Inaendelea.....
Mwanzoni mwa mwaka wa 2015 mahusiano kati ya Mzee wangu na Mama angu hayakuwa mazuri walikua wanarumbana sana mpk Mama akawa anatwambia kua ataondoka.Na kweli Mwez wa Tatu aliondoka bila kumtaarifu Mzee.
Mama angu alikua yupo kwenye kikundi cha vikoba bahat nzur alikua ndo mtunza hazina wao.sasa siku wanakorofishana na Mzee hii pia ilikua ni sababu, mzee alikua hataki kabisa Mama awe kwenye kikundi.Na siku Mama ana plan kusepa alitushirikisha Wanae ila akatwambia tusimwambie Mzee.Alisepa na hela ya wanakikundi m 2.8 pamoja na hela ya Ticha mmoja hivi alikua anafundisha shule moja na Mzee sh 400k.
Siku anaondoka alituita wanae tuliopo akatupatia kila mtu 50k na 300k kwa ajili ya matumizi ya home ila alitusihi sana tusije tukatoe no ya simu yake kwa watu ( hasa wanakikundi ) maana alibadili no ya simu.Hakubeba Nguo zake aliondoka na mkoba wake tu, me binafsi sikutaka kujua ni wapi anaenda ila nilikua na muhurumia sana.Baada ya yeye kuondoka na Kutokupatikana kwenye simu Wanakikundi walitaka kuzimia,Walienda Police wakachukua RB ya kumkamata ambapo mpaka Leo hawajawi kumkamata.Ila pesa alilipa Mzee ila Mzee alilaani sana hicho kitendo akaapa mbe yetu kuwa Mama ndo basi tena (



lakini leo hii wapo pamoja tena ).
Nyumbani nilibaki mimi wadogo zangu wa tatu na bro wangu ( mtoto wa Bamkubwa lakin yeye ni tofauti na yule wa mwanzo.Huyu alikua home kuishi baada kumaliza chuo wa walimu ko alikua anasubiria Ajira ambayo alipata mwezi wa Tano 2015 kama nitakua sahihi ).Bro wangu kabisa yeye alikua chuo pamoja sister angu.
Mwezi wa Tano Sister angu alirud home baada ya kumaliza Chuo Ualimu walipishana na huyo bro wangu ( mtoto wa bamkubwa ) yaani huyu anatoka huyu anaingia.Mimi wakati huo nime lisiti mtihani wa Form four.Nilikua nasoma Tuition jioni huku asubui nakuwa kwenye harakati zangu.
Kipindi cha kampeni za Uchaguzi kuna tukio nililifanya...
Me binafsi na Familia yangu tupo Chadema sasa kipindi hicho cha Kampeni harakat nilipunguza hii ni kutokana kulisit Pepa.Kuna siku moja Mzee alikuja Home na mgombea udiwani wa Chadema kutuomba kura.Tuliokuwa tunasifa za kupiga kura nilikua mimi na Sister.Sasa baada ya Huyo mgombea udiwani kuondoka aliniachia Picha ya Lowasa kubwa zile za kubandika kwenye mabango.kwa vile nyumba yeti ilikua karibu na barabara nikaamua niibandike kwenye ukuta nyuma ya Nyumba.Sasa hapo tulipokuwa tunaishi tulikua tunaishi na jamaa mmoja hivi alikua amepanga kagheto kake yaan alikua ni jirani yetu.
Huyo jamaa alikua ni mwendesha bajaji za Mizigo alafu ana ubaunsa fulani hivi kingine ni mwana Ccm damu damu.Siku ya tukio nilibandika picha ya Lowasa vizur tu kwenye ukuta wa nyumba yetu nikaondoka kwenda Kigera kwenye kampeni za Mbunge.Nilivyorudi nakuta picha ya Lowasa imechanwa na kutolewa pale ukutani alafu kuna picha ya Magufuli ( Hapa kazi tu ).nilipandwa na hasira kishenzi nikaulizia nani kafanya vile watoto wakanambie ni yule dereva bajaj ndo kafanya vile.nilimfuata gheto lake hakuepo kwa muda huo ko nikamsubir mpk usiku kwenye saa mbili hivi alivyokuja.Nilimuuliza kiupole tu " mbona umechana picha yangu " akanijibu kunya nikamuacha nikaenda nikachana picha Jiwe na mimi.Kesho yake asubui alivyokuta picha imechanika akamaindi sana.Alinifuata mpk ndani akanivuta mpk nje ( jamaa alikua ana ubaunsa na me nilikua kimbaumbau



) tulivyofika njee ananiuliza kwanini nimechana picha, nikamwambia kidharau kwani ajaona pakueka hiyo picha mpk aweke kwenye ukuta wetu.Akaanza kuiponda nyumba na mawe akidai lazima anishikishe adabu me na Ukoo wangu.Alimtukana Mzee mpk Mama ambao hawa usiki na Sister angu alipigwa kofi alivyo hoji tatizo.Sister alikua anafua ko nilichukua ndo iliyokua na maji yalio suuza nguo nika ya mwaga kisha nikampiga nayo kichwani huyo fala.
Na ilitua vizuri pembeni mwa kichwa chake mpk alianguka chini, aliinuka na kuanza kunifukuza nilikimbila ndani chumbani kwangu nikachukua Nondo ( zile za kunyooshea Nondo zinaitwa bender ) alivyoona ivo akaanza kukimbia lakin alikosea kuanguka, nilimpiga nayo mgongoni na shingon mpk nikaona mtu ametulia tiiii....damu ndo zina mtoka sikioni.Nilivyoona hivo nilikimbilia Iringo kwa bibi yangu nikijua kuwa nimeua.Simu, ndala vyote niliacha home.
Mzee alijulishwa hilo tukio ko aliwai home kuona nini kinaendelea.Jamaa alienda police lakin Mzee alimazana nao na jamaa akalipwa fidia ( 170k ) hata siku naambiwa kuwa mambo yameisha nilkua siamini kama ni kweli.Tokea hapo huyo dereva bajaji alikua ananiogopa kisenge yaani nilkua nikikutana nae hajiamini ila me pia nilikua na taadhari nae mpk siku anahama pale mtaani.
Maisha yalisonga na Kura nilipiga na Mtihani nikafanya fresh majibu yalikuja sio mabaya sana
Tutaendelea bado safari ni ndefu...