Hai: DC Sabaya awataka Utumishi kueleza kwanini hawajapeleka majina ya Walimu waliostaafu Hazina

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amewapa siku tatu maafisa utumishi wilayani humo kuhakikisha wanatatua changamoto za waalimu wapatao 105 wanaodai malimbikizo ya fedha zao.

Aidha amebainisha kuwa fedha hizo ni pamoja na malimbikizo ya kupandishwa madaraja mishahara na fedha za kustaafu ambazo wamekuwa wakisotea kwa muda mrefu sasa bila kupata majibu ya Stahiki zao na barua kutofikishwa azina.

Akizungumza na waalimu hao wastaafu Mh lengai ole sabaya amesema kwamba serikali imekuwa ikijitahidi kulipa madeni lakini maafisa watumishi hao wamekuwa wakiwazungusha waalimu hao kupata mafao yao kwa makusudi wakiacha kupeleka barua zao kwa Katibu mkuu utumishi kuizinisha malipi yao.

Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya afisa utumishi Semati Lendina kukiri makosa yake ya kuacha kushughulikia barua za wastaafu hao na kumuomba radhi mkuu huyo wa Wilaya kwa kukiri kumekuwepo na uzembe juu ya utekelezaji wa madeni ya wastaafu hao.

Wastaafu hao wapatao 105 wanadai kiasi cha shilingi milioni 170 fedha zao za kupandishwa madaraja na zingine zikiwa ni fedha za mishahara pamoja na nauli za kuhamishwa eneo moja la kazi kwenda kwingine jambo lilopelekea kupeleka malalamiko hayo kwa Mkuu wa Wilaya.

Wameeleza kuwa kumekuwepo na madai kwa maafisa utumishi hao wamekuwa kikwazo katika kupata stahiki zao kutoka hazina jambo linalowapa kipindi kigumu katika maisha yao ya ustaafu.

Wakizungumzia malalamiko hayo mwalimu Eliamulia kisiri pamoja na Charles kimambo wamesema kwamba walistaafishwa kazi bila kupewa haki zao za msingi ikiwemo mishahara kabla ya kustaafu ikiwemo pamoja na malimbikizo ya kupandishwa madaraja pamoja na fedha za kustaafu.

Waalimu hao mbele ya mkuu wa Wilaya walionyesha barua zao mbalimbali ambazo wameandika wakidai stahiki zao bila mafanikio na zimekuwa zikiishia kwa maafisa utumishi bila kuwafikia mabosi wao ambao ni wizara ya elimu hususani mtendaji mkuu ambaye ni Katibu mkuu wa utumishi.

Hata hivyo Mara baada ya maamuzi hayo mkuu wa Wilaya alimwagiza afisa utumishi huyo yeye na wenzake wapatao watatu kujitathimini ni kwanini wasiwekwe ndani kwa masaa kadhaa kwa uzembe ndipo aliwasamehe Mara baada ya kukiri makosa na kusema kwamba huu ni mwaka wa baraka asingependa kumwona mtumishi wa serikali anaanza mwaka vibaya.

Afisa utumishi huyo akizungumza kwa niaba ya wenzake Semati Lendina aliomba radhi kwa kusema mkuu wa Wilaya naomba niombe radhi kwani tumeshindwa kufanyakazi ya kuwasaidia barua za wastaafu kufika kwa Katibu mkuu na kuagiza kulipwaa madeni yao.

Mwisho wa mjadala huo Mara baada ya mkuu wa Wilaya kusikiliza kero za waalimu wastaafu hao mbunge wa jimbo la hai Saashisha Mafuwe alisema wako tayari kusaidiana na mkuu wa Wilaya kwenda kwa pamoja ofisi ya Katibu mkuu kuomba waalimu hao kupata stahiki zao kwani walitumikia vyema serikali kipindi cha utumishi wao.

Mkuu wa Wilaya ameagiza hadi kufikia siku ya ijumaa saa nne asubuhi afisa utumishi awe amefikisha malalamiko ya waalimu hao wastaafu Ofisini kwake na baadae kufikisha kwa Katibu mkuu wa wizara ya utumishi kuomba kufanyiwa kazi malipo hayo.

IMG_20210111_155002_9.jpg
 

Mkuu wa wilaya ya Hai na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo imetoa siku tatu kwa Idara ya Utumishi kutoa maelezo kwanini kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili hawakufikisha Kwa Katibu Mkuu Utumishi na Hazina, nyaraka muhimu za walimu waliostaafu kwa zaidi ya Miaka Miwili sasa ili wapewe.

DC Hai Lengai Ole Sabaya ameitaja hatua ya Idara ya Utumishi kutopeleka taarifa za kupanda madaraja kwa walimu hao hadi wanastaafu na taarifa muhimu zinazohusu Madeni yao ya kufungasha mizigo kuwa ni jaribio la kuikosanisha Serikali na Watumishi wake na kwamba Serkali inayoongozwa na Rais Magufuli hakuna namna ingekosa kulipa Sh. Mil. 172 kwa walimu hao.

Ole Sabaya amesema pamoja na maelezo hayo baada ya siku tatu walimu wote waandikiwe barua na utumishi kuthibitisha madeni hayo na kwamba Ofisi yake itafanya mawasiliano na hazina kufikisha nyaraka zote za muhimu ili walimu hao wapate stahiki zao zilizocheleweshwa kwa uzembe wa watu wachache walioshindwa kufanya wajibu wao.
 
Katika maisha yafaa kuwatambua aina tofauti ya watu na kuishi nao kama Tabia zao zilivyo.

Wengine ni kuangalia hindi gani mambo yao yaende,wengine ni kazi yao danganya toto ndio kwenda mipango yao na kadhalika nakadhalika.
 
Katika maisha yafaa kuwatambua aina tofauti ya watu na kuishi nao kama Tabia zao zilivyo. Wengine ni kuangalia hindi gani mambo yao yaende,wengine ni kazi yao danganya toto ndio kwenda mipango yao na kadhalika nakadhalika.
Tunaomba urudie kusoma hii coment yako

Asante
 
Sifa zingine ni za Kijinga na Ulaghai..

Katika Taarifa ya Habari Saa 2 Usiku huu imerushwa habari ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Ole Sabaya pamoja na Mbunge feki wa Jimbo la Hai eti wamewakusanya akina bibi Waalimu Wastaafu kusikiliza Malalamiko yao kwamba hawajalipwa Mafao yao Tangu walipostaafu katika vipindi tofauti mwaka jana.

Sasa kituko ni anasingiziwa Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo eti ndo sababu Walimu hao hawajalipwa mafao yao, na ameagiza eti Afisa Utumishi huyo ahakikishe Wastaafu hao wanalipwa ndani ya Siku 3, hivi huu si ni Ujinga na Ulaghai wa wazi?

Sote tunafahamu Serikali ya Magufuli hailipi Wastaafu na Rais yuko busy kujenga Miradi anayoijua mwenyewe nyumbani Kwao Chato, Sasa Afisa Utumishi Hai ana nguvu gani kuwalipa Wastaafu?

Sifa zingine ni za Kijinga na Ulaghai!
 
Hyo taarifa hujaielewa vizur , umekuja kumuatack DC sababu upo oppressed Sana na mindset yako ipo totally negative , Mbunge feki how comes ? Thibitisha ..... Dc amefatilia majina ya hao walimu hayajafika hazina miaka miwili sasa , Nani yupo responsible kuyafikisha hazina ? Ametoa sku tatu utumishi wapeleke hayo majina hazina ,kama ofisi ya mkuu wa wilaya itafanya sehemu yake ili wapate mafao Yao....Sabaya alishawahi kunipiga Kofi kipind tunasoma Ikizu sekondary mi nikiwa form one yeye form four ...ila siwez mchukia Kwa kiwango kama chako aiseee
 
Hyo taarifa hujaielewa vizur , umekuja kumuatack DC sababu upo oppressed Sana na mindset yako ipo totally negative , Mbunge feki how comes ? Thibitisha ..... Dc amefatilia majina ya hao walimu hayajafika hazina miaka miwili sasa , Nani yupo responsible kuyafikisha hazina ? Ametoa sku tatu utumishi wapeleke hayo majina hazina ,kama ofisi ya mkuu wa wilaya itafanya sehemu yake ili wapate mafao Yao....Sabaya alishawahi kunipiga Kofi kipind tunasoma Ikizu sekondary mi nikiwa form one yeye form four ...ila siwez mchukia Kwa kiwango kama chako aiseee
Kumbe jamaa lilikuwa libabe kuanzia siku nyingi?mbowe hana hamu nalo asee
 
Back
Top Bottom