Haki za kupanga na kupangisha kwa mtanzania zinasemaje?

tkaungya

New Member
Jul 2, 2010
1
0
Huyu mtu aliye jenga nyumba anakuwa ametumia fedha nyingi sana kujenga nyumba.

endapo anataka kuitumia kibiashara ni haki gani za msingi anazotakiwa kupewa mpangaji na ni haki gani za msingi anazotakiwa kupewa mwenye nyumba?

Ni nyumba ya namna gani ambayo serikali inairuhusu kuwa ya kupangisha?

Na malipo yakoje?
 
Kaka swali lako refu itabidi uende kwenye sheria zinazohusu mambo ya upangishaji. Lakini kwa kifupi ninazozikumbuka ni zifuatazo:-
Haki za mwenye nyumba:
Kulipwa kodi yake kutokana na mkataba unavyosema baina yenu, kuingia na kukagua nyumba kwa ruhsa ya mpangaji,
Wajibu wa mwenye nyumba: Ni kuhakikisha nyumba anayopangisha ni nyumba ambayo inafaa kukalika, mfano ina choo iko katika hali nzuri sio imebomoka kiasi haifai kukaliwa na binadamu, wajibu wa kufanya matengenezo makubwa katika nyumba kama ktk mkataba hamkukubaliana kuwa itakuwa matengenezo ya mpangaji, wajibu wa kulipia kodi za serikali za nyumba hiyo kama haiko katika makubaliano na mpangaji, Biashara utakayofanya iwe ambayo mmekubaliana na mwenye nyumba wakati unapanga ukibadilisha kama hatoridhika nayo ana haki ya kusitisha mkataba wako mf. Umepanga ili uendesha duka la vifaa vya shule, mara umebadilisha unaweka baa ya kunywa pombe za kienyeji na unasababisha wapangaji wengine wenye biashara zao kutoridhika na biashara hiyo mpya.

Haki za mpangaji:
Kuishi katika nyumba aliyopanga bila kubugudhiwa na mwenye nyumba,

Wajibu wa mpangaji:
Kulipa kodi kama walivyokubaliana na mwenye nyumba, kuishi katika nyumba anayokaa bila kuichafua kiasi cha kufanya hiyo nyumba isikalike na mtu mwingine, kutopangisha mpangaji mwingine bila makubaliano maalum na mwenye nyumba akiondoka, kulipia matumizi mbali mbali ya umeme na maji, simu kama vitu hivyo vipo na havikuainishwa kwenye mkataba kuwa viko katika kodi, wajibu wa kutobadilisha sura ya jengo alilopanga bila idhini ya mwenye nyumba na akiondoka hatakiwi kubomoa kiasi cha kuharibu jengo aliloliacha, wajibu wa kuhakikisha unachokifanya hakiwaudhi wapangaji wengine, wajibu wa kulipia kodi za serikali za biashara unayoifanyia hapo mahali.

Serikali inaruhusu nyumba yeyote bora iwe na huduma muhimu za binadamu kama maji, choo, na mazingira masafi ya kufanyia biashara. Lakini pia eneo hilo liwe limeruhusiwa kwa biashara hiyo unayoifanya. Mf. huwezi kuweka baa eneo la shule ni makosa. Au ukaweka kituo cha kuuzia mafuta wakati watu wanaishi kwenye nyumba hiyo hiyo au kiwanda ukajenga sehemu ambayo imetengwa kwa ajili ya mambo mengine.

Malipo ni makubaliano ya mwenye nyumba na mpangaji. Lakini vigezo vifuatavyo ndio vya kuzingatia. Jinsi ya kulipa kodi - kwa siku, wiki, mwezi au mwaka n.k., au malipo kwa ukubwa wa eneo, mita za mraba, kwa chumba nk.

Kila la kheri
 
Sheria haiangalii nyumba imegharimu kiasi gani .Inaangalia makubaliano kati ya mpangaji na mwenye nyumba Mazee. Hayo makubaliano au mkataba unapaswa kufuata sheria ya Ardhi.Land Act 1999 Sect. 77(i)

Haki za mpangaji na mwenye nyumba zimeanishwa. Itafute uisome kwa sababu inamhusu kila mmoja wetu. Kama wewe si mwenye nyumba basi ni mpangaji.
 
Pia sheria zinaangalia thaamani ya eneo nyumba ilipo iendane na uhalisia wa kodi anayolipa au kuuziwa mtu
 
Sheria pekee nayoijua mie ni "Nikitaka kutimuliwa (Notice) itambidi mzee anipe miezi 2 kabla" lasivyo awe mpole tu!.
 
Back
Top Bottom