JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Amani iwe nanyi wanajamvi!
Leo napenda nichukue fursa hii kumpongeza mwanajamvi Pasco kwa kuona mbali juu ya utawala wa mh Rais wa JMT ndugu John Pombe Magufuli.
Rais amefanya mambo mengi mazuri lakini akiteleza anaanguka kwelikweli, na mimi naanza kuona ugumu wa huko tuendako.
Kiongozi wa Nchi ukiwa mkali kupindukia athari zake ni nyingi kuliko faida!
Msaidizi wako akifanya kosa moja japo dogo adhabu yake ni kufukuzwa kazi!
Hii hali inaweza kuzalisha viongozi wanao subiri waambiwe cha kufanya ndio watende kwani watakuwa wanaogopa kubuni mambo mapya ambayo huenda bosi wao asiyapende na hivyo kusababisha wafukuzwe kazi LIVE.
Uongozi wa kiimla hushabikiwa sana na watu lakini huwa na madhara makubwa sana katika jamii.Hapa napenda niwarudishe nyuma kidogo wakati wa utawala wa Hitler.
Hitler alipendwa sana na wajerumani hasa vijana wa wakati ule.Hata alipo panga kuwafurusha waisrael warudi kwao kwani wanabana nafasi za kazi za wajerumani, alishangiliwa sana.walimuona ni kiongozi wa ndoto zao.
Hivi tujiulize kwa kadri tunavyo mjua Anne kilango Malecela, toka akiwa mbunge, naibu waziri wa Elimu na mkuu wa mkoa, ni kweli ghafla amekuwa jipu na hivyo kustahili kufutwa kazi kwa mtindo ule?
Kama amekuwa jipu basi hakuna msafi ndani ya Chama cha Mapinduzi. wahenge walisema kosa moja haliachi mke, leo hii hakuna subira ukikosa jambo dogo ujue kazi huna.
Ukimya wa Mawaziri wengi ni dalili kwamba wameanza kuchukua tahadhari sana katika utendaji wao, tofauti sana na walivyo anza majukumu yao.
Hii siyo dalili nzuri kiutendaji, ni kama wameporwa uhuru wanaogopa jambo baya kuwatokea.
Nina miezi sasa sijawasikia mawaziri wakitoa matamko kama awali ni dalili kuwa hamkani si shwari.
Tupende tusipende demokrasia haiepukiki.Viongozi walioteuliwa wana haki ya kusikilizwa.Naanza kutilia shaka hii one man show