Haki sawa

Haki sawa

Huo ufala sasa..... demokrasia ikizidi ni ujinga km sio utumwa. Hakuna jipya kk , yote ni mapokeo. Nyajibu za kila siku kifamilia ziko wazi sana

Ufala uko wapi hapo? Unasikiliza story za kijiweni washkaji wanavyoishi na wake zao?
 
Acha kumtesa mwenzio kwani kuwa wawili tu ndo iwe sababu ya yy kutokuwa na msaidiz au ni mama tu wa nyumban? Me nipo na mume wangu tu hatuna mtoto na wala mimba sina ila mfanyakz nnae tena tulipotoka tu honeymoon akaletwa

Kumtesa???? anamtesa wakati wapo wawili tu ndani ya nyumba, kweli??? kufua, deki, chakula cha wawili kinamshinda??? ridiculous kabisa... anyways, makuzi/malezi yanatofautiana, nisiwe hakimu...
 
Wanawake wa siku izi ni htr tupu. Jana nimenuniwa mwenzenu. Kisa eti alikuwa busy na sikumsaidia.
Cha kushangaza ni kuwa kulikuwa na shughuli mbili;
1. Kuosha sufuria 3, sahani 2, bakuli 1, mwiko, upawa na vijiko.
2. Kwenda kununua nyama buchani umbali wa m.150 toka nyumbani kwetu.
Nikamwambia zote zake. Kanuna mpaka Leo.
Hahahahaaaaa.....
Wajibu wa Mke ni nini? Dada zangu haki sawa zinawapeleka kombo. Kuweni makini.

Zamu yako kupika.
Kwani muliandikishiana mkataba yeye aje kufanya kazi hizo kwako?
Kwani yeye mtumwa wako?
 
Acha kumtesa mwenzio kwani kuwa wawili tu ndo iwe sababu ya yy kutokuwa na msaidiz au ni mama tu wa nyumban? Me nipo na mume wangu tu hatuna mtoto na wala mimba sina ila mfanyakz nnae tena tulipotoka tu honeymoon akaletwa

nadhan mume wako anamatatizo siyo ajabu wewe ukafikir sawa kuna haja gan ya kuoa kama shughuli zote azifanye house girl
 
Kuandaa chakula ni ihsani yake tu lakini sio akiacha umuone kakosea. Mke akikataa kunyonyesha mtoto wako basi hana kosa, ni mtoto wako atakama amemzaa yeye

Aisee unakosea sana kwani hujui kwamba hata mwanamke ana ovum(yai) ambalo likiungana na sperm ndio mtoto anakamilika...
Akiacha kumnyonyesha atakiona cha mtemakuni
 
Aibu aibu..... nilimsema mpaka akanikoma Jana. Akapanga vitu vyake eti anarudi kwao. Nikamwambia akasimulie yaliyotokea bila kupotosha lolote, akaogopa na kurudi ndani....
Namuandalia somo lake LA wajibu wake wa ndani!!!

Hahahhh yanii hapo ni utam kolea..
 
Wanawake wa siku izi ni htr tupu. Jana nimenuniwa mwenzenu. Kisa eti alikuwa busy na sikumsaidia.
Cha kushangaza ni kuwa kulikuwa na shughuli mbili;
1. Kuosha sufuria 3, sahani 2, bakuli 1, mwiko, upawa na vijiko.
2. Kwenda kununua nyama buchani umbali wa m.150 toka nyumbani kwetu.
Nikamwambia zote zake. Kanuna mpaka Leo.
Hahahahaaaaa.....
Wajibu wa Mke ni nini? Dada zangu haki sawa zinawapeleka kombo. Kuweni makini.

makosa ni yako ww inaonesha ulimzoesha hvyo ndio maana leo ameona tofauti..... Wengi huwa tunakosea kutoa mwongozo na msimamo mwanzon kabisa mwa ndoa
 
Mwanamke ni kama mtoto unavyomlea ndivyo anavyokua na lugha uliyoitumia inaweza ikawa chanZo cha kununiwa kaka
 
Kumtesa???? anamtesa wakati wapo wawili tu ndani ya nyumba, kweli??? kufua, deki, chakula cha wawili kinamshinda??? ridiculous kabisa... anyways, makuzi/malezi yanatofautiana, nisiwe hakimu...

Kama hzo kazi mnaziona rahisi sana mbona huwa nyinyi wanaume hamzifanyi?
 
Kama hzo kazi mnaziona rahisi sana mbona huwa nyinyi wanaume hamzifanyi?

hapo ndip mnakoseaga kwan majukum yako ww ni yapi?? Inamaana hakufundishwa kaz kama hzo kwa wazaz wake?? Usasa na haki sawa ndio yanayowaletea matatzo katka ndoa...... Mbona mama zetu na bibi zetu hawakuwa na haya mnayoyataka nyinyi?
 
Kama hzo kazi mnaziona rahisi sana mbona huwa nyinyi wanaume hamzifanyi?

Ndio maana nikasema malezi/makuzi yanatofautuana. Kwa nini nisiweze?? Baada ya ndoa ni wakati muafaka kuwa wawili ndani ya nyumba, kusaidiana shughuli ndogondogo za ndani. Sidhani kama kuna haja ya kuwa na msaidizi wakati mpo wawili tu, hata mimba bado hamna..
 
hapo ndip mnakoseaga kwan majukum yako ww ni yapi?? Inamaana hakufundishwa kaz kama hzo kwa wazaz wake?? Usasa na haki sawa ndio yanayowaletea matatzo katka ndoa...... Mbona mama zetu na bibi zetu hawakuwa na haya mnayoyataka nyinyi?

Dunia imebadilika kila upande tatizo mnaangalia upande wa wanawake tu, hao bibi zetu kwani walienda shule au walikuwa wanaenda maofisin? Walilelewa mazingira ya kwamba ukikuwa kazi ni moja tu kuolewa, kuzaa na kumtumikia mumeo, ila mabadiliki ya maisha yamefanya sasahv hatulelewi hvyo tena kwani priority ya kwanza ya mtoto wa kike au kiume ni elimu kwanza, then kazi au biashara hayo yaliyobakia ya kaz za ndani ni ziada. Mm nilivyolelewa kwetu tupo watoto 4 wasichana wawili na wanaume wawili kabla ya wazazi kuleta msichana wa kazi wote tulikuwa na zamu ya kufanya kaz za ndani kuanzia usafi wa ndani hadi kupika na kuosha vyombo na tulizifanya kwa usawa hakukuwa na kazi hii ya wasichana hii ya wavulana, si usawa nilianza kuuona toka kwetu nikiwa mdogi
 
Back
Top Bottom