Haki na demokrasia haikai chumba kimoja njaa, umaskini, maradhi na ukosefu mkubwa wa huduma. Idadi ya waChina ni robo ya dunia, kama kila mchina angepewa haki na demokrasia ya kusema na kutenda wachina wangekuwa ombaomba duniani, wangekufa njaa, wangeshindwa kujivisha, wangeshindwa kujilaza.
Hata wazazi wetu kama wangetupa demokrasia na haki zetu za kulala na kuamka asubuhi huenda tusingekwenda shule.
Hata ulaya usipolipa kodi adhabu yake ni kubwa sana.
Lazima tuburuzane wenyewe kwa wenyewe ili tuzalishe kwa wingi ndipo tuje tukae kitako tugawane ziada (surplus) kwa haki (equitably). Masikini hana haki wala demokrasia atakunywa maji pamoja na mifugo kwenye dimbwi moja kama hakuna maji safi kwaajili ya binadamu, sisi ni masiki bila hata ya kupepesa macho, hatuwezi kuwaza kugawana ambacho hatuna badala ya kuwaza kwenye kuzalisha kwanza. Hata wazungu hawakuanza na demoakrasia, na mataifa walioanza na haki na demokrasia yalifeli, kama vile USSR, North Korea, Venezuella, Tanzania, Cuba.
Wazungu walituletea demokrasia na haki mapema kwakuwa wanajuwa kuwa vitatudumaza kiuchumi. Tutatumia muda mwingi kubishana, barabarani kuomba kuomba kura, kuomba wanachama ma kiandamana kudai haki na demokrasia, tutapigana risasi wenyewe kwa wenyewe na kuuana na kusahau muda wa kuzalisha.
Mbaya zaidi hata hao watetezi wa haki na demokrasia wanafanya hivyo kama ajira yao na sio hasa kutoka mioyoni mwao. Primary goal yao ni kipato sio kile kile kilichoandikwa kwenye makablasha yao.
Lazima watu wote bila kujali jinsia, dini, vyama vya siasa, kabila au rangi tukae kitako tutengeneze agenda yetu ya miaka 100 ijayo inayoonyesha tunakotaka kuwa na namna ya kuwa tunachotaka. Falsafa yetu ni nini?
Rais Samia sina mashaka anaifahamu falsafa hii, wanzungu watatupenda sana kama tukihubiri haki na demokrasia kwenye mataifa yetu kwakuwa wanafahamu madhara yake kiuchumi. Wao bado wanapora hadi leo kutoka mataifa mengine resources za kwenda kutekelezea haki na demokrasia kwenye mataifa yao, sisi tutakwenda kupora wapi?
Kwakuwa kanuni ya maendeleo ni kupora haki demokrasia resources (personnel, money, materials and Time) za wengine bila kuwalipa kabisa au kuwapa kidogo sana ndio maana labda JPM hakuongeza mishahara watumishi, alipora wafanyabiashara, hakuajiri sana, alipunhuza wenye vyeti feki bila kuwalipa, hakuna dawa kwenye zahanati, hakuna pesa kwenye mawizara na ofisi, hakuna kusafiri nje, hats yeye alitumia magari kusafiri, nk ili spate fedha za maendeleo na ndiyo maana Leo tunaona hayo tunayoyaona kwenye awamu ya tano.
Kama unataka maendeleo lazima upore haki, demokrasia na resources za watu wako au za watu wengine, nothing less nothing more. Hiyo ndiyo maana sasa hivi Wachina wanapora, wamarekani wanapora , Rwanda inapora kutoka DRC, na ulaya wanapora hiki na kile kutoka kwa wengine kwa njia mabalimbali zikiwemo, mikataba, kibiashara, kivita, na mikopo.
Kwakuwa sisi hakuna kwa kupora nje ya nchi kilichobaki ni kupora kifogo haki, demokrasia na nguvu za watu wetu wenyewe kwenye kuzalisha. Mfano, wafungwa wapewe zana za kisasa za kilimo, kuchimba na kuvua wakalime sana, wakachimbe sana na kuvua sana kwa ujira mdogo kabisa wa chakula na mavazi na matibabu tu, wanajeshi wazalishe mahitaji yao na ziada badala ya kusubiri vita ambayo haipo, watu wooote walipe kodi wakiwemo wabunge na kila mtu nchini, hakuna msamaha wa kodi kwa mtu wala taasisi yoyote ile, demokrasia ipewe nafasi kidogo sana ili watu watumie muda wao kufanyakazi, wakulima lazima walime kwa lazima mazao yanayotakiwa, sio hiari. Kama tukisema mkoa huu umlime alizeti kuondoa uhaba ya mafuta ya kula lazima watu walime sio kwa hiari. Mfugaji lazima afuge kwa tija kwa lazima sio hiari yake, alazimishwe afuge mbegu fulani inayotoa nyama ya uzito fulani na ngozi yenye ubora fulani, na maziwa kiasi fulani.