Umenena vema lakini kuna mahali you are not right.Kila mtu anachukia uzembe iwe kazini au nyumbani. uzembe una madhara makubwa sana kwa ustawi wa familia au Nchi. Kuna ubaya gani kutumia kutumia leadership stile ya great leaders kama Washington au Churchill au Mandela? mimi najua kwa vyovyote vile RC aliunda kamati ya kufuatilia wafanyakazi hewa na ndio walio mpa taarifa ile. katika kamati ile kwa vyovyote vile ras alikuwemo, RSO alikuwemo pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote. kwanini asiwaadhibu wote walio mfikisha RC pale?

Kwa taratibu za nchi, mkuu wa mkoa anawajibika kwa rais, yeye alitakiwa agundue makosa alafu awawajibishe watendaji wake LAIKIN HAKUFANYA HIVYO, hakuweza kwenda extra miles, suala la ghost workers ni headache, alitakiwa kuwa makini na hii ni kwa wafanyakazi wote, tunatakiwa kuwa makini kwa kazi tunazokuwa tumepewa, kazi nyingi sana zmeharibika kwa style hii ya mama KILANGO, nadhan huu c muda wa kubembelezana, unaiongelea MAREKANI NA GEORGE WASHINGHTON, UNASHINDWA KUELEWA KWAMBA US WAMAEANZA KUPRACTISE DEMOCRACY MIAKA 250+ ILIYOPITA, MIFUMO ISHANYOOKA , UNAIONGELEA SA BILA KUJUA HALI YA S.A ILIKUWA VP NA ILIATHIRIWA VP NA APATHEID. TANZANIA TUMEAZA DEMOCRACY MIAKA YA 90 SO BADO NA HALI YA KUBEMBELEZANA C MAHALA PAKE MKUU, OUR TPP LEADERS NEED TO DISPLAY THEIR COLOURS.
 
Kuna siku atajikuta yuko peke yake.

Magufuli hayuko peke yake na haji kuwa peke yake hata siku moja.Magufuli yuko na Mungu na wananchi.Wakizira Tanzania ina watu milioni 45 atapata watu kibao wa kujaza nafasi zao.Na wasithubutu.Hao walikuwa wakijiona miungu watu maofisini mwisho wao umefika .Wachape kazi au wafungishwe virago na Magufuli.Wakizira wawe nyumbani wakiwa ofisini watatolewa mkuku.
 
Sasa miaka yote walikua wanasikilizwa je wametufanyia nini au wametuletea kituganu hasa cha maendeleo???

Zaidi ya hao viongozi kuzidi kujitunisha musuli na kujichotea mali za umma???

Ukikutana na waziri au mbunge huku ulaya mbona anaonekana kama ni mtu wa kawaida wakati hapo TZ utadhani umekutana na mtume.

Tunahitaji kiongozi mkali wa kunyosha hao watu wanao chezea maisha ya watanzania. Baada ya viongozi kunyooka ndio tujadili namna ya kuiingoza nchi kwa jinsi unavyo taka au unavyo dhania.

Tukipoteza chance hii tutakuja kujuta huko mbele. Mfano tu Marehemu Sokeine
Mm cjui wa Tanzania wanataka rais wa aina gn. Kweli tumelogwa na alietuloga keshakufa. Si ni ss tulikuwa tunamlalamikia kikwete na utawala wake dhaifu? Leo tumempata Magufuli japo sikumchagua lkn nafurahia anavyowanyoosha viongozi wazembe big up Magu.
 
Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show
Hivi kwa mfano ile Ripoti ya Shinyanga ingeaminiwa kwamba ipo sahihi na Rais asingejiuliza usahihi wa ile Ripoti je ni fedha kiasi gani ambazo tungeendelea kupoteza. Hivi ingekuwa ni wewe utamuelewaje msaidizi wako unapomtuma kazi na akutengenezee ripoti ya kimagumashi, utajiuliza sana na matokeo yake lazima ufanye kama alivyofanya JPM.
Wengi wakati ulee tulisema ooh JK mpole, ooh Rais gani hana maamuzi magumu sasa amepatikana huyu bwana tumeaanza kulalama. Tumwache atengeneze njia ili watendaji wa serikali wabadilike na wafanye kazi. Huyu amejitakia, kwa hiyo wala mheshimiwa Rais hajakosea.
 
Back
Top Bottom