Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli

Kuna siku atajikuta yuko peke yake. Dalili zinaonesha mawaziri wake wengi wameingiwa uoga fulani na ndio maana siku hizi siwasikii sana kama mwanzo. Juzi nilijiuliza hivi Makamba JR yupo? Jenista Mhagama? Zaidi ya nusu ya mawaziri wake wako kimya wanaogopa kutumbuliwa, wanasubiri watumwe tu na bosi wao.
Huko kuwa kimya ndo kutasababisha watumbuliwe, Magufuli anataka watendaji, alishasema hilo wakati anawaapisha wakuu wa mikoa, kwamba ni nafuu utende halafu akosee kuliko kukaa tu bila kutenda.

Kilango ametimuliwa kwa sababu ametoa taarifa ilitoonyesha alikuwa hayumo kwenye utendaji, angekuwa mtendaji angejua kuwa watumishi hewa wapo, au walao angekosea na kuhesabu watu walio studylive kuwa watumishi hewa, kosa ambalo ni la kiutendaji na Magufuli asingemind.
 
Kuna siku atajikuta yuko peke yake. Dalili zinaonesha mawaziri wake wengi wameingiwa uoga fulani na ndio maana siku hizi siwasikii sana kama mwanzo. Juzi nilijiuliza hivi Makamba JR yupo? Jenista Mhagama? Zaidi ya nusu ya mawaziri wake wako kimya wanaogopa kutumbuliwa, wanasubiri watumwe tu na bosi wao.
mkuu yaan hata akibaki mwenyewe hii nchi itaenda, na kabla hajakwama atawaboa wanao mkwamisha, nahisi umesahau kuwa rais anataarifa ya kila wazir na watendaji wake, hvyo uoga wao ni kwa sabab ya udhaifu wao, hii nchi kwa sasa inahitaji sana mtu kama magu, ili inyooke,

Hii ni Zawadi kutoka kwa Mungu..
 
Mm cjui wa Tanzania wanataka rais wa aina gn. Kweli tumelogwa na alietuloga keshakufa. Si ni ss tulikuwa tunamlalamikia kikwete na utawala wake dhaifu? Leo tumempata Magufuli japo sikumchagua lkn nafurahia anavyowanyoosha viongozi wazembe big up Magu.

Kwa kweli inatakiwa tuweke vyama kando kwanza. Hata mimi nilikua sipendi ccm. Hasa nikiangalia huko vijijini watu wanavyopata shida ya maji, shida na matibabu na huduma za hospitali, halafu hao wakubwa wakiishi kwenye maisha ya raha.
Leo hii inatakiwa tuungane watanzania ili tupige vita dhidi ya mafisadi. Tuonyeshe kwa dermacation kubwa tu kua watanzania wa ccm na ukawa tuko pammoja dhidi ya ufisadi na wazembe.
 
Hivi kwa mfano ile Ripoti ya Shinyanga ingeaminiwa kwamba ipo sahihi na Rais asingejiuliza usahihi wa ile Ripoti je ni fedha kiasi gani ambazo tungeendelea kupoteza. Hivi ingekuwa ni wewe utamuelewaje msaidizi wako unapomtuma kazi na akutengenezee ripoti ya kimagumashi, utajiuliza sana na matokeo yake lazima ufanye kama alivyofanya JPM.
Wengi wakati ulee tulisema ooh JK mpole, ooh Rais gani hana maamuzi magumu sasa amepatikana huyu bwana tumeaanza kulalama. Tumwache atengeneze njia ili watendaji wa serikali wabadilike na wafanye kazi. Huyu amejitakia, kwa hiyo wala mheshimiwa Rais hajakosea.
Kweli kabisa wacha Magu awatumbue tu walizowea kufanya kazi kwa mazowea wakikosa wanachekewa tu na Jk au wanahamishiwa idara nyingine. sasa wengine wajue wakikosea tu wanawajibishwa. Magu aliwaatahadharisha kbs siku ile alivyowateuwa kuwa wafurahie na kushangilia wanapochaguliwa pia wafurahie na kushangilia atakapowafukuza.
 
Kwani si ndiyo ilikuwa inasemwa kwamba Kikwete anaongoza ikulu kwa remote kutoka msoga! Au imekuwaje tena?
 
Mama amekuwa mfano wa wale wote ambao walidhania tuko katika zama za kuleana na kustiriana na kuoneana haya na Upendeleo fulani kwa Mh.JPM yeye hana hilo anaileta Nchi kwenye reli Hongera Mh. Iweke Nchi katika miiko maadili kanuni ni mwongozo inayotakiwa na Serikali yenye kuheshimu Wananchi wake pasi na Zongezonge
 
Kwani si ndiyo ilikuwa inasemwa kwamba Kikwete anaongoza ikulu kwa remote kutoka msoga! Au imekuwaje tena?
 
Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna

Mkuu kwenye ubunge ni ufundi wa maneno na huko elimu sikupata kusikia kipya alichokifanya anyway huenda alihitaji kukumbushwa au kuambiwa namna ya kuifanya hiyo kazi lakini kwenye ile speech ya kuapishwa kwao pale ikulu ningekuwa mimi ningebwaga manyanga mapema maana ilikuwa na viashiria vyote labda Mama hakusoma vipimo vya hali ya hewa vizuri, ukiona hali ya hewa haitabiriki bora kutoingia chomboni ukabaki nchi kavu salama
 
Amani iwe nanyi wanajamvi!

Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.

Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.

Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!

Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!

Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.

Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.

Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.

Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?

Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.

Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.

Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.

Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.

Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show
mnaoguswa mtalia sana. Pasco nani asiyemjua kuwa alikuwa na Edo?
 
Makonda kila siku anabuni vitu mbona haja fukuzwa
 
Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza kifamilia au kikampuni kiwe cha serikali au binafsi.
Magufuli ni mkali kupindukia kwa majipu,wezi,wavivu, watu wasiowajibika,wasio wabunifu na ambao kazi zao ni kumpelekea raisi taarifa za uongo ambazo hawajazihakiki wenyewe kabla ya kuzipeleka.

Siku njema huonekana asubuhi.Sasa mtu kama kamteua siku chache tu keshaanza kumpelekea taarifa za uongo unategemea amleee?

Ukipewa kazi yoyote kuna kipindi cha matazamio (probation period) Ukileta uzembe katika siku hizo uwe umekaa siku moja ,mbili au 20 utatolewa mkuku kama mbwa.

Mtu akiona stahili ya Magufuli hawezi keshasema ajiondoe mwenyewe kabla hajamng`oa
Mkuu hapa umemaliza kila kitu.Kutoa taarifa za uongo kwa Rais ni jambo zito hasa ukizingatia ni taarifa ambazo zingeendelea kuliletea taifa hasara.Hata kama ameongopa kwa kusababishiwa na mtu mwingine haitoshi kukwepa adhabu hiyo ndogo alopewa kwa kuwa bado alikuwa na nafasi ya kurekebisha alichoongopewa lakini hakufanya hivyo na ni sign ya kutokuwajibika hivyo hakukuwa na njia nyingine ya kumsaidia na hapa wala tusimlaumu Rais.Nimesema adhabu ndogo kwa kuwa kama Rais angeamua kujikunjua ukali wake nadhani angeweza kumuacha mikononi mwa Takukuru ili kuona kama hakuwa na lengo la kucover madudu kwa kukusudia lakini tushukuru Rais labda amezingatia background nzuri ya mamaetu huyu na ndo mana ameamua kulala nae mbele POLE POLE.
 
siku moja uwe kiongozi halafu uige staili hii uone utakavyo baki peke yako. kimsingi wote hatupendi uzembe kazi, lakini je, inawezekana mkuu wa mkoa kupita kuhakiki taarifa alizo pewa na wasaidizi wake? mimi ninge muelewa kama angewaadhibu wakurugenzi na wakuu wa idara walio mpa Mkuu wa mkoa taarifa za uongo.
Kama imekuuma sana Mchukue Anna mkanywe nae soda! Yani mtu ana ambiwa kabisa mkoa mzima hakuna mtumishi hewa ana kubali tuu kirahisi...!
 
Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza kifamilia au kikampuni kiwe cha serikali au binafsi.
Magufuli ni mkali kupindukia kwa majipu,wezi,wavivu, watu wasiowajibika,wasio wabunifu na ambao kazi zao ni kumpelekea raisi taarifa za uongo ambazo hawajazihakiki wenyewe kabla ya kuzipeleka.

Siku njema huonekana asubuhi.Sasa mtu kama kamteua siku chache tu keshaanza kumpelekea taarifa za uongo unategemea amleee?

Ukipewa kazi yoyote kuna kipindi cha matazamio (probation period) Ukileta uzembe katika siku hizo uwe umekaa siku moja ,mbili au 20 utatolewa mkuku kama mbwa.

Mtu akiona stahili ya Magufuli hawezi keshasema ajiondoe mwenyewe kabla hajamng`oa

Nakuunga mkono sana, sasa hebu tuwaulize wanaofikiria ati amewonewa, walitaka afanywe nini baada ya kudanganya katika jambo ambalo MH. Rais amelipa kipaumbele? Je, watetezi mnajua kwamba madhara ya kutochukua hatua haraka na na kwa makini yanaweza kusababisha mmomonyoko zaidi? kwani kila mmoja atafikiria kufanya kosa akitegemea ati kusamehewa; we need zero tolerance on weak and fraudulent performances.
 
Back
Top Bottom