Haipiti wiki naota napiga pepa la form 4

Haipiti wiki naota napiga pepa la form 4

Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi. Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia. Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?

Katika ulimwengu wa kiroho ni ishara kuwa umekwama kimaisha. Unaweza ukaona kama mbona upo poa lakini inaashiria hata hapo ulipofikia unaweza kwenda mbele zaidi kimaisha. Hii ndio maana yake.

Sasa kwa nini urudie kuota mara kwa mara? Hii ina maana kwamba kuna maandalizi kabambe unatakiwa kufanya ili uvuke hapo ulipokwama. Ukishayapatia tu hayo maandalizi ndoto hutoweka. Ningekuwa nafahamu maisha yako halisi ningeweza kupata idea ya nini unachopaswa kufanya so far. Ukishamaliza kujiandaa vema na ku exploit vizuri hio outcome ya maandalizi yako then mambo yako yananyooka sawa na namna inavyopaswa kuwa.

Hii ni taarifa muhimu sana katika mwenendo mzima wa maisha yako. Unapaswa kumshukuru Mungu sana kwa taarifa hii nzuri inayokuonyesha nini cha kufanya.

Kwa nn ndoto ni ya f4 na sio drs7 na sio f6 na sio UE ilhali umepitia mitihani ya chuo? Jibu ni kwamba inaashiria daraja ama uwezo ama uzito wa maandalizi ya kufanyika. F4 ni four years hivyo maandalizi ni ya muda mrefu kidogo kulinganisha na f6 ambayo ni 2 years ama chuo ambayo probably ni 3 years to 4 to 5 years.

Tahadhari: Kuna ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili. Hii tafsiri ni ya ulimwengu wa kiroho. Kuna wengi hawataweza kuelewa hii tafsiri.
 
Nakuunga mkono mkuu, kama ni mkristo baada ya kutoka kuota hivyo kemea sana ndoto hiyo..Mungu ni mwema.
Hii ndoto siyo ya kukemea, muotaji anakumbushwa kuwa hajakamilisha ratiba yake, kuna mitihani bado hajaivuka, inaweza kuwa Elimu, Kazi, hali ya kiroho chake na hata maisha yake kwa ujumla, anatakiwa kuchukua hatua. Kama ni shule maana yake kuna level anatakiwa kwenda, kama ni hali ya kiroho bado kuna hatua za kuchukua ili kusonga mbele, kama hali ya maisha kuna hatua za kuchukua na kuvuka kwenda mbele.
 
Me pia Niko mtaa napambana but naotaga napiga pepa la form 4 maala mdaa unakata naamka mda mwingine naota Niko na washkaji wa olevo au primary darasani ticha agawa pepa akifika kwangu ndoto na kata sijui ikoje hiyo japo nilisha malizaga chuo since 2013 napambana na mji wa yesu wa dar
 
Kumbe ni wengi
Me nilikua naota sana hizo tena moja ya sifa zake unajiona kabisa kichwa empty na paper imeshafika haujajiandaa nikamuuliza dada mmoja hivi mlokole akaniambia level ya elimu uliuokua nayo haitoshi unatakiwa usome tena inawezekana wakati uko unakua uliweka malengo makubwa sana ku achieve kielimu for me seems to be soundable
 
Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.

Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.

Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?
Hii ndoto nimekuwa niiota sana karibu kila mwezi ila nachuliaga poa,naotaga nakaribia kupiga paper lakn sina maandalizi kabisaa..yaani ni kama ulivyoeleza.Walau na mimi nimepata mafunzo leo.
 
Form four hukupata bashite... ukarudia mtihani mkuu?
 
Form four hukupata bashite... ukarudia mtihani mkuu?
Hapana mkuu nilifaulu nikachaguliwa kuendelea na A-Level, sikuwahi kuwa kilaza wa kiwango hiko
 
  • Thanks
Reactions: cai
Dahh! naona intellectuals wanaota mambo mazito kweli. Tusio na elimu wala familia tunaota ndoto nyevu tu! sijui hata zina maana gani!! Mnitafsirie tafadhali
 
Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.

Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.

Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?
Ukiona hivyo ujuwe kuna BASHITE anatumia VYETI VYAKO...aisee una hisia kali sana wewe...lazima kuna BASHITE anafanya hayo unayoyawaza wewe na kuota
 
Dahh! naona intellectuals wanaota mambo mazito kweli. Tusio na elimu wala familia tunaota ndoto nyevu tu! sijui hata zina maana gani!! Mnitafsirie tafadhali
Hizo hata ukiota deile mbona raha tu
 
Jamaa yangu yani Mimi naota hadi primary na chuo ,Mara nyingi chuo aisee .....
 
Kuna Mwalimu mmoja wa Biblia anaitwa Mwakasege yupo dodoma anaendesha semina yupo live youtube fuatilia anasomo hili la ndoto. jinsi ulivyoandika ni kama ulikuwepo alitoa mfano wa ndoto yako. Mcheki Youtube kama utapata ya juzi na jana. Ipo poa sana.
 
Huu Uzi WA mleta mada ni WA muhimu sana ,MTU anaweza ona ni utani Ila ni kweli ndoto hizi hata Mimi zinanitokea,pamoja na kuwa nimemaliza medicine bachelor...
[HASHTAG]#msaada[/HASHTAG] Tafadhali Ndugu.
Kunawakati nilikuwa naota naokota shilingi mia za safaru barabarani nipo na wenzangu wao hawazioni mm ndiye naepekenyua kwenye mchanga na kuokota nyingi mmno kila tunapokuwa tunapiga hatua tukitembea na haziishiiiii mchangani...
 
m
EXAMINATION DREAMS
In examination dreams, which Freud
considered to be "typical dreams," the
dreamer sees himself back at school taking
an examination.
Freud mentions this type of dream several
times in The Interpretation of Dreams (1900a).
The dreamer is embarrassed to see himself as
an adult among much younger fellow
students and obliged to retake an
examination that he already passed a long
time ago. "It would seem, then, that anxious
examination dreams (which, as has been
confirmed over and over again, appear when
the dreamer has some responsible activity
ahead of him next day and is afraid there
may be a fiasco)" (1900a, p. 274). The
meaning of the dream would be: "Don't be
afraid of tomorrow! Just think how anxious
you were before your Matriculation, and yet
nothing happened to you"
Note. Ndoto hii huwajia watu walio pasi mtihani tu. Kamwe mtu aliyepiga f f f f haoti ndoto ya kurudia mtihani!
mkuu hata mm nilikua naiotaga hio ndoto ....mm nikahisi ndio najitabilia future yangu kwamba cku moja nikifanya mtihani mwingine nitaferi..
kumbe maana yake ni hio..
afadhar hofu imenitoka
 
Back
Top Bottom