Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.
Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.
Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?[/QUOTE
Ndoto za namna hiyo zinatokana na maisha na athari ya kisaikolojia iliyojengeka wakati ukiwa kidato cha nne au wakati ukijiandaa kwa mitihani, fikra/hofu zako ulizielekeza sana kwenye tukio hilo hivyo kujijenga katika memory. wengi hupatwa na tatizo hilo,ambapo wengine huota mara kwa mara wapo shule wakiwa assembly wakicheza mpira, darasani n.k japo wamemaliza miaka kadhaa iliyopita, na ndoto nyingi huhusisha maisha ya sekondari.