Haki haidaiwi kwa maandamano-PENGO

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Kardinali Pengo ameiasa jamii kuacha kudai haki kwa Njia ya MAANDAMANO,amesema kuwa baadh ya wanasiasa huwahadaa vijana kwa kuwahamasisha vijana kuandamana jambo linalohatarisha usalama:
My Take:MAANDAMANO MBONA YANAOGOPWA?
Sosi:TANZANIA DAIMA JUMAPILI
 
Pamoja na kuwa si busara kukimbilia maandamano kila wakati. Lakini ukweli utabaki kuwa Maandamano ni njia ya kuwasilisha ujumbe, hata kanisa hufanya maandamano, taasisi mbali mbali hufanya maandamano, katiba inaruhusu maandamano. Labda alimaanisha kuwa maandamano si njia pekee ya kudai haki, au si hatua ya kukimbilia katika kudai haki, inawezekana anahimiza umuhimu wa majadiliano ya pande mbili. kwani faida ya majadiliano ni kuwa huacha watu wa pande mbili wakiwa wameshikana mikono kwa furaha, wakati maandamano ya kudai haki huacha jamii ikiwa katika mapande mawili makubwa, na ambayo yamesimama juu ya misingi imara ya chuki, visasi, na ujeuri. Muanzisha Thread umeiweka kwa kifupi sana hiyo taarifa, sijui lengo lako ni nini? Siamini kama Tanzania Daima wameandika taarifa nyeti kama hiyo kwa ufupi huo. Nakushauri usiwe mwoga wa kusikiliza mawazo yanayokinzana na ya kwako ,Wape wasomaji uhuru wa kusoma habari kamili na kuelewa kwa uwezo wao kiakili badala ya kuwalazimisha waelewe ulivyoelewa.
 
Consiglier nakuunga mkono, sidhani kama Pengo ametamka moja kwa moja kwamba maandamano si njia muhafaka kutumika katika kudai haki, Bajabiri ata siku nyingine inabidi awe makini ktk kudadafua mambo; Pengo ni mtu mwenye uelewa wa hali ya juu hawezi kupinga kihivyo wakati dhana ya maandamano iko wazi: labda kama alikuwa anataadharisha waandamanaji kuwa makini kuepuka ghasia zinazoweza kuatarisha maisha yao ktk mchakato huo, ''Nia na madhumuni ya maandamano siku zote ni kuleta mabadiliko'' sasa ambaye ataki mabadiliko ndiye anaye atarisha maisha ya waandamanaji.
 
Afadhali mwenzenu kawaonya kuhusu maandamano. Huyu nasikia ni kama mungu hapa duniani. Sasa acheni kumsikiliza muone.
 
Afadhali mwenzenu kawaonya kuhusu maandamano. Huyu nasikia ni kama mungu hapa duniani. Sasa acheni kumsikiliza muone.

Siku hizi mmeacha kuandama kuunga mkono kila asemalo mwenyekiti? Unakumbuka Darwin's Nightmare?
 
Cons n PrN,
tanzania Daima lipo mtandaoni mwaweza ileta link,ila cna maana yoyote wadau,
Mkumbuke,hawa viongoz wetu wa kidin nao ni vigeugeu az politicianz,cwaamini sana
WALITUAMINISHA KUWA MR MSOGA NI CHAGUO LA MUNGU,
CKU IZ WANAUZA UNGA,hawaeleweki sana!
 
exactly; hawa jamaa huwa nawasikilizia kwa ''machale sana'' siwapi 100% ktk siasa.
 
Kardinali Pengo ameiasa jamii kuacha kudai haki kwa Njia ya MAANDAMANO,amesema kuwa baadh ya wanasiasa huwahadaa vijana kwa kuwahamasisha vijana kuandamana jambo linalohatarisha usalama:
My Take:MAANDAMANO MBONA YANAOGOPWA?
Sosi:TANZANIA DAIMA JUMAPILI

Mie mkatoliki (samahani-nasema ili niwe na amani) na namheshimu sana Kardinali wetu!

Kwenye hili nasema kakosea! Angeshauri aina hani ya maandamano yanafaa naamini mimi nisingrkuwa na taabu na kauli yake! Maandamano ni njia ya kujieleza kama jamii au kundi itumikayo hata kabla ya kuzaliwa Jesus.

Inaogopesha taasisi za dini zinapooanza kujiingiza katika siasa (heri wangekuwa wanashauri yenye akili na matarajio mema) na kuongea matamshi yanayoongeza nyongo katika matumbo yetu wananchi!
 
Consiglier nakuunga mkono, sidhani kama Pengo ametamka moja kwa moja kwamba maandamano si njia muhafaka kutumika katika kudai haki, Bajabiri ata siku nyingine inabidi awe makini ktk kudadafua mambo; Pengo ni mtu mwenye uelewa wa hali ya juu hawezi kupinga kihivyo wakati dhana ya maandamano iko wazi: labda kama alikuwa anataadharisha waandamanaji kuwa makini kuepuka ghasia zinazoweza kuatarisha maisha yao ktk mchakato huo, ''Nia na madhumuni ya maandamano siku zote ni kuleta mabadiliko'' sasa ambaye ataki mabadiliko ndiye anaye atarisha maisha ya waandamanaji.

acha ushabiki ndugu yangu. Huyo Pengo unayemsema kuna wakati msaidizi wake Kilaini alitamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, kwanini asitumie uelewa wake kupinga hilo? Dini isikufunge ndugu, hao mapadre wenyewe ndio walevi, wazinifu, wahubiri sadaka n.k.
 
Afadhali mwenzenu kawaonya kuhusu maandamano. Huyu nasikia ni kama mungu hapa duniani. Sasa acheni kumsikiliza muone.

Mungu yupi asiyejua kinachotokea duniani? Madagascar Ravalomanana kakimbia nchi sababu ya maandamano, Misri, Tunisia n.k.
Anatakiwa kujiuliza kwanini watu wanaamua kuandamana na ku riskmaisha yao, sio kulaumu wanaoandamana.
 
Afadhali mwenzenu kawaonya kuhusu maandamano. Huyu nasikia ni kama mungu hapa duniani. Sasa acheni kumsikiliza muone.

Mungu wako labda Rejao. Kwetu sisi ni kiongozi wa kiroho ambaye hafanani na wale viongozi wa Al Shaabab wala marehemu Osama Bin Laden.
 
Kardinali Pengo ameiasa jamii kuacha kudai haki kwa Njia ya MAANDAMANO,amesema kuwa baadh ya wanasiasa huwahadaa vijana kwa kuwahamasisha vijana kuandamana jambo linalohatarisha usalama:
My Take:MAANDAMANO MBONA YANAOGOPWA?
Sosi:TANZANIA DAIMA JUMAPILI

Huyu naye kakurupuka tu, hajui yaliyompata Mubarak baada ya watu kuamua kukutana pale Tahrir Square!?
 
Jaman mi nasema hawa religious leaderz bhana,c wa kuwaamini,wengne ni UWT
Huyu naye kakurupuka tu, hajui yaliyompata Mubarak baada ya watu kuamua kukutana pale Tahrir Square!?
 
acha ushabiki ndugu yangu. Huyo Pengo unayemsema kuna wakati msaidizi wake Kilaini alitamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, kwanini asitumie uelewa wake kupinga hilo? Dini isikufunge ndugu, hao mapadre wenyewe ndio walevi, wazinifu, wahubiri sadaka n.k.
Tofautisha tabia na uwezo wa mtu wa uelewa. Uelewa wa Pengo ni zaidi ya ufikiriavyo... achana na Pengo (viongozi wa kanisa katoliki) kama unabisha waulize freemasons na Illuminati.
ukadinari hakupigiwa kura kama wafanyiavyo wanasiasa. Sila kila asemalo pengo basi likubalike na kila mtu, hata Yesu na Manabii wengine Akiwepo Muhamad (mtume) walikubaliwa kila kitu na jamiii waliokuwa wahaihubiria juu ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu. kuna msemo usemao kila mtu ni mfalme kwenye ubongo wake. Pole weee
 
Back
Top Bottom