Best home tutor
Senior Member
- May 8, 2026
- 194
- 265
✍️Anaandika Askofu Bagonza
"Mmoja amesema, “Hakuna haja ya kuandamana, CCM itawapa katiba mpya”. Huo ni uongozi. Hiyo ni diplomasia. Hiyo ni hekima. Hata kama huwezi, unajenga matumaini ya wanaokudai kuliko kutunishiniana misuli na raia wako.
Basi na atokee mwingine aseme;
1. Tundu Lisu ataachiwa. Sitisheni maandamano yenu. Ipeni nafasi serikali ilifanyie kazi hili kwa umakini. Tamko hili halipunguzi chochote ila linaongeza kitu.
2. Tume huru ni sehemu ya katiba mpya. Msiandamane kupata kipande. Subiri mpate kitu kizima.
3. Utekaji umetufarakanisha. Kila chama na kila dini wameathirika. Maandamano yenu yanatupa nguvu ya kukabiliana na watekaji. Tulieni wasije kujichanganya na maandamano yenu. Hamasa yenu imetupa nguvu ya kuwakabili watekaji.
4. Ndugu zetu na ndugu zenu wametekwa na kutuumiza sote. Serikali yetu mnayoichukia na kuipenda itahakikisha wanapatikana na watatusaidia kujua mbinu za watekaji.
5. Maandamano ya 29/10/2025 yameleta madhara makubwa kwa taifa letu. Taifa limegawanyika na kuvimba kwa chuki. Hatupendi yarudiwe. Tumeubaini mwanya uliotumiwa na kuchelewesha serikali isishughulikie kero zilizobainishwa na tume na kugeuka kuwa vyanzo vya maandamano hayo. Tumejifunza. Tukae pamoja haraka na kupitia kero hizo.
6. Maandamano ni haki yenu. Haiwezi kuzuiwa na chombo chochote. Serikali haijashindwa kushughulikia madai yenu. Hata mkilazimika kuandamana kwa AMANI, Serikali itawalinda na kuwasikiliza. Ikiwa mnaweza kusikilizwa bila kuandamana, kwa nini kuandamana?
7. Vikundi vinavyojitokeza kuzuia maandamano na kuzungumzia masuala ya ulinzi na usalama, havijatumwa na serikali. Vikundi hivyo vina haki kuonyesha mapenzi na uzalendo bila kuingilia masuala ya ulinzi na usalama. Mamlaka husika zinashighulika navyo.
8. Tunao wajibu wa kulitetea taifa letu ili liendelee kuvutia watalii, mitaji na uwekezaji. Makundi ya “vigilante”, “militia”, “wasiojulikana”, “redbrigade”, “green guard”, “panya road” nk vinalichafua taifa na kuvutia ugaidi nchini. Picha za polisi wenye silaha si kivutio cha utalii. Aidha wahalifu wa fedha na haki za binadamu wanajificha humo. Serikali inaonya vikundi hivyo kuacha mara moja.
9. Bajeti ya serikali ndo kwanza imepitishwa. Inalenga kupunguza ukali wa gharama za maisha na ajira kwa vijana. Tuipe fursa bajeti hii ili ianze kazi ya kutatua kero hizo. Wakati huo huo milango iko wazi kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kero hizi zinazolalamikiwa.
10. Malalamiko ya wanaopanga kuandamana kupiga uhalali wa serikali tumeyasikia. Aidha maamuzi ya nchi za magharibi pia tumeyasikia. Madai yote ya ukweli na uwajibikaji tumeyapokea. Serikali imeanza mazungumzo ya kidiplomasia na nchi za magharibi kuhusu masuala hayo. Serikali iko tayari kushiriki mazungumzo ya ndani ili kutafuta muafaka wa madai haya. Serikali inaamini maandamano juu ya suala hili yangefanyika baada ya kushindwa kwa mazungumzo.
Serikali inayokubali kushindwa na raia wake ndiyo serikali makini. Kutunisha misuli na kutumia magenge ya “Mbwa Mwitu” ni sifa ya serikali za kibabe zinazoongozwa na magenge ya madawa ya kulevya. Tusifike huko."
Je Nini maoni yako?