Huyo Magufuli hakuwa na sifa hizo. Angekuwa ni mpenda maendeleo ya kweli, asinge ubariki ule uhuni wa baadhi ya wabunge na madiwani wa upinzani wa kuchezea hela za walipa kodi, kwa kuunfa mkono juhudi zake feki!
Angekuwa ni mpenda maendeleo ya kweli, angepunguza pia matumizi kwenye serikali yake na yale ya wabunge! Badala ya kuwaonea watumishi wa umma pekee! Alimsifia hadharani DED aliyenunua gari la kutembelea kwa milioni 400! Yeye mwenyewe alijiimarishia ulinzi na msululu wa magari ya kifahari kwenye misafara yake!
Wakati mwingine jaribu kutofautisha kati UZALENDO kwa nchi na UBINAFSI wa mtu. Rangi nyeusi kamwe haiwezi kulinganishwa na rangi nyeupe!
Huo ni mtizamo tu, kwani wakati chato, shinyanga na mikoa mingine ikiwa kwenye giza totoro kwenye awamu ya kwanza, pili, tatu na ya nne ilikuwepo mikoa ambayo umeme ulikuwa umawaka hata kwenye mashamba ya migomba na kahawa vijijini, ilikuwepo mikoa ambayo barabara zake za kuunganisha kata na kata zilijengwa kwa kiwango cha lami. Ilikuwepo mikoa ambayo ilikuwa na usafiri mzuri wa barabara, reli, ndege na majini wakati mikoa mingine ilikuwa na baranara za vumbi tu. Alichofanya JPM ni kuwakumbuka wale waliokuwa wamesahauliwa kabisa kwenye awamu zikizopita, bahati ambaya na kwao chato kulisahauliwa pia.Magufuli angekuwa na sifa ya kupenda maendeleo a singetumia mabilioni ya walipa kodi kujenga kijiji chake alichozaliwa na kuwaacha mamilioni ya waTanzania katika hali mbaya kiuchumi,kijamii,afya na elimu.