Haji Manara amtaka Rais wa Yanga, Eng. Hersi kuitisha Kikao kujadili kauli ya Rais Karia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amezungumzia sakata la mechi ya dabi ya Kariakoo pamoja na kauli ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, kuhusu ombi la Yanga SC la kutaka Bodi ya Ligi ijiuzulu.

IMG_3563.jpeg

Soma: Manara amchana Rais wa TFF, Wallance Karia, adai anakiburi cha madaraka ya kulevya

Akizungumza na waandishi wa Habari, Manara ametoa wito kwa Kamati ya utendaji ya klabu hiyo kuitisha mkutano wa dharura kujadili kile kilichonukuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ndugu Wallece Karia juu ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu mpira wa Tanzania.

"Usitumie kiburi cha uongozi kuwadhalilisha wenzio kwasababu wametumia kanuni, bila heshima Karia unaukosea Mpira na unaikosea Yanga. Na viongozi wa Yanga najua hawawezi kukwambia kwasababu utawafungia na katika hili omba radhi kwa kufuta kauli zako za jana" — amesema Manara kufuatia kauli ya Rais wa TFF Wallace Karia

"Nazungumza kwaniaba ya wana Yanga tena ni mjumbe wa mktano mkuu kikanuni, kamati ya utendaji chini ya Rais wetu Hersi iitishe mkutano mkuu wa Dharura ajenda iwe moja tu kujadili hili sakata tutoe maazimio ya mkutano mkuu" amesema Manara
 
Yanga mshakuwa makumbusho ya bagamoyo sasa.
Tff ina shabikia mashujaa united sasa
 
Kati ya jambo analokosea manara ni kutotambua ukishakuwa na Manara Tv hutakiwi Tena wewe mwenyewe Haji Manara kama mkurugenzi kuwa na mijadala mingi. Kila kitu ushaenda kuhojiwa Manara Tv kushambulia, kukosoa au kupongeza. Kwann hajifunzi Kwa Millard Ayo
 
Huyu albino anajiinua sana. Kwani yeye nani hadi ameshauri eng. Hersi??
 
Yanga lazima watecheza hiyo mechi kwasababu inaongozwa na watu wajanja wajanja wa mjini kama Eng. Hersi. Hapa wanawapotezea tu muda mashabiki wa Yanga. Hersi hawezi kusimama imara kutokana na sababu nyingi zikiwemo kuutaka ubunge na kulinda maslahi ya biashara. Huyu huyu Hersi agome kuipeleka Yanga uwanjani, Thubutu! Ninalo liona kuna baadhi ya viongozi wa Simba watepewa adhabu ili kujenga daraja la aina flani ya maelewano.
 
Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amezungumzia sakata la mechi ya dabi ya Kariakoo pamoja na kauli ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, kuhusu ombi la Yanga SC la kutaka Bodi ya Ligi ijiuzulu.

View attachment 3274361

Soma: Manara amchana Rais wa TFF, Wallance Karia, adai anakiburi cha madaraka ya kulevya

Akizungumza na waandishi wa Habari, Manara ametoa wito kwa Kamati ya utendaji ya klabu hiyo kuitisha mkutano wa dharura kujadili kile kilichonukuliwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ndugu Wallece Karia juu ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu mpira wa Tanzania.

"Usitumie kiburi cha uongozi kuwadhalilisha wenzio kwasababu wametumia kanuni, bila heshima Karia unaukosea Mpira na unaikosea Yanga. Na viongozi wa Yanga najua hawawezi kukwambia kwasababu utawafungia na katika hili omba radhi kwa kufuta kauli zako za jana" — amesema Manara kufuatia kauli ya Rais wa TFF Wallace Karia

"Nazungumza kwaniaba ya wana Yanga tena ni mjumbe wa mktano mkuu kikanuni, kamati ya utendaji chini ya Rais wetu Hersi iitishe mkutano mkuu wa Dharura ajenda iwe moja tu kujadili hili sakata tutoe maazimio ya mkutano mkuu" amesema Manara
Kumbe bado anaisemea yanga
 
Back
Top Bottom