Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Inaendelea....

Dawa tulizokua tunauza ni zile za asili kama Nguvu za kiume, Kichocho, Amiba,Kisonono na nduguye Kaswende na mjomba wao U.T.I, dawa kuacha pombe,Ngiri,Mchango ( uzazi kwa kina Mama) na nyingine nyingi tu, zilizokua na bei kubwa ni dawa za uzazi na Vidonda vya Tumbo.

Kuna baadhi ya dawa hatukua nazo wakati huo ila zilikuepo kwenye karatasi la orodha ya madawa.

Dokta alitusihi sana tusiuze dawa ambayo haipo yaani kama dawa amna na mteja anaitaka tumwambie kuwa imeisha.

Dawa ambazo hatukua nazo ni ya kuacha pombe ma Miguu kuwaka Moto ....basi kwenye kisiwa cha ILUGWA biashara ilikua nzur tuliuza sana tu.

Tuliingia kwenye kisiwa cha Kweru Mto mapema tu kwenye saa tano asubui.Hali ya Hewa ilikua nzuri pia.Tulifika tukaenda guest kama kawaida tukanywa chai na kuingia mzigoni.

Biashara ilikua mbaya siku hyo kila mtu anakwambia hana hela tulizunguka sana ingawa tuliuza lakin sio kwa kiwango kikubwa.Dawa iliyokua inahitajika sana sana ni ya kuacha Pombe alafu hatukua nayo, nyingine zilizokua zinauzika sana ni za magonjwa ya zinaa.

Madawa yalikua hayana madhara kwa mujibu wa dokta na kile cheti cha wizara ya Afya ( upande wa Tiba za asili ) kilithibitisha basi na sisi tukawa tunajua hivyo.

Kuna Mwenyekit wa sehemu hyo alituzingua sana mimi na huyo rafiki angu ( maana tulikua tunatembea pamoja tofauti na dokta ambae yeye alikua kivyake ).Mwenye kiti na watu wake walitushika mim ma rafiki wakatupeleka ofisi ya mtendaji kujibu shtuma ambazo tulikua hatuzijui.

Walidai tuwaonyeshe vibari vya kufanya biashara pale sisi tukawa kile cheti cha wizara.Walituzingua kidogo lakin baadae naona wali lainika wakaanza kuulizia yale madawa na jinsi yanavvyofanya kazi

Tuliwapa ka elimu tuliko karirishwa na boss dokta kisha Huyo mwenyekiti akaulizia dawa ya kuacha pombe aione.Yule Rafiki angu alisema imeisha ila me nilidakia nikasema ninayo huku namuangalia usoni rafiki ( alikua ni Muoga ).Alinuliza inatumikaje nikamwelezea kisha akauliza na bei nikamwambia ni 35k, alilia nipunguze nikamwambie anipe 25k akadai ananipa 20k....nilisema tu kwa vile ni wewe muheshimiwa lete tu kisha nikampa dawa na wengine walinunua za nguvu za kiume kisha wakaturuhusu tuondoke.

Mwenyekiti nilimpa dawa ya kisonono maana ya kuacha pombe hatukua nayo na jinsi alivyotupotezea muda wetu kutupeleka kwa mtendaji niliona atibu kisonono wakati akijua kuwa anatibu kuacha pombe.

Tulivyokua tunarud guest rafiki angu yeye alikua ananisifia " we jamaa ni hatari aisee..." ila nilimwambia dokta asijue na kingine nilimwambie tumekuja kutafuta hela ko awe mjanja.

Tulipokua tunakaribia na guest tuliyofikia tulikutana na Wadada wamekaa nje duka moja hivi tukawafuata tujaribu bahati yetu, tuliwapa zile karatasi za orodha ya madawa huku nikizipa promo dawa ( nilikua naongea utadhani Dokta Og kumshinda yule rafiki angu )

Mdada mmoja aliulizia dawa kuacha pombe inafanyaje kazi.....nikampa maelekezo kuwa ukichanganya kwenye chai au uji basi ukienda kuonja hata kilevi chochote lazima utapike ko pombe itakukinai na utajikuta automatic pombe umeicha ...Mmoja wa wale wadada alikua so interested na mimi ko alitaka nimpe hiyo dawa akamueke Baba yake nikampa dawa ya kutibu U.T.I ( Mungu anisamehe kwa kweli ) sikumchaji hela kubwa nilimwambia anipe 10k tu maana alikua amenunua dawa ya Uzazi na kweli alitoa hyo na kunipa kisha nikawaaga tukaondoka kwenda guest.

Rafiki angu alivyoona me nauza dawa sana ila kiujanja aliiga na yeye mbinu zangu maana jioni yake tuliuza uza kidogo.

Nilikua nafanya vile maana dokta mwenyewe ndo alituambia kuwa dawa hazina Madhara yoyote basi niliona sio dhambi kujiongeza.

Usiku huo nilimtafuta yule manzi wa kisiwa cha Ilugwa tuliongea mengi akidai kanimisi anataka show...tulifahamiana zaidi nitamuelezea tena huko mbele....

Kesho yake tuliamka asubui tukafanya ibada kama kawaida ilikua siku ya Jumamosi ( Sabato ) kazi tulikua hatufanyi ko siku tuliitumia kusafir kwenda Nansio Ukerewe.

Hali ya hewa siku ilikua mbaya upepo unavuma kwa kasi mawimbi ndo usiseme.Tulisubir bot ije kwa muda kidogo ilivyofika saa 1 na nusu ikawa imekuja tukapanda.

Kalikua ni ka bot kadogo tu hata sio kubwa ila ilikua ya abiria.Nilikua na ogopa kusafir siku hyo maana hali ya hewa ilikua mbya dokta yeye hata hawazi ( maana kazoea ndo safar zake mara nyingi ).nilipanda tu ilimradi nimepanda hofu ilikua kubwa na sehemu yuliyokua tunaenda ni mbali.

Boti ilianza safar kama kawaida me hapo ni kusali kimoyomoyo ( Nilimkumbuka Mungu nikidai anione huruma ) kadri bot ilivyokua inazidi kwenda ndo mawimbi nayo ndo yalizidi kuiyumbisha ile bot mpk tunafika sehemu hauoni visiwa wala milima ni maji tu pande zote.

Tumbo liliniuma kwa uoga maana boti ilikua inapigwa na wawimbi yale ya ubavuni mpk maji yakawa yanatulowanisha.

Rafiki angu yeye alikua bize ana chati na simu wakati huo dokta yeye anasoma zake biblia mara gazet mara kitabu cha roho ya unabii.

Nilitamani kumwambia rafiki angu aache kuchati ila nilishindwa hofu ilikua kubwa.Wimbi moja kubwa hatari liliipiga bot ikayumba sana mpk simu ya rafiki angu ilianguka ziwani, wamama walipiga uwiiiii tunakufa nikajua basi boti inazama mpk nilimwambia konda tukizama utaniokoa me sijui kuogolea.....konda alicheka tu akasema nisiwe na hofu chombo kipo imara.

Tulifika sehemu moja hivi ndo tunaona nga'mbo mara boti ikazima sasa acha ianze kuyumba yumba kwa nguvu mpk kila abiria tukawa tuna hofu kubwa mwenye kusali anasali kuna mdada mmoja alilia akijilaumu kwann alipanda ile boti.

Konda ilibidi aizamie ile injini aone ina shida gan tulikaa kama nusu saa boti ikitengenezwa ( nyavu za wavuvi ndo zilikua zimeishika injini ko ikazima ghafla...niliwalaan hao wavuvi japo nilikua hata siwajui )

Mungu ni mwema tatizo walilitatua na safar ikaanza tukafika ng'ambo salama.
Tukapanda teksi kuelekea Nansio ili twende Ukara.

Nitarejea tena.
 
Aisee very interesting...kama hii tabia umefanikiwa kuiacha basi umefanya kazi kubwa maana ilishakomaa
 
Back
Top Bottom