Haijawahi kutokea toka 1995, Hatimaye Lowassa apotezwa kisiasa

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Tokea mwaka 1995 jina Lowasa lilitawala media zote za Tanzani mpaka 2015 lakini kwa mwezi huu Machi 2017 Lowasa kapotezwa vibaya na DR Magufuli katika media za siasa hapa Tanzania. Hii inamaanisha kwamba Lowasa yupo hoi Kisiasa na tayari kuna tetesi na mikakati ya Wanachadema kuanza kumpotezea na wengine wameenda mbali na kumshauri Mzee wetu Lowasa kuachana na Siasa yaani Astaafu mambo ya siasa.

Katika zama hizi za Magufuli hakuna siasa za rushwa na magenge na hicho ndo kimempoteza Lowasa kabisa katika media za siasa
 
Lowassa apumzike umri umekwenda abaki kuwa mshauri .kuna vijana damu inachemka. Yupo Tundu Lissu machine .huyu kwangu anaimudu sana CCM na atamwangusha babu kipara 2020
Tatizo anayegombea urais kupitia chadema baada ya muda anafutika. Tundu asikubali hyo chance abaki kwenye ubunge.
 
Tatizo anayegombea urais kupitia chadema baada ya muda anafutika. Tundu asikubali hyo chance abaki kwenye ubunge.
Lissu atabaki kujifurahisha eti naye ni rais kwa sababu tu ni rais wa TLS, CHADEMA wenyewe hawawezi kufikiria hata kupendekeza jina lake, nchi haiwezi kuongozwa na mtu asiye na busara kama Lissu
 
Lowassa alikuwa moto wa Mabua
tuliwaambia Mbwembwe zitawaisha
Tunamsubiri huyo Lissu naye
 
Upepo hulazimisha Bendera kwenda unako elekea ila siasa kuonekana maana siasa anapo pesa jukwaa ahutubie kwa sasa hamna siasa za majukwaani ndo maana inaonekana lowasa hayupo lisu anasikika kwa kuwa mwanasheria sio kisiasa ili tujue uwezo wa kila mmoja inatakiwa wasimame jukwaani sio mmoja asimamae mwingine ajifiche
 
Tokea mwaka 1995 jina Lowasa lilitawala media zote za Tanzani mpaka 2015 lakini kwa mwezi huu Machi 2017 Lowasa kapotezwa vibaya na DR Magufuli katika media za siasa hapa Tanzania. Hii inamaanisha kwamba Lowasa yupo hoi Kisiasa na tayari kuna tetesi na mikakati ya Wanachadema kuanza kumpotezea na wengine wameenda mbali na kumshauri Mzee wetu Lowasa kuachana na Siasa yaani Astaafu mambo ya siasa.

Katika zama hizi za Magufuli hakuna siasa za rushwa na magenge na hicho ndo kimempoteza Lowasa kabisa katika media za siasa
Kama Lowassa kafutika kwenye media za siasa mbona hajafutika kichwani mwako? Hayo ni mahaba yako kwa Mzee Lowassa. Siumeona na thread unamuanzishia?
 
Lowassa ataendelea kuheshimika kwa busara na hekima. Ujuzi wake na ujanja katika siasa naona umezidiwa kidogo tu na Mzee JK. Kinachofuata licha ya kuwa ni hisia zangu tu ni kuwa Wazee hao watatengeneza bonge la counterattack itakayohakikisha "The Board" [Mtandao] kupitia chama fulani hivi inarudi na kutawala Tz. Hawatofanya tena kosa la kugombea fito. Hapo ndipo Tanzania mpya yenye uchumi endelevu, maendeleo ya dhati, PPP inayofanya kazi, furaha na amani itakaporejea ktk ramani. Kwa sasa tuendelee tu na hizi drama za Bandari, Bashite, mayala (Njaa), ukanda, vita vya ku blackmail washukiwa, kukimbia viongozi wa kidunia, BASATA, Policcm wasiojua sheria, mihimili mingine isiyochimbiwa sana chini kutojielewa majukumu yao.
 
Back
Top Bottom