Hainaga digirii

Status
Not open for further replies.
Lakini kweli bana.....
Umeona mkuu, sema Da Sophy na b2k wamejikita sana kwenye suala la kusoma.

Mara nyingi unakuta mtu anasema yaani mme wangu katembea na housegirg? wanasahau kwamba jambo la kwanza kabisa Housegirl ni mwanamke, Housegirl ni kazi anayofanya na haimtofautishi yeye na anayefanya kazi nyingine kuwa wanawake. Na wala haimaanishi mtu kuwa house girl havutii au hana sifa alizonazo anayefanya kazi nyingine.

Ni eneo pana sana, isingekuwa vema kuwalaumu wenye degree na matokeo yake huenda ikaleta maana kwamba mleta uzi anachuki binafsi na wasomi.
 
Last edited by a moderator:

Mhhhh na wanaume wa style hizi wakipata watoto utackia hamna kuolewa hadi umalize chuo upate degree uwe na kazi yako....nyooooo ila mtoto wa mwenzio umuoe akiwa na certificate..shame on u
 
aah wapi
pamoja na changamoto zote tunazopitia Elimu ni muhim kwa mtt wa kike hii yote ni ktk kumjengea uwezo wa kujitegemea.

so ukipata opportunity ya kusoma itumie.kuna wengi tu huko mtaani wanatamani kusoma wamekosa nafasi kwa sbb mbalimbali.
na mashirika mengi duniani yanafanya kila jitihada kumkomboa mtt wa kike kielim, kwani hawajui kuwa hao watt wa kike wana papuchi?

hayo mambo ya kuringa ni hulka tu!
kuna wanawake wamesoma sn na wako poa.

ladies pigana mpaka kieleweke.


if u think education is expensive try ignorance! !!!
 
MAsikini wa Mungu...wasio na digriii mtaji wao papuchi ndo maana povu linawatoka...

Wakati wenye digriii hiyo ni starehe kama starehe nyingine ...wao hiyo ni ajira wako tayari waiendee hata kwa sangoma...

wasamehe bureee...


The thing is, there is life outside kuonjeshana chumvi. Na hapo ndo umuhimu wa degree unapojulikana.
 

Shosty umeingia chaka. Sicho nlokisema. Nnesema hainaga digirii na ni ukweli upende usipende utake ustake. Kwani hao wene digirii hebu kawaulize kama mama zao wana hizo digirii, mbona wao wamepata digirii ambazo mama zao hawana? Jibu ni kwamba mama zao wana nidhamu ya unyumba, wametulia ndicho kimewezesha wao kupata maendeleo. Ndipo nkasema kama unadhani digirii ndo kila kitu na kwamba eti aso nayo kakosa yote imekula kwako na mfano nimekupa. Kama una jengine uliza uzuri usije na nyodo lakini.
 
Nimeipenda hii...so wenye shahada wanaingia chumbani kidegree degree wakati non commissioned mnashughulika vilivyo sioooo...i see!
 
Naomba nikuulize bila nyodo, mwanamke kuwa na digrii ni hasara?

Kama mama hana digrii na mtoto asiwe na digrii? Au kama mzazi aliwakuza kwenye nyumba za kupanga, na mtoto akuze wanawe kwenye nyumba za kupanga?


Na je, hakuna wanawake wenye digrii waliofanikiwa kwenye ndoa zao?

Labda kitu cha mwisho, mwanamke unampa nafasi gani katika dunia ya leo? Unaweza kunijibu mtazamo wako wa nafasi ya mwanamke katika mahusiano, na nafasi ya mwanamke katika jami kwa ujumla.

 
MAsikini wa Mungu...wasio na digriii mtaji wao papuchi ndo maana povu linawatoka...

Wakati wenye digriii hiyo ni starehe kama starehe nyingine ...wao hiyo ni ajira wako tayari waiendee hata kwa sangoma...

wasamehe bureee...

Mwenye digirii na aso nayo wote wana papuchi. Tatizo la baadhi wa wadigirii ni kujisahau wakidhani midhali washavekwa digirii basi wamemaliza yote. Hapo ndipo wanapopigwa bao, na badala ya kuangalia walipojikwaa wanalaumu walipoangukia, ndo chanzo kuona hata wengine wanadiriki kutafuta mbinu za kufukuza mume. Hata ukafukuza mume ukabaki na digirii yako sanasana utakuwa mlevi wa pombe tu. Kwani wangapi tumewaona wamejishusha bei hadi kwa wauza mikaa wanajiparamisha almurad wapoze hizohizo papuchi unazozisemea. Kusitirika ni zaidi ya digirii nakuambieni. Huyo unomfukuza kwako kwa kujiona digirii yako ni zaidi yake, kuna mwenzio akimpata haoni digirii, yeye anaona mwanaume kwanza digirii ziada tu. Ndo nnachokuambieni.
 
wewe una shida umekutana na wenye degree wangapi ambao wanafanya unachokisema?research yako uliifanyia wapi?kama inakuuma sana na wewe kamata shule uwe na hiyo degree!tunalia kila siku mtoto wa kike apewe nafasi ya kwenda shule we unaleta ujima wako hapa!akili zako zimekaa eneo moja tu la mwili!imekuuma saana nenda shule!
 
Nahisi sijawahi kukuelewa mantiki yako, au huwa najikanganya.

Ni kuwa unaipa papuchi nafasi kubwa sana kwenye mahusiano ya ndoa au unaona papuchi haina nafasi kivile? Au unajaribu kuonesha kuwa wanawake wote ni sawa as long as wote wana papuchi?

Nisaidie kunijibu hili nitaelewa, nafasi ya tendo la ndoa kwenye ndoa ni ipi?

 
Msomi ni msomi tu, lazima kunatofauti ndo maana huyo mwanaume hakukuoa ww ngumbaru akaoa mwenye degree,
nadhani alihitaji watoto wake wapate maisha mazuri, wasome shule nzuri na hata ikitokea akafa waendelee kupata huduma. Mtoa mada sijui umenielewa?
 

Nakujibu moja baada ya jengine kama ulivouliza. Mwanamke kuwa na digirii ni faida, lakini sio haimalizi kila kitu katika kumkamilisha kama mwanamke. Awe na digirii yake lakini ajue digirii haikuumbwa, kaisomea tu imsaidie lakini yeye ni mwanamke, alinde utu wake wa kike. Asikubali digirii ikampora uhalisia wake wa kike.
Hata kama mama hana digirii, anapaswa kujitahid wanawe wapate maendeleo makubwa ikiwemo hiyo digirii, lakini pia awalelee vyema watakapopata hiyo digirii isije ikawapoteza, maana wapo walopotezwa na digirii zao wenyewe. Ni kama kumnunulia mwanao gari halafu akaliendesha rafu likamuua. Gari ni faida lakini kifo ni hasara. Kwa hivo lazima umsaidie mwanao maendeleo yasimpotoshe.
Wanawake wenye digirii waliofanikiwa katika maisha yao ni wale walotambua kuwa ndoa hainaga digirii, na kwamba digirii haitunzi mume.
Nafasi ya mwanamke katika jamii wala si ya kuuliza, ni kubwa. Lakini akiweka mbele kiburi na nyodo kuwa ati nina digirii sijui kitukitu gani hiyo nafasi mwenzangu nakwambia itamshinda. Sasa kama digirii unaitumia kuvunja nyumba yako, hapo ndo umeienzi nafasi ya mwanamke au umechemsha dada hebu sema mwenyewe. Na kama kwa digirii hiyo, hata unapokosea hujikubali kurekebika ati kisa digirii, sasa hiyo ni digirii au majanga? Bibiye unapoishi na mwanaume elewa ana hisia, usipomjali lazima atapindukia kule anapopata wa kumjali. Basi kama la kumjali limekushinda, mshukuru yule aliyekusaidia kumjali, hili nalo linahitaji digirii? Watoto wa mumeo ni wanao, hili nalo unapinga? Kama ukipinga wanao mwenyewe watakuumbua maana watasema hawa ni kaka zao. Kama digirii yako haikusaidii kutambua hili, ni ya kazi gani hiyo digirii? Mwanamke tumia digirii yako kujenga jamii si kubomoa, likikushinda hili basi digirii zako ni bure.

Uliza jengine. Leo nipo kujibu maswali.
 
Mmmh hii kali! kusema kote huko na majivuno ingekuwa kitu cha maana basi kumbe kushobokea wanaume! Ujinga mtupu, hapo ndio wanaume wanapotake advantage kwa wanawake nakututumia vibaya sana. Hapo ndio umuhimu wa shule ulipo kuchanganua mchele na pumba unajisifu kutumiwa???? DUH UMILEMEBE WA HALI YA JUU!!!
 

King'asti:kwanza nimecheka sana,kila nikitaka kucomment naona napoteza muda kwenye hakuna;thanx umenisaidia kwa baadhi ya majibu.wataishia kupangiwa mikao mbali2 kitandani na kuita fundi bomba etc ila wakati wa mipango ya maana watatafutwa wenye degree zao na
 
Nimkupata kabisa, tuko sawa hapa.
Labda swali la nyongeza, huu 'utu wa kike' ni ukoje? Unapimwaje? Na unadhani unafanana dunia nzima?
Au utu wa kike wa Saudi Arabia ni sawa na utu wa kike wa Italia?

Nimekubaliana na wewe kabisa hapa, sina swali


Hivi kutokubali kurekebishwa ni sababu ya digrii au ni tabia ya mtu?
Hamna wanawake wasio na digrii na bado wana kiburi na wabishi?
Au unamaanisha kuwa digrii inampa mwanamke nafasi ya kuonesha kiburi chake zaidi? Lakini wakati huo huo kiburi ni nini? Ni mambo gani mtu afanye yakubalike ni kiburi na mengine yakubalike ni kulinda nafasi yake kama mke?

Bibiye unapoishi na mwanaume elewa ana hisia, usipomjali lazima atapindukia kule anapopata wa kumjali. Basi kama la kumjali limekushinda, mshukuru yule aliyekusaidia kumjali, hili nalo linahitaji digirii?.
Halihitaji digrii kwa kweli, labda nisaidie kuchora mstari, niruhusu hadi wapi ili nionekane namjali na si mtumwa tena? Kuna mwanamke alikuwa anampa GoTi mmewe ili asiachike. Alionyesha kujali kwa hali ya juu, lakini was it worthy?

Ha ha a ha, Da Sophy bana. Kukubali mtoto wa nje wa mme ni matokeo ya mambo mengi, makuzi yanachangia sana. Kama umetoka kwenye jamii ambayo mitala ipo, sio ish kukubali mtoto wa nje wa mme. Na hii wala haihusiani na digrii kabisa, hii inahusiana na hisia zaidi. Ukute nyie mnamwambia akubali watoto wa nje wa mumewe wakati yeye bado yuko kwenye maumivu makali, is it fair? Jivalishe viatu vyake uone.
Ujue ni rahisi sana kushea mume ukiwa nyumba ndogo, kwa nini? Sababu unajua fika nyumba kubwa ipo na umekubali ukiwa unajua hilo. Ila ni vigumu sana kuwa nyumba kubwa wakati kuna nyumba ndogo, ni dhahiri kabisa 'nchi' yako onakuwa imeingiliwa. Ni sawa na rais wa nchi asikie kuna mtu mwingine kajotangaza rais wa nchi hiyo hiyo. Kwa hapa, jaribu kumpa muda huyo mnayeshea naye. Ukweli ukiingia akili na kukubaliana na matokeo hamtagombana kiasi kikubwa, utabaki wivu wa kike wa kawaida tu.
Ni sawa na wewe usikie sasa hivi huyo bwana ana ingizo jipya na wamezaa, utajisikiaje?

Labda nikuulize, je ulipoamua kuwa na uyo bwana, ilikuwa sababu ya kumkomoa mkewe au mlipendana tu? Kama sababu ilikuwa kumkomoa mkewe, basi endelea kumfanyia huyo bi mkubwa kila aina ye sinema, sababu ndio lilikuwa lengo.

Ila kama sababu nimlipendana nyie kwa raha zenu, msaidie mwenzio maisha yake yawe marahisi. Labda hata hukujua kama mkewe ndiye huyo, angeweza kuwa mwanamke mwingine yeyote. Kwa hiyo kiuhalisia wewe na huyo nyumba kubwa hamna ugomvi, ila aliyewakosanisha ni huyo mwanamme. Na kama umeshamauumiza kwa kumchukua mumewe, sasa ya nini azidi kuumia kwa vitimbi? Hivi unadhani ukimuona chini ya futi 6 utafurahi? Unaweza furahi kwa muda ila mbeleni kuna muda wa kujuta, si unajua ujana nao una mengi. Mchunie tu, hata kama ana vitimbi, tayari wewe ushabeba kombe, unaweza kuta hata mengine anayafanya akiwa hajui.
(Nimetumia nafsi ya pili -wewe, simaanishi wewe kama wewe, ni ili tu ujumbe wangu ufike)
 

mindset ya kitumwa hiyo mwanaume mwanaume we mwwnamke unadekezwa na nani?
 
Hivi viungo vyenye chumvi navyo wanatumia kufanya application ya job eh!!!
Wivu Ni dhambi kubwa sana. Msameheni huyu.
Watu wanajuta Kwa kukosa fursa ya elimu, wengine ndo kwanza Hata hawajutii. Utatumia kiungo cha chumvi lakini hakitathibitshwa na TCU hahaaaaaaaaaaaaa
 
Alipokuwa anasoma mwenzio wewe ulikuwa unafanya mazoezi ya kwa bed sio.Mwache aringe na digrii yake,usimwonee gere.Wewe utabaki na hako ka utamu kako,wajanja wajisevie wasepe.
 
Da sophy usiwe unapotea sana bwana, tunakumiss mnooo.
Anyways, mie mamangu pia alikuwa na madigirii, mengine hata hajayatumia vizuri aka- rip. na yeye kakaa kwenye ndoa yake hadi mwisho, na mie pia inshaallah ntakaa.
Kwako nyodo zinakuwa kama nini vile? What makes you decide hii ni nyodo na hii sio?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…