Haipiti wiki naota napiga pepa la form 4

Haipiti wiki naota napiga pepa la form 4

Nilivokuwa kidato cha tano nimewahi kuota nimefeli somo moja kwenye mtihani wangu wa kidato cha sita kilichokuja kutokea lile somo matokeo yake yalikuja kuwa suspended kwa sababu ya continuous assesment nilijiuliza sana uhusiano wa kile nilichokiota mwaka mmoja kabla ya tukio na tukio lenyewe mpaka hivi sijapata maana yake.
Note.baada ya academic master kushughulikia matokeo yalitoka nikiwa nimefaulu
Ndoto ni taarifa ya mambo yanayowahusu binadamu. Sema huwa tunapuuzia sana ndoto ndo mana mambo tuliyoyaota yanatutotea. Unapoota ndoto ukichukua hatua jambo hilo linaweza lisitokee, japokuwa kuna ndoto za taarifa ambazo hata ukiomba matokeo yake hayabadiliki na ndoto kama hizi zinakuandaa kukubaliana na jambo litakalitokea hata kama litakuwa la maumivu km kufiwa na ndugu wa karibu. Kwahiyo ni muhimu kufuatilia ndoto tunazoota
KIIMANI KUNA JARIBU UNAPITA UNAKUMBUSHWA UCHAKARIKE ULIVUKE..

KUNASEHEMU/KIUCHUMI/KIKAZI/ ETC UNATAKIWA KUFIKA LAKINI UMEBAKI STAGNANT.

NDOTO YA NAMNA HIYOO NI NZURI UKIJIONGEZA TU UNATOBOA KIU YA UNACHOHITAJI KWA MDA MREFU.

SALIIIIIIIIIIIIIIIIII

MUHIMU: FATA HUU USHAURI UKIFANIKIA USISAHAU KULETA MREJESHO.

Nilikuwa na hii hali sana sana, ila ikaisha, Ila kwa kweli kila nilipokuwa naifanya nilikuwa na matatizo, yani haijawahi kuwa rais, ila hii hali iliisha. Pia kila wakati nilipokuwa naota, nilikutana na changamoto ngumu na zilinitesa sana. Hakuna anayekuloga wala, we mwombe Mungu na angalia kazi yako au biashara yako au chochote unachokifanya, kifanye kwa makini na mwombe Mungu akusaidie.
 
Ndoto yako kiimani ina maana sana. Huenda kuna stage au jambo ulitakiwa kulifanya au uliruka huko nyuma na wakati wa kulifanya jambo hilo umefika na hujui cha kufanya. Ndio maana unaona ndoto yako unaota hujui cha kujibu au umechelewa. Na ndoto kujirudia zaidi ya mara 2 ina maana kubwa sana usipuuze kabisa tafuta msaada kwa watumishi au watu wenye hekima wakusaidie maana ya ndoto hiyo ili uvuke sehemu uliyokwama ktk maisha yako.
NB. Unaweza kufatilia semina ya Mwl Mwakasege Dodoma anafundisha somo la ndoto.
 
Na mimi ndoto kama hii huwa inanitokea sana, najiulizaga lkn huwa napuuzia baada ya mda, sasa hapa umenifanya nitafakali upya,, kunakitu tunakisea kwenye maisha.
Tupo wengi Mkuu, hata mimi mara kadhaa, tena katika level tofauti, leo nikiota, primary, olevel alevel....
 
Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.

Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.

Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?
Utakua na nyota ya ualimu
 
Muhimu sana kama uko maeneo ambayo redio sauti ya injili inashika ebu sikiliza semina ya neno la mungu na christopher mwakasege na somo lake la ndogo kuanzia saa 11 jioni itakusaidia sana tusidharau ndoto ni ulimwengu mkubwa sana ambao hatujui
 
Katika ulimwengu wa kiroho ni ishara kuwa umekwama kimaisha. Unaweza ukaona kama mbona upo poa lakini inaashiria hata hapo ulipofikia unaweza kwenda mbele zaidi kimaisha. Hii ndio maana yake.

Sasa kwa nini urudie kuota mara kwa mara? Hii ina maana kwamba kuna maandalizi kabambe unatakiwa kufanya ili uvuke hapo ulipokwama. Ukishayapatia tu hayo maandalizi ndoto hutoweka. Ningekuwa nafahamu maisha yako halisi ningeweza kupata idea ya nini unachopaswa kufanya so far. Ukishamaliza kujiandaa vema na ku exploit vizuri hio outcome ya maandalizi yako then mambo yako yananyooka sawa na namna inavyopaswa kuwa.

Hii ni taarifa muhimu sana katika mwenendo mzima wa maisha yako. Unapaswa kumshukuru Mungu sana kwa taarifa hii nzuri inayokuonyesha nini cha kufanya.

Kwa nn ndoto ni ya f4 na sio drs7 na sio f6 na sio UE ilhali umepitia mitihani ya chuo? Jibu ni kwamba inaashiria daraja ama uwezo ama uzito wa maandalizi ya kufanyika. F4 ni four years hivyo maandalizi ni ya muda mrefu kidogo kulinganisha na f6 ambayo ni 2 years ama chuo ambayo probably ni 3 years to 4 to 5 years.

Tahadhari: Kuna ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili. Hii tafsiri ni ya ulimwengu wa kiroho. Kuna wengi hawataweza kuelewa hii tafsiri.
Huwa naota sana hiyo na kuna kipindi nilijikuta nimeacha kazi mambo yakawa magumu sasa nikazidi kuota mara nyingine usiku mmoja naota hiyo ndoto zaidi ya mara tatu...dah umenigusa sana kwa tafsiri hiyo


Cc Fredom tommorrow
 
EXAMINATION DREAMS
In examination dreams, which Freud
considered to be "typical dreams," the
dreamer sees himself back at school taking
an examination.
Freud mentions this type of dream several
times in The Interpretation of Dreams (1900a).
The dreamer is embarrassed to see himself as
an adult among much younger fellow
students and obliged to retake an
examination that he already passed a long
time ago. "It would seem, then, that anxious
examination dreams (which, as has been
confirmed over and over again, appear when
the dreamer has some responsible activity
ahead of him next day and is afraid there
may be a fiasco)" (1900a, p. 274). The
meaning of the dream would be: "Don't be
afraid of tomorrow! Just think how anxious
you were before your Matriculation, and yet
nothing happened to you"
Note. Ndoto hii huwajia watu walio pasi mtihani tu. Kamwe mtu aliyepiga f f f f haoti ndoto ya kurudia mtihani!
Exactly.
 
Unatakiwa umuombe Mungu sana,anka ucku omba,kemea nguvu na upinzani wa shetani ktk maisha yako
 
Huu Uzi WA mleta mada ni WA muhimu sana ,MTU anaweza ona ni utani Ila ni kweli ndoto hizi hata Mimi zinanitokea,pamoja na kuwa nimemaliza medicine bachelor...
[HASHTAG]#msaada[/HASHTAG] Tafadhali Ndugu.
Kunawakati nilikuwa naota naokota shilingi mia za safaru barabarani nipo na wenzangu wao hawazioni mm ndiye naepekenyua kwenye mchanga na kuokota nyingi mmno kila tunapokuwa tunapiga hatua tukitembea na haziishiiiii mchangani...
Omba sana Mungu aifungue hio milango ya pesa
 
Me nilikua naota sana hizo tena moja ya sifa zake unajiona kabisa kichwa empty na paper imeshafika haujajiandaa nikamuuliza dada mmoja hivi mlokole akaniambia level ya elimu uliuokua nayo haitoshi unatakiwa usome tena inawezekana wakati uko unakua uliweka malengo makubwa sana ku achieve kielimu for me seems to be soundable
Mi karibia kila siku naota nipo shule, ila dah sina hata mpango wa kusoma kwakweli
 
Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.

Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.

Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?
Mkuu niko km wewe asee.
 
Back
Top Bottom