Hakika kauli hii ilinishangaza

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Tarehe 08 Desemba 2008 siku ya Jumatatu majira ya saa 4 usiku nilifiwa na shemeji yangu mdogo wake kabisa na wife. Shemeji yangu huyo aliugua kwa zaidi ya wiki mbili na siku alofariki ndo siku aliruhusiwa toka hospitali moja kubwa ya private akiwa na nafuu kabisa. Hata nami niliporudi job majira ya saa 11 jioni nilimkuta nyumbani na tulitaniana huku akiwa na furaha kubwa ya yeye kutoka hospitali.

Mnamo majira ya saa 4 za usiku hali ilibadilika ghafla na kupelekea Shemeji yangu huyo kuanza kutapika damu mbichi kabisa mfululizo na wakati tukimkimbiza hospitali ile ile alokuwa kalazwa kwa zaidi ya wiki 2 alifariki tukiwa njiani.

Ilibidi turudi nyumbani na mwili ili tujue nini tunafanya, niliwajulisha jamaa na marafiki usiku huo huo na baadhi walifika home na walilala na sisi pale nyumbani. Mimi na wife tuliamua ni lazima kesho tusafirishe mwili kwenda kuzika nyumbani hivyo, usiku ule ule tulifanya mchakato wa kupata gari kusafirishia mwili, sanduku (jeneza) na vyote vihusianavyo na msiba.

Mwili tuliamua ulale palepale home kwavile safari tulipanga iwe kesho yake asubuhi na tulipanga twende hospitali mapema ili tumpate daktari aje na dawa autibu mwili kabla ya kuanza safari kuelekea mkoani, Kilichonikuta hapa ndo chanzo cha habari yangu hii ya kweli kabisa ilonitokea nikiwa moja ya mikoa ya Magharibi mwa nchi yetu.

Mapema asubuhi nilienda kwanza job nikachukua Compasionate leave siku 14 ndipo nikaamua kwenda hospitali kumpata daktari wa kuja kuutibu mwili kabla ya kuanza safari ya mkoani. Wanasema, ukistaajabu ya Ndugai utayaona ya Tulia na kweli niliyaona. Tukiwa mimi na Mchungaji wangu tulipofika hospital ndo tukakutana na maajabu ya Rajabu kumuoa Mwajabu binti wa Mzee Rajabu.

Kwanza, tuliambiwa dawa hakuna baada ya vuta nikuvute ndpo jamaa akatuambiwa dawa zimeisha na kuwa kwasasa hospitali hiyo ya wilaya (jina kapuni) imebaki na dozi ya kutibu miili 2 tu na hivyo hawaruhusiwi kutibu mwili wowote ule nje ya miili hiyo miwili wanayopaswa kuitibu. Mchungaji akamuuliza miili hiyo ni ipi?

Jamaa, akajibu siruhusiwi kuitaja miili hiyo ila kifupi dawa hamna... Mimi Nikaingiza mkono mfukoni nikatoa elfu 30 nikamshikisha jamaa. Shaaabashiiii, jamaa akasems kwa sauti ya juu, nanukuu.." akifa Mbunge au Mkuu wa wilaya shauri yao mimi siwezi kufa njaa kwaajili ya kusubiri miili yao" Tulipigwa na bumbuwazi mimi pamoja na Mchungaji wangu ila tulishukuru kwani elfu 30 ilitufanya tujue mengi. Yaani Mtumishi wa Serikali anaamua kubuni uongo ili tu kuhalalisha mazingira ya yeye kupata fedha.

Mwili ulitibiwa na tukasafirisha kwenda kuzika Kanda ya Kati salama salimini. Leo nimekumbuka tukio hili lilotokea miaka 15 ilopita tena nilkiwa mkoani. Nawatakia Jumatano Njema na Mungu awabariki sana.

Vipi wewe uliwahi kutwa na tukio gani lilohusisha rushwa/ hongo ndipo ukapewa huduma?
 
Anayetakiwa kuthibitisha kifo cha mtu ni daktari, waswahili huwa mnazika hai waliozimia kwa ujuwaji.

Mtu anapofariki kuna process ya tangazo la kifo na kibali cha mazishi ili baadaye uprocess death certificate, halafu utashangaa na wewe naye unajiita msomi huku unafanya mambo kienyeji.
 
Aiseh! NDIO maana jemedari makonda ameanza kazi rasmi!atumbue majipu kama hayo!!
FB_IMG_1699989623291.jpg
 
Pole kumpoteza mpendwa wako.

Huduma nyingi Nchi hii inatolewa kwa kutoa rushwa. Hasa hospitali za Serikali, Trafiki, Mahakamani n.k

Kuna siku nilitaka niwafukuzishe kazi maaskari fulani wa barabarani kwa kuendekeza rushwa, bahati roho ya huruma iliniingia. Maana nilikuwa na hela za Moto siku ile zaidi ya laki 1.5.

Nimepanga wakiendelea, nitawashikisha hela za moto hasa Maaskari kipande cha Mikumi hadi Makambako.
 
Babu hela za moto ?
Umenistua huo msemo wanautumia hapa nilipo kumaanisha hela za masharti .

Askari ukitaka wakuheshimu siku jitoe ufahamu wajaze kwenye kumi na nane zako utakuja kujua askari wanaombaga msamaha na ni wapole sana
 
Nlikuwa nimemaliza form 6 .....huko kanda ya ziwa....tunafatilia birth certificate kwa ajili ya kuapply mkopo.... aseee wale wamama kwa mkuu wa wilaya hawana muda na mtu watu nyomi balaaa...nilifatilia for consecutive 3dys bila bila... mwsho nikakasirika nikatoa shiit nyingi pale pale kwa DC...nikashangaa mama mmoja anasema huyo anayetoa kashfa aje kwa kujiamini nikaenda nikashangaa...ananiambia una sh ngapi ..
Huwezi amini nilitoa 20k wakaprint cheti muda huo huo...nikasepa zangu capri point kulaa PRIMUS..
 
Babu hela za moto ?
Umenistua huo msemo wanautumia hapa nilipo kumaanisha hela za masharti .

Askari ukitaka wakuheshimu siku jitoe ufahamu wajaze kwenye kumi na nane zako utakuja kujua askari wanaombaga msamaha na ni wapole sana
Haha ....sio hela za manyoka Mkuu

Nina access ya kupata hela za moto za Takukuru, kwahiyo ilikuwa rahisi kuwapa na kuwafukuzisha kazi.
 
Kuna siku waniliotea Road mara 4, alafu kote wanataka hela utasema waliziweka
Anhaa wanasumbuaga sana wanabuni hata kosa la uongo .

Dawa yao ni kuwafukuzisha kazi tu hamna namna na ukizingatia ajira zao zimeandikwa kwa penseli basi hadi raha

Hiyo access sinayo japo nina uwezo wa kuwazingua ila kwangu mimi wangeondoka wengi kazini maana ni wasumbufu sana .
 
Ukifanya hivyo, wengi watabaki bila ajira

Ni kuwaonea huruma tu
 
Anayetakiwa kuthibitisha kifo cha mtu ni daktari, waswahili huwa mnazika hai waliozimia kwa ujuwaji.

Mtu anapofariki kuna process ya tangazo la kifo na kibali cha mazishi ili baadaye uprocess death certificate, halafu utashangaa na wewe naye unajiita msomi huku unafanya mambo kienyeji.
Wewe ndugu yangu Ramani na vichochoro vya Tanganyika usilinganishe na Mwananyamara.
Mtu kazima saa 4 usiku, wakasafirisha asubuhi bila kusikia wala kuona akitikisa kidole, tuseme walizika siku ya tatu baada ya kuwa amezima, jumla damu aliyopoteza bado alikuwa hai?

Yawezekana hayo madai yako yakawa kweli kwa baadhi ya matukio na hasa kwa Waarabu na wanaofanana nao mtu akizima ndani ya masaa 6 yuko chini ya futi 6 lkn kwa tulio wengi ambapo maiti kama haivuji lazima ikae siku 2 au 3 tukisubiriana,wangekuwa wamesha fufuka wengi sana.
 
Wewe na mkeo mna mioyo migumuuu .... njiani mkaamua kurejesha mwili nyumbani na kulala nao ... kisha kufanya maamuzi ya kusafiri kesho yake (hongereni manake mliweza kuwa na fedha za akiba na watu wa karibu walowasaidia).
Poleni
Chai ya pili pili nayo ni tamuu
Kwa hiyo kama wana usafiri wao ulitaka mpaka wakubembeleze na kukulazimisha uwachangie nauli? Acha kukariri dada.
 
Anayetakiwa kuthibitisha kifo cha mtu ni daktari, waswahili huwa mnazika hai waliozimia kwa ujuwaji.

Mtu anapofariki kuna process ya tangazo la kifo na kibali cha mazishi ili baadaye uprocess death certificate, halafu utashangaa na wewe naye unajiita msomi huku unafanya mambo kienyeji.
Hii ni chai. Mtu hawezi kumrudisha akiwa njiani mgonjwa anayempeleka hospital eti amefariki. Big no. Kwanza kile kiwewe unachokuwa nacho hutaamini kama amefariki na utataka tu kumfikisha hospital.
 
Wewe ndugu yangu Ramani na vichochoro vya Tanganyika usilinganishe na Mwananyamara.
Mtu kazima saa 4 usiku,wakasafirisha asubuhi bila kusikia wala kuona akitikisa kidole,tuseme walizika siku ya tatu baada ya kuwa amezima,jumla damu aliyopoteza bado alikuwa hai?

Yawezekana hayo madai yako yakawa kweli kwa baadhi ya matukio na hasa kwa Waarabu na wanaofanana nao mtu akizima ndani ya masaa 6 yuko chini ya futi 6 lkn kwa tulio wengi ambapo maiti km haivuji lazima ikae siku 2 au 3 tukisubiriana,wangekuwa wamesha fufuka wengi sana.
Unabisha kitu ambacho hujui. Ni hivi: unaweza kudhani mgonjwa amefariki kumbe amezimia. Sasa kitendo cha ku-assume amefariki na kusitisha huduma kinafanya afariki kweli. Ina maana kwamba kama ukimpa huduma mapema atazinduka.
 
Nilipomaliza kidato cha sita, nilienda kwa binamu yangu mkoa wa Mara . Nikapata maambukizi ya staphylococcus. Nilijua ni bacterial infection kwakuwa baada ya kutibu mara kadhaa bila mafanikio, ilibidi kufanya kipimo cha culture.

Aisee ugonjwa ulinitesa , maana Kila nikimaliza dozi siponi. Yaani mayibabu yenyewe yalikuwa ya kusuasua kwakuwa nilikuwa nategemea fedha ya matibabu kutoka kwa binamu.

Baada ya kusubiri kwa muda huku nikiendelea kuugua, hatimaye Bina akanipa tsh2000/- nikatibwe. Kwa miaka Ile ilikuwa hela nyingi. Nimefika hospitali ya mkoa, nikajiandikisha , hatimaye nikaingia kwa daktari. Nikamweleza jinsi nimekuwa na maumivu kwenye njia ya mkojo kwa muda mrefu, na dawa nilizokwishakutumia. Ajabu, akaniambia ili aniandikie dawa, nitampa 2000/-.Nikawa nimemwelewa kuwa anataka rushwa. Nikakubali lakini nikapania moyoni kuwa nitamkomesha. Akaniandikia Vipimo, nikaenda maabara, baada ya mchakato kuisha nikarudi chumbani kwa daktari.

Akaniandikia dawa pale na kunielekeza kuwa niende nikazinunue. Nikambadilikia , nikamwambia wee jamaa nimeshakulipa Kila kitu hapa siondoki bila dawa. Akashangaa maana niliongea kwa sauti ili hata walio nje wasikie . Akaona hili ni Soo . Akachomoa Ile buku mbili akanipa, nikachukua cheti nikatoka nje. Nikapitia dirisha la dawa nikanunua nirudi home. Bahati nzuri nilipona.
 
Back
Top Bottom