screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,829
- 15,791
Salaam ndugu wanajukwaa natumai mu wazima. Tatizo langu ni moja tu, ni tatizo ambalo limekuwa likinisumbua tangu mwanzoni mwa mwaka labda pengine jukwaa hili la madokta naweza pata ufumbuzi.
Yaani pamoja na kuwa nimepata digrii ya halali bila kufoji vyeti miaka zaidi ya mitano iliyopita ila bado naandamwa na ndoto ambayo imekuwa ikinipa tabu sana, wakati mwingine naota kesho ndio pepa la necta halafu sijasoma kabisa, wakati mwingine ndio nimeanza pepa halafu hakuna nnachojua, wakati mwingine nimechelewa kuingia kwenye pepa, yaani pepa linakaribia kuisha mi ndo naingia.
Nikistuka najiskia vibaya sana kwa muda halafu fahamu zikiniijia nafurahi kwamba kumbe hiyo stage nilishavuka kitambo. Nini chanzo cha ndoto hizi, na kwanini zimeanza mwaka huu na zimekuwa zikijirudia rudia?