Haina majotro maana yake ni nini?

Dio

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
1,274
158
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu,
kuna kitu kinanitatiza kwenye tangazo la bia moja wanaslogan inayosema
"HAINA MAJOTRO"
mimi mpaka leo sijajua maana ya hilo neno,na hata nikiwaeleza watu wanaopenda kulitumia hili neno hawanipi jibu la kuniridhisha,ndio maana nikaamua kuleta hapa kwa great thinkers wanisaidie kupata jibu
asanteni.
 
Nenda baa ya hapo jirani halafukunywa kama chupa tano mfulilizo then utapata jibu
 
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu,kuna kitu kinanitatiza kwenye tangazo la bia moja wanaslogan inayosema"HAINA MAJOTRO"mimi mpaka leo sijajua maana ya hilo neno,na hata nikiwaeleza watu wanaopenda kulitumia hili neno hawanipi jibu la kuniridhisha,ndio maana nikaamua kuleta hapa kwa great thinkers wanisaidie kupata jibuasanteni.
Sio slogan ya hiyo bia, ni slogan ya tamasha la FIESTA 2011/2012 linalodhamiwa na bia hiyo.
 
Haina Majotro aka Majasho=Haina noma=Hakuna Tatizo,yaani haina shida.
 
Hilo ni neno ambalo limeletwa mtaani ili liweze kupata mashiko, kama mengine mfano,,umefulia, masharabaro,masela etc, lakini pamoja na promo, halina mashiko kwa watu wenye akili zao na limebakiwa kutamkwa na wajinga wajinga tu.

kwa sasa linatumiwa na waandaaji wa fiesta,,baada ya fiesta litasahaulika.
 
Semi na Methali za wazee wetu wa kale zote unazijua ? Achana na maneno yanayoanzishwa na malimbukeni hua yanakuja na kupita kisha kusahaulika kabisaa.
 
222707_193621114017305_100001082538083_517397_1481312_n.jpg Haina Credit..........................................................................................................................
 
Asanteni kwa wote mliochangia kwenye uzi huu,angalau nimepata japo kamwanga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom