Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Tulipokuwa sekondari, kulikuwa na shamba la migomba. Basi tulitakiwa kuilimia migomba hiyo ili istawi na msimamizi wa kazi hiyo alikuwa ni mwalimu wetu wa kilimo ambaye alikuwa akiogopeka kama simba kutokana na ukali wake na kucharaza fimbo pale mwanafunzi anapomuudhi!.
Basi tukawa tunaenda shambani, mwalimu akiwepo shambani tunalima kweli kweli!, akiondoka tu; mtu mmoja anapanda sehemu ya juu ambayo anaweza kumuona akirudi. Basi sisi wengine wote tuna kaa chini tunajipumzikia. Yule mchunguliaji akimuona anarudi haraka tunainuka na kuanza kulima kwa kasi na mwalimu akifika anatukuta tupo bize tunalima hata muda wa mazungumzo hatuna ila kinachoshangaza tupo pale pale alipotuacha tunalima!
Baadae mwalimu akastuka kwamba kutakuwa kuna tatizo mahali kwa jinsi anavyowasimamia wanafunzi wake. Akaamua kubadilika. Akawa kwanza anawapatia wanafunzi ndizi wanakula na kupunguza njaa na kuhisi kua ndizi zile na shamba ni lao, kisha ndio anawaambia "Jamani ehh! ndizi hizo ni za kulimia, hebu nendeni shambani!" basi utakuta kila mmoja na jembe lake begani anaelekea shambani bila kusukumwa na mwalimu wala mtu yeyote analima, utamkuta anarudisha udongo kwenye shina la ndizi na kung'olea majani badala ya kuyafukia hata kama hakuna anayemuona, na akitoka hapo roho safiiiii. mara Siku mbili shamba lote li safi kabisa na migomba inapepea!.
Juzi nimekutana na mwalimu, ameshastaafu tayari wakati tunapita kwenye shamba lile tukakuta ndizi bado zipo na zimetawi kweli, nikamkumbusha kisa kile. Alichosema ni kuwa "Kijana wangu, nilichojifunza ni kuwa unapoongoza watu unatakiwa uwajengee mazingira ya kukuheshimu na kukuamini lakini sio kukuogopa. Vinginevyo hauwezi kuwaona wale unaowaongoza katika sura zao halisi na hilo litakupa ugumu sana kufikia kile unacholenga. Laiti nisingebadilika wakati ule, ungekuta pengine watoto wale wangeendelea kulima hapa tu! mpaka ningestaafu na shamba lisingeisha pamoja na kuwa nilikuwa nawaona wako bize wakati wote wanalima na sasa kusingekuwa na ndizi ya kuvuna hapa!".