Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Daaaaah....uchawi mbaya sn nimejitahidi kupita kimya kimya nikashindwa nikasema ngoja nidondoshe hizo thanks (likes) tu ila bado kanafsi kakawa kananisuta nipunguze uchawi imenibidi tu niandike. Itoshe tu kusema mkuu umeshindikana
 
kwa sisi tuliokulia dar es salaam uswahilini, tandale, manzese, keko, mwananyama, mbagala, mabibo, nk nimeshuhudia matukio ila wewe ulikuwa kiboko mkuu
 
Inaendelea

Maisha yalikua yanasonga tu hivyo hivyo kibishi...Nadhani jamaa aliona hela zake zinazid kupotea akaamua kutokutunza humo ndan mwake..ilo lilikuwa pigo kwetu na hela nilivyokua nazitumia vbya hata ningejua niwekeze tu kwenye biashara.

Ka hali kakanza kuwa kagumu demu nae akawa anataka hela basi ikawa ni mwendo wa kusema uongo ili nihurumie.kuna siku nilimwambia demu kuwa saiv mishe zangu haziko poa ko hela ni ngumu kidogo alinuna wiki nzima anitafuti na mimi simtafuti ( nilianza kumuona ni kero kwenye maisha yangu )...mpk siku moja ndo akanitext kunipa hi na blah blah nyingi tu kuwa eti me ndo mwanaume wake wa moyoni wengine ni wa kupita

Wivu ulinipata kusikia hvyo kuwa siko mwenyew ila me ndo napendwa..nilisema haiwezekani lazima nimkomoe huyo Manz ili tukiachana nisiwe na majuto..nilikuwa nawaza nitamkomoaje huyo demu..niliona njia bora ni kumrekod wakti namgonga ili akija kunizingua na expose video mtandaoni..kuna siku alikuja ni mgonge sikumrekod nilishindwa kabisa kufanya hivyo sijui kwa sababu nilikua Nampenda sana.

Kuna siku moja nilikua church ( siku hyo tulisali kimtaa ) basi bna me kwa vile ni muimba kwaya ilinibid nikae sehemu ya waimbaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa washiriki ya nyimbo...siku hyo Lizzy alikua amependeza na kigauni chake ambacho nilimnunulia kidume mie...basi tulikua tuna chat akanitaka niende sehem alipo kuwa amekaa tukae wote ( alikua amekaa nyuma kabisa ) siku shindwa kukataa mbele yake..ko nilimdanganya teacher kuwa naenda chooni..teacher alinitaka niwai maana kwaya yetu ndo tulikua tunaimba huduma kuu..basi nilienda sehemu alipo manz angu tukakaa stor za hapa na pale...basi tuliita kuimba nikawai kuimba tulivyo maliza nikarud kukaa na manzi yangu.

Manzi ilikua iko fb ila sasa ilikua imesahau password yake..aliniomba nimsaidie..nilimshauri afungue account mpya tu aanze moja na kweli alikubali nikamfungulia mpya.

Usiku wake nikiwa home nimelala niliamua kuingia kwenye hyo account yake ya fb mpya..aisee Ila Wanawake wanapata wakati mgumu sana mitandaoni kutongozwa kama kote...niliingia nilikutana na text nyingi tu za wanaume just imagine mpk Mzee wangu alikua amemtumia text "hi mrembo " nilimchuna maana nilijua ndo zake hizo...ukiachana na text nyingine za kuomba namba,hello mrembo,cjui unaishi wapi mrembo na nyingine nyingi kuna text iliingia ilinistua sana.

Ilikua ni ya jamaa mmoja hivi tunasali ila yeye alikua ni mwanachuo ( udom ) alikua likizo..text ilikua inasema hivi " we lizy wewe mbn siku unanikwepa au vivulana vyako hvyo vinakudanganya "...niliamua kuwa lizy cku hyo niliamua kuchat nae nikijifanya mimi ndo lizy sasa.

Jamaa alitiririka mengi sana nilikua namuuliza maswali ya kumtega nae anatiririka tu bila kujua anae chat nae..nikimuuliza kama alisha sex nae kiujanja sana..alisema hivi " niwie radh bby siku ile ulivyokuja tukasex c unajua ckua nimejiandaa vizur ndo maana nilishindwa kukuridhisha kipenzi" ( hizi chatting mok leo bado zipo kwenye account ya lizzy )...nilijisikia vbya hasira na wivu vikaambatana yaani manzi yangu inaliwa na hilo lijamaa nilisema sikubali aisee.tuliendelea kuchatt nikaamua nimuombe hela huyo msela wa manz yangu....nilimuomba 50k akasema hana hapo alipo labda kesho yake, nikamwambia potezea tu.Aliniomba no ya simu ya M-PESA nikampa yangu, cjakaa sawa ikaingia text ya imethibitishwa umepokea 55k kutia kwa huyo fala...asubui ilifika nikawai kwa wakala na kweli nikatoa 50k huku nikisema ngoja nijipooze na hicho ki hela.

Ila nilisema nitakulaje hela ya mwanaume mwenzangu...wakat na waza hayo text iliingia ya bro wangu ( yule mtoto wa bamkubwa tulie kuwa tunaiba nae ) akitaka nimpelekee kadeti town anipe hela.

Hizo Kadeti zilikua za huyo hyo mtoto wa mwenye nyumba..tulivyoona hela kahamisha tukaamua tuchukue nguo tuwe tunauza nyingine nazimodoa navaa tena ananiona nimevaa.Nitaelelezea baadae ngoja niendele na huyu manzi kwanza.

Kweli nichukua Kadeti ( zilikua suruali mbili ) nikachukua na zile 50k za yule fala nikaingia town.Nilifika kazin kwa huyo bro akaona mzingo kisha akanipa 20k na kunitaka nimtafutie mzigo mwingine.

Niliamua niende dukani nikamnunuliee nguo Manzi yangu kwa ile ile hela ya huyo fala wake...nilinunua kigauni cha 35k chenj iliyobaki nilimpelekea huyo manz angu pamoja na hilo gauni.demu alifurah akijua kuwa nimempa zawadi kumbe alkua hajui ni pesa ya boy wake ndio imefanya hayo mambo.

Kesho ilifika siku nilikua natoka tizi la kukimbia kwa ajili ya kutafuta pumzi ya kuimba.nilifija kuchukua simu nakuta text ya huyo boy wa manzi angu ilikua inasema hivi "yaani wewe Holly holm ndo wakunifanyia hivi aisee rudisha hyo hela au umpe muhusika yaani Church minister mzima unakua tapeli" nilimjibu tu kawaida kuwa hela simpi ng'o na cha kunifanya hana.

Jamaa kumbe ile no niliyompa kutuma ile hela ilikua whatsapp na picha yangu juu kumbe alisave na kuniona mimi badalaya ya demu wake.Alinitishia kuwa atanifanyia kitu kibaya me nilimwambua nakisubiri hicho kitu.Wakat huo hata manz ajui hyo inshu sikuona ni vyema kumwambia.

Nitarud nielezee jinsi nilivyo mfanya huyo boy wa manzi angu....

kikoozi
Mzee endeleeaa
 
Inaendelea

Basi baada ya huyo boy wa manz angu kuwa ananitumia text za vitisho kuwa nirudishe zile heka zake na kunambia niachane na Manzi ake...nilikua na mpuuza lkn ilifika wakati nikaona huyu mazoea yamezidi sasa...aliniwapa washkaj zake no yangu na wao wakaanza kunitukana kweli matusi mabaya eti kuwa wakinishika watani fira....niliona sasa wamevuka mipaka yao...

Nilimuita huyo demu siku hyo akaja nikamgonga na kumpiga picha za uchi, alafu nikamwelezea huyo demu kuwa unatoka na fulani akaruka vby mno nikamuonesha mpk zile text nilizokua na chat nae..akaamua kusema kuwa huyo jamaa ni kweli alimtongoza lkn alimrusha na huwa ana msumbua lkn siku mwambia kuhusu huyo jamaa kunitukana na washkaji zake...nilimuacha tu akasepa zake hakujua lililokua moyoni mwangu.

Nilipanga kuwa fanyia tukio hao jamaa mpk wakiwa wananiona wawe wanapita mbali...of course me vitu vyangu nilikua nafanya kwa uhakika..kuna msela wangu mmoja ( yule wa utotoni ambae tulikua tunaiba nae usiku )...yeye bado alikua anakaa Iringo ( mpaka saiz bado yupo Iringo )...niliamua kumtafuta kwa ajili ya huo mpango...na kweli jamaa alinambia ni mimi tu nikiwa tayar nimwambie.

Huyo boy wa msela kuna siku alini text tena nilimjibu majibu ya dharau akajaa..akasema atanikomesha...nilimwambia tu your welcome.Nilimpanga siku hyo demu nikamwambia kesho jumamosi baada ya ibada twende Iringo, alikubali bila kupinga ( maana alikua sana ananisikilizia ).

Kesho yake tupo kwenye ibada nikamuona huyo boy kakaa benchi za nyuma ( me nilikua nakaa bench za mbele kabisa za Waimbaji )...nilimuona nikajisemea tu moyoni kuwa leo unalo labda usiingiee kwenye kumi na nane zangu...nilmtext tukachat nae kidogo..nilikua namwambia kuwa leo jioni nitakua Iringo na demu wako...nilimuona ananiangalia vby ( na huku tupo kanisani )..akaniuliza iringo sehem gani nikamwambia kastamu akasema ok...

Kiukweli nilikua nimeplan siku hyo kumpiga huyo jamaa atakama ni kumuua ni muue tu.Alafu alivyokua mjinga alikua ananidharau kwa vile yeye yupo chuo me hata veta tu siijui.alijiamin kupitiliza.Nilimpanga yule muhuni wangu kuwa nitakuja leo huko mitaa yao na Manzi angu.

Midaa ilifika ya jioni ( saa 10 ) demu akajaa tukapanda boda mpk iringo.Tulivyofika tukaenda kwao na huyo muhuni wangu ( huyo Muhun wangu alikua kaachiwa Mji baada ya Wazaz wake kufariki ko mji ni wake mpk saivi ).

Nilivyofika nilimwambia Manzi ampigie huyo msela wake aje iringo.alimpigia tena akiwa kamuweka loudspeaker tunamsikia...jamaa alikua anasema huyo fala wako yuko wapi ( yaani mimi ).

Kufupisha habari ni kuwa huyo jamaa alijichanganya kuja yeye na wasela wake wawili na kapikiki kao..nilikua na hasira cku hyo ( sio za demu ila ni za kutukanwa na wale mafala )..Walifika nilivyoona waona hao wasela wake wawili mpk nilicheka, nilijisemea kuwa " huyu jamaa ananileteaje mabishoo wanipigie " alafu walivyowajinga sijui walikua wanajiamin vpi walikuja mpk maeneo ya ziwani ( kuna milima ).nilijitokeza tu huku zuna nimeiweka kiunoni ( Zuna ya muhuni wangu ), mpaka sehemu waliyokua wamesimama na Manz yao ( maana manzi alienda kuwapokea )

Nilivyofika walipo nikawapa hi wakajibu...alafu nikawaambia mlikua mnasemaje sasa.Me hua na roho mbaya nikichukia, nilimpiga ngumi ya pua huyo jamaa na alivyokuwa ni white damu zilimuahi kutoka, wale wengine walivyoona hivyo wakajamu wanataka kunipiga nikachomoa Zuna niliwapiga bapa mpk mmoja akakimbia.nilimrudia yule jamaa lengo langu nilikua ni mtoe roho ( sema yule muhuni ndo alinishika nisimuue )..tulimbeba mzima mzima kwenda nae mlimani yule muhuni amfire ( sory kwa lugha mbovu ) maana tulikubaliana hvyo amfire.Jamaa alilia siku hyo akiita watu wamsaidie lkn watu ndo kwanza hawana habar nae na wasela wake cjui hata walipotelea wapi.Kuna mvuvi mmoja nae alikua ana sapoti tumpige huyo jamaa ( chanzo chenyewe alikua hajui yeye anasapoti tu ).

Tulimpandisha mlimani jamaa analia tu simu,hela zake muhuni akachukua..Muhuni haku mfira ila tulimpa onyo na kumtaka atupatie 200k..alidai hana tukashuka nae mpk ghetto kwa muhuni tukaandikishiana kuwa tumemfumania inabidi atulipe hyo hela siku flani na mashahid walipatikana pale wa uongo na kweli.Jamaa tulimuachia kama saa moja usiku kwa makubaliano ya kupewa hizo hela baada ya wiki moja...ila nilimpiga siku hyo, tokea hapo alikua ananiogopa vby mno..nilimpiga mkwara mzito kuwa siogopi cha nani kama anataka kwenda police aende atanikuta tu niko kanisani.

Manzi nae aliniogopa alikua hajawi kuona hasira zangu ila me nilikua sina shida nae maana nilikua namtafutia mbadala wake kimya kimya.

Hizo 200k tuliambulia kupewa 60k tu ko nikampa muhuni wangu 20k nikabak na 40k nikafnyia yangu...hivyo ndo nilivyomfanyia huyo msela alijiona kuwa kayapatia maisha mbele yangu.

Nikirudi nitaendelea kuwaelezea tena harakat zangu za wizi mpaka Mzee wangu kuwekwa ndani na Mkuu wa Wilaya, Me kukamatwa kwa kosa la wizi, Mahusiano yangu na yule demu wa kisiwani, kutapeli na vingine vingi mpk kufika hapa nilipo

story bado ni ndefu ko kuna matukio mengi mengine niliyafanya ila cjaandika maana nilisahau kuyaweka.Binafsi nayaleta nikiwa nimeyapanga kwa Miaka.

nitarudi tena.
Nilitaka kupita kimya kimya bila comment, hii episode imefanya nicheke sana maana hiyo ngumi ya pua ni shida. Umenikumbusha mbali sana ha ha..

Ila jamaa ulikua na matukio sio mchezo,,eti mnasemaje sasa,, hajakaa sawa ngumi ya pua.. anyway story nzuri sana.
 
Inaendelea

Samahani sana kwa kuchelewa kupost...tanesco sio watu.

Tuendeleee....

Baada ya kuwa tunakosa hela kwa yule jamaa pindi tukiingia kuzisaka ilibidi tuhamie kwenye nguo zake, jamaa alikua na nguo nyingi alafu mpya mpya vi kadeti,staff jeans na vishat vizur vizur...

Nilikua nikiviiba tu naenda kuviuza chapu kwa wadau wangu.bro wangu ( mtoto wa bamkubwa ) ndo alikua muda mwingine ananitafutia wateja.

Kuna fundi fulani hivi alitaka kunidhurumu hela ya nguo nilizomuuzia nilimuashia moto kazini kwake hatokuja kusahau..

Kuna siku moja Jamaa angu mmoja hivi Baba ake alikua ataka kuoa ( kwa sherehe ya harusi ).sasa huyo jamaa angu Baba ake alimpa tenda kuwa atafute vijana Watatu kwa ajili ya kulinda Eneo ambalo sherehe ilitakiwa kufanyika ( Ukumbi mmoja unaitwa Eva Green upo karibia na Tembo beach )...tulipatikana mimi na washkaj zangu wawili mmoja ni yule rafiki angu tuliyekuwa tunauza nae dawa visiwani.

Jumla tulikua tunao linda ni wanne, yule jamaa ambae baba ndo mwenye shughuli na sisi watatu.

Huyo mzee alituahidi kutulipa 30k kila mtu baada ya sherehe kuisha..tuliikubali hyo tenda chapu na tulitakiwa tulinde kwa siku nne, ilikua ni pamoja na kufanya usafi kwenye huo ukumbi.

Sehemu niliyokua naishi mimi ni mbali na hao washkaji zangu ko ilikua ikifika saa nne usiku walikua wananipitia home na gari ( Bwana harusi ndo alikua ni dereva ).

Siku ya jumamosi usikusasa nyumban kwa Bwana harusi kulikua na Muziki ( mkesha japokua ni wasabato ila walifanya kibishi ).siku hyo hawakuja kunipitia home ilibid mimi ndo niwafuate huko kwenye mkesha wa harusi.

Yule Manzi angu nae ni jirani na huyo mshkaji wangu ( baba ake anae oa ) basi nilivyofika kwenye mkesha nilimuona manz angu kakaa nje kwao nikamuita kumuomba papa akanibania eti yupo mwezini alitaka nimshike ni hakikishe me nikapotezea.

Tulikaa kwenye mkesha mpaka kwenye saa sita hivi tukaondoka kuelekea Lindoni.kwa vile tulikua wengi tuliamua kutembea miguu.Wale washkaji wangu ni waoga ila wana mikwara hatari usiombe waanzishe ugomvi wewe upo utapigana pekee yako.

Tulipitia ile barabara ya kwa Mkuu wa Mkoa..tulipofika hapo sasa kwa mkuu wa mkoa tulisimamishwa na fenda imejaa mapolisi walio kuwa Doria...walituuliza " Mnatoka wapi na mna kwenda wapi"...wale jamaa zangu ni waoga ( japokua me nae muoga lkn hao ni balaa )..nilimjibu yule afande alie uliza swali kuwa "Tunatoka road na kwenda Tembo"..walisema kufanya nini nikawaambia kuwa sisi tunalinda ukumbi walitwambia tu "Usiku huu kuweni makini" kisha wakasepa.

Jirani na hapo kwa mkuu wa mkoa kuna Ukumbi mmoja unaitwa Musoma club.Siku hyo kulikua na harusi hapo.Maafande walivyo sepa zao tukaamua kuingia kwanza hapo kwenye harusi kuiba vinywaji ( me nilkua na begi alafu nilikua nimevaa kihuni kishenzi ).tukifika kwenye harusi tulikuta ndo inaisha vinywaji havikua vingi sana tukatoka.tukaamua kuitafuta harusi moja ilikua inasikika tu kwa mbali.Tuliifatilia mpaka kuipata, kumbe ilikua iko pale Ukumbi wa Dayosisi jirani na Tanesco.

Kuingia ilikua tabu maana mlinz aligoma tusiingie ndani mpk tumuonyeshe kadi.tulileta noma pale mlangoni mpk mlinzi akaturuhusu mwenyewe kuingia.Tulivyofika ndani sasa tulikuta napo harusi ndo inaelekea kuisha ila watu walikua wana serebuka na muziki alafu mezan kuna vinywaji tulianza kupita navyo tukiviweka kwenye begi langu...tamu zangu zilikuja mara baada kumuona Mama alikua anaweka vinywaji kwenye mkoba ( vinywaji vilikua vipo chini ko alikua amekaa na muda mwingi aliutumia kuangalia chini badala ya kuangalia mbele.

Mezani niliona simu nikasema hik lazima nichkue nisepe nayo bila rafiki zangu kujua.wakati yule mama anaendelea na zoezi lake la kuweka vinywaji kwenye mkoba wake..nilipitia ile simu ya yule Mama nikatoka nayo nje ya ukumbi spidi kama vile sio mimi.

Niliondoka eneo lile na kukimbia kuelekea Line Police...nilitoa betri kwenye ile simu ( tecno smart phone L6) pamoja na kutupa line zilikua kwenye simu.

Niliamua kuelekea Lindo kuwa subiri wale washkaj waje wanipe habari, walivyo kuja hata hawakujua kuwa me nimepiga tukio.

Kesho yake ilifika siku ya harusi tulienda kujiandaa kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji ( Maana wote tulikua ni waimbaji wa choir )...baadae sana ndo niliwaambia kuwa siku ile niliiba kisimu cha tecno nikawaonyesha.Walitaka niuze alafu tugawane hela wote. kuna fundi simu ndo nilimuuzia bei ya kutupa tu 70k nikawagawia 30k wale jamaa na mi nikabak na 40k ya bure bure.

Nitaendelea tena kesho.
 
Umenikumbusha tecno l6 kangu kalikua kanakaa na chaji balaa hadi siku 3-5 kinachaji tu
 
Nakufatilia sana wewe jamaa inabidi tukulete NJIA PANDA na Dokta Issac marlaw CLOUDS story yako itabamba ile mbaya
 
Wewe ulikuwa ni mwizi sugu bila shaka utakuwa unaendelea na wizi ila kimya kimya mngetembelea mitaa nilipokuwa naishi na hakika sasa hivi ungekuwa kuzimu una busu miguu ya shetani..
Hahhahahhaah,usijivune bro huenda ungefanywa mbaya tu vilevile
 
Inaendelea

Harakati za kuiba na Kusali ziliendelea kama kawaida...kuna kipindi nilichalala vibaya mno nikawa nawaza napataje pesa sasa...sikumbuki ilikua ni juma ngapi? ila ilikua ni September.....niliamua kwenda mitaa fulani hivi lbd nitakutana zari huko njiani lakini hakukua na zari la maana nililokutana nalo...niliudhika sana nikawa narud home, mara nikakutana na wale wanaonunua vyuma chakavu, walikua ni wababa wawili wako na baiskeli wana piga promo biashara yao "* tunanunua vyuma chakavu..tunanunua vyuma chakavu*"..basi nikawaita waje ( home kulikua kuna bomba flani hivi refu la chuma la yule yule Jamaa nae mwibia ).....niliwaambia nina mali kama vipi twendeni mkaione tupande bei....wakakubali tukaanza safari kwenda home, kufika nikawaonyesha mzigo ulikua tu hapo nje...

Hao wanunua vyuma waliliona ila wakasema kuwa hilo chuma ni refu sana na wao hawajatembea na msumeno wa kukatia ko labda waende kuchukua msumeno ndo warudi...ilikua mida ya saa saba kuelekea saa nane...niliwaza sasa hawa waje waende tena warudi c kushikwa nitakua nimeshikwa na jamaa kama akirudi ghafla...

Niliwaza nikakumbuka kuwa mle chumbani kwa yule jamaa huwa kuna machuma matatu yapo kwenye kabati la ukutani...nilisema yes hayo ndo nachukua moja nawapa hao wakuda.

Yalikua ni machuma yale ya kwenye Mashine za ku pampu maji ziwani....niliwaza hapa nitakua na 40k kuendelea...hilo chuma ni zito mtu mmoja hulibebi..

Niliwaambia wale wakuda wanisubir niwaletee mali, nikaangia chumban kwa jamaa na gunia ili nilibebe lakin lilinishinda..nikawaita madogo wanisaidie, yule ambae sio mwizi alkua ana shangaa ana leta usabato wake pale eti kuwa mnachokifanya sio kizur...nilimwambia tu hela ninazokupa unafikir hua zinatoka wapi?..ila alisema sio poa ninayo fanya, siku mjali nilimwambia beba mzigo.

Kwenye ile harakati ya kunyanyua lile chuma maana tulikua tumeshalitoa kabatini, lilituteleza tukiwa tumelinyanyua bahati mbaya likatua kwenye mguu wangu wa kulia. hayo maumivu yasikie tu kwa jirani, nilivumilia kiume tukalitoa hivyo hivyo kibishi mpaka nje kwa wale wakuda ( nawaita wakuda kwa sababu ni Wakuda kweli )... tulivyolifikisha wakaliangalia mmoja akacheka na kusema eti hili ni chuma DONGO ...( hivi kweli kuna chuma dongo )...nilishangaa kusika chuma * dongo* ndo chuma gani hilo.

Walisema hua hayana thamani yale na walivyoniua nguvu ni baada ya kulipima wakakuta ni kg 33 aisee kuna vitu vinafurahisha...niliwaambia kuwa hawako serious na kazi za watu yaani chuma tuna beba watu watatu tena kwa shida eti liwe kg 33.walitoa 6k kunipa eti ndo lina thamani ya bei hyo...niliwaangalia vbya wakati huo nasikilizia maumivu ya mguu, niliwaambia madogo tulibebe tulirudishe ndani...lakin hao wakuda waliniuliza " unataka sh ngap dogo tukupe "...niliwaambia 50k wakasema hilo chuma halina thamani lbda tukupe 20k...niliona hawa wakuda ni matapeli tu hawako serious tulilibeba chuma kurudisha ndani.

Wakuda wakaanza ku toa matusi eti nimewapotezea muda wao...tulivyo rudisha chuma ndani ilibidi niwarudie hao wakuda ili wanitukane vizur niwasikie.Nilikua nimekaa kwenye ngazi za mlangoni nasikiliza tu matusi yao...mdogo wangu wa kike alikua ndo anatoka shule muda huo ko alikuta hako ka mzozo.

Niliona wavuka mipaka sasa na matusi yao nilimwambia huyo dogo langu aingie chumban kwangu aniletee kilichopo chini ya Uvungu ( alikua anakijua nachokitaka )....alikuja na Panga ( lile lile ambalo mzee alitaka kumkata nalo Mama 2013 )..nililipokea nikawafuata hao wakuda japo na maumivu ya mguu lkn nilikua siyasikii sana.

Walivyoona hivyo walibaa na huku ni wakubwa kwangu walishindwa cha kufanya, niliwafuata nikiwa nime kunjia sura sicheki wala nini..mbona walilala mbele wakaacha baiskeli yao na kilo yao na ningewapiga bapa sema walikimbia.

Nilichukua baiskeli nikawatupia na ka kilo kao nikawaambia wasepe kabla sijawaua ( nilikua sitaki waendelee kubaki pale maana kama yule jamaa angetokea ingekuwa shida kwangu ).

Wakuda walisepa madogo wakabak wanacheka tu huku wakinambia "holy holm we ni nyokoo ".

Nilirudi chumban kwa yule jamaa hata nijipooze na ka kinywaji ( vilikua kwenye fridge yake ) nilichukua Alvaro mbili moja nikampa dogo langu wa kike na moja nikanywa, pia nilikuta vi Apple nikachukua kamoja ile namkatia dogo langu Kisu kilikua ni kikali kisenge kikapita na mimi kwenye kidole cha mkono wa kushoto, maumivu ya kidole na mguu yasikie tu....nilijiaulumu kwann nimefanya kile kitendo nilimuomba Mungu anisamehe tu.

Niliuguuza majeraha yangu tena nilichoma sindano ya tetenasi kabisa...mambo yalizidi kwenda na siku zangu zilikua zinahesabika kwa kweli.

Nitarudi tena kuendelea.
 
Back
Top Bottom