SoC03 Tukithubutu, tukafanya tutasonga mbele kwa nguvu ya kilimo

Stories of Change - 2023 Competition

Auntyg

New Member
Jun 8, 2023
2
4
Tunaposema Uwajibikaji ni kitendo Cha kutimiza majukumu Fulani husika Kwa maslahi binafsi au ya jamii husika. Kilimo ni uzalishaji wa mazao ya biashara na ya chakula. Kilimo ni sekta muhimu inayobeba dhana nyingi sana. kiuchumi, kitamaduni, hata jamii Kwa ujumla

Tunaposema kilimo ni mama tunamaanisha kilimo ni sekta inayotegemewa na sekta zingine kadhaaa zinazoleta faida kiuchumi nchini. Sasa Ili sekta zingine ziwe Imara inabidi hata kilimo kisimame imara

Kilimo hakita simama Imara Bila ya nguvu kazi ya vijana kuwa Imara Kwa kujituma na kutimiza majukumu yao juu ya kilimo na huweza kuwa Bustani ya mboga, zao la chakula, au biashara n.k.

Je ni sekta zipi zinazonufaika kupitia kilimo Bora na endelevu !? na Kwa namna gani?
Sekta zinazonufaika kupitia kilimo endelevu ni kama
 Afya ni hali ya Mtu kuwa kiakili na kimwili. Afya Bora hali ya mwili na akili kuwa sawa na Kinga ya mwili imara. Kupitia kilimo tunapata matunda na vyakula vya asili kama vile majimbi, ndizi, viazi n.k ambayo hujenga mwili ya Mtu.
Wauguzi hutoa Ushauri kutumia vyakula vya asili

IMG_20230715_233111.jpg

na

IMG_20230715_233727.jpg
Chanzo Cha picha (la Maison jahazi na Wikimedia common)

Kupitia lishe nzuri na virutubisho vya vyakula vitamin kadhaaa. Hugenja mwili na afya kuwa Bora hivo basi Kila Mtu mwenye utashi wa jambo hili mwenye nguvu ajitume kuboresha kilimo tupate matunda, mboga za majani, vyakula.

Serikali ihimize Kwa kaulimbiu iisemayo kilimo kwanza. Ili wahimize ulaji wa vyakula vya asili
IMG_20230715_235017.jpg

1. kilimo ndio chanzo Cha madawa ya asili mfano mwarobaini, alovera, n.k
Dawa za asili pia hutumika kulinda Kinga za mwili Kwa binadamu. Watu hupanda mti wa alovera n.k kwaiyo tukumbuke KUTHUBUTU juu la swala ya kilimo. Katika sekta ya afya. Afya bora ni Mali

Viwanda ni sehemu ya shughuli za uzalishaji Kwa kubadilisha (malighafi) na kuwa bidhaa Kwa msaada wa mashine. Nchini Tanzania tunaviwanda mfano mwatex, meTl, sayona n.k
Viwanda vingi vinategemea. Malighafi kutoka kwenye mashamba.

Serikali ijuwe kuwa kilimo Bora ndio maendeleo ya viwanda ambayo Hutusaidia kukuza uchumi wa nchi nakumbuka kaulimbiu nzuri isemayo. Tanzania ya viwanda.

Viwanda ndio maendeleo chanya ya nchi mfano malighafi hubadilishwa na kuwa bidhaa. Mfano zao ya pamba.

IMG_20230716_001651.jpg

Picha kutoka Kwa (single news mara region)

zaoao la pamba (malighafi) inayosaidia katika uzalishaji wa nguo za cotton. Mfano ni mwatex
Kuwajibika katika kilimo ndio Chachu ya maendeleo kwa wakulima, viwanda na biashara kukua. Kilimo Bora huleta malighafi Bora Kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zenye ubora stahiki Kwa jamii. Pia tuna zao la mkonge ambayo ni malighafi pia kwajili ya uzalishaji wa Katani.
IMG_20230716_002359.jpg

Picha kutoka (muungwana blog)
Hivyo serikali itie mkazo katika mazao ya biashara na utunzaji wa mazao hayo kwani huleta maendeleo ya kiuchumi.

Biashara: ni shughuli za kiuchumi zinazojumuisha uzungushaji wa bidhaa Kwa malipo Kwa malipo ya kifedha. Kupitia biashara kilimo kinachangia kupata bidhaa za Moja Kwa Moja kutoka mashambani Kwa kuuza. Mfano ni viungo kutoka Moja Kwa Moja kwenye mashamba Bila ya kupitia kiwandani na ndio chanzo cha ujasiriamali. Mfano nyanya, hoho, ndizi, n.k, kilimo husababisha kupunguza utegemezi wa kiuchumi hasa Kwa vijana wanao jituma au juhudi katika. Ajira binafsi ya kilimo mfano genge la mboga mboga, matunda n.k.
IMG_20230716_102933.jpg
Picha kutoka (Muungwana blog.)
Pia Kuna mazao ya kuchakula ambayo watu huuza katika maeneo yasiyo patikana Kwa wingi
Mfano mahindi, maharagwe, Mchele, ngano n.k kama picha inavo jieleza hapa
IMG_20230716_103611.jpg

Picha kutoka. EMTEE (ems) Twitter .
Tunaona ni namna gani kilimo pia ni chanzo Cha biashara za Nafaka kwani sio sehem zote ardhi kila zao linakubali. Hivo kila anaejituma ndie ananufaika katika kilimo

Chakula ni kirutubisho muhimu ambacho wanyama hapata Kwajili kupata nguvu mwilini. Lishe Bora, na afya
Kilimo ndio chanzo cha chakula mfano kupitia Bustani za mboga, au matunda ni vyakula tosha Kwa jili ya watu wale wapate nguvu na kufanya shughuli zingine. Tukumbuke hatuwezi ishi Bila kula chakula Bora na safi na Salama. Kitu kizuri zaidi vyakula vya asili ndio kwenye virutubisho mwili. Mfano wali, ndizi, majimbi, viazi.
IMG_20230716_105529.jpg

Picha ni kutoka Facebook chagga people

Picha inaonesha chakula aina ya ndizi nyama. Nikimaanisha ndizi ni zao kutoka shambani na ndizi Ina virutubisho mwilini

Utamaduni ni mfumo wa maisha ya watu wanavyokishi katika mazingira halisi . Kiuchumi, kisiasa, kijamii n.k
Kilimo pia ni tamaduni za makabila mbali mbali ambayo wamejikita asilimia 94.5% katika kilimo
Wachaga, waziguwa nk. Pia Tanzania kilimo ni uhalisia wetu tangu Enzi za. Mwalimu Nyerere: kipindi Cha ujamaa.

Serikali ihimize upya ama mkazo juu ya utamaduni wa kilimo kwani pia ni utii wa itikadi zilizo anzishwa na wazee wetu tokea kipindi Cha ujamaa na uhuru Kilimo ni utamaduni sio tu Tanzania asilimia kubwa barani. Africa.

Uoto usio wa asili.mfano miti tukumbuke kilimo pia sio katika mazao Bali hata miti. Na miti hiyo hiyo ndio chanzo Cha maji, hewa ya Oxygeni na ni makaza ya baadhi ya viumbe hai.

Kilimo Cha miti Hutusaidia kupata mbao, vivutio Kwa watalii hasa misitu, utengenezaji wa fanicha, na karatasi kutoka kwenye mbao. Watu wanajisahau katika kauli mbiu isemayo Kata mti, panda mti. Hii sote ni kuhakiki uoto upo nchini na maji kuwepo. Serikali ihimize katika upandaji miti ambapo faida ya miti pia tunapata Kuni, mkaa n.k.

IMG_20230716_112533.jpg

Picha kutoka (foundation for Environmental protection) FEP Twitter

Picha inaonesha Mtu anapanda mti pia ni kilimo Cha upandaji miti kutengeneza misitu na kujilinda dhidi ya ukame. Pia tunasema uoto wa asili hata usio wa asili ni chanzo Cha maji. Maji tunapata kutoka Kwa baadhi ya miti hata migomba kupitia mizizi Kwa asili ya Mti husika inasadikika kuwa maeneo yenye miti mingi, migomba huwa na vyanzo vya maji hasa mito, maporomoko n.k. Umuhimu wa kilimo Cha miti pia migomba ni maji kwani maji wamebeba asilimia kubwa ya maisha ya binadamu kwani maji ni uhai.

Yaani hutumika katika sehemu nyingi mfano .kunywa Ili kuongeza wingi wa damu na maji mwilini, kufua nguo n.k, kupikia, usafi Kwa ujumla. Maji hayo hayo ndio inasaidia umwagiliaji wa mimea Ili ikuwe na iwe Bora pia
Hivo basi. Kilimo ni mama Kama watu wasemavyo maji ni uhai.

 Nini tuzingatie katika kilimo?
1. Mazingira sadifu Kwa ajili ya kilimo. Eneo la shamba lisiwe karibu sanaa na Makazi ya watu hasa mazao ya biashara
2. Utumiaji wa samadi au mbolea za asili na pembejeo za kilimo Ili kupata mazao Bora
3. Umwagiliaji hasa mazao ya chakula katika shamba dogo mfano. Bustani
4. Kulima mazao tofauti tofauti Ili Kutunza rutuba ya udongo
5. Kuzingatia kipindi husika la zao Fulani kutoka kana na hali ya hewa

Nini kifanyike Ili tuwe na kilimo endelevu chenye ubora!
Falsafa yangu ni kwamba serikali ndio yenye uthubutu mkubwa kuhimiza kilimo Bora katika nafaka na mazao ya biashara. Aidha Mtu binafsi au jumuiya. Ili uongozi wa viwanda vinunue malighafi kutoka katika wakulima wa mazao haya. Ili kuwa na faida pande zote mbili.

Pia itafanya watu wawajibike katika kilimo Ili kukuza biashara zao za Nafaka, malighafi kama pamba na matunda na vyakula vingine.

IMG_20230716_114353.jpg

Pichani ni kutoka (kisangilo agro chemical)

Faida za kilimo
Kilimo ni chanzo Cha malighafi
Kilimo ndio ujasiriamali pia
Kilimo ni sekta au chanzo Cha biashara kubwa
Kilimo ni ajira binafsi
Kilimo hutupatia chakula
Kilimo ni mama Kwa sekta mbali mbali

Hitimisho
Kilimo kweli ni mama wa sekta kadhaa katika maendeleo yote ya kijamii. Kila mtu awe na falsafa chanya juu ya kilimo. Huweza kumkomboa Mtu kiuchumi . Hasa tu Kwa yule anaewajibika bila kukosoa ama kukiuka sheria za nchi.

"Tukithubutu, tukafanya daima tutasongambele Kwa nguvu  ya kilimo Bora na endelevu"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom