Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Inaendelea

Mwaka 2017 kiukweli ulikua ni mwaka wangu wa kushika hela tena bila kutoa jasho yaan nilikua ni kuingia nakuchukua kama zangu vile...

Nilinunua Godoro na kitanda nikatunza kwa mshikaji wangu mmoja hivi maana home nilihisi watakuja kuni stukia huo mpango wangu.

Jamaa naona alianza kuhisi kuwa kuna kitu hakiko sawa kwenye hela zake..siku moja usiku aliniita chumbani na kuanza kunielezea kuwa kuna vitu vyake vinapotea...roho ilianza kunidunda hofu juu ila sikutaka agundue hilo.

Alisema tu kuna vitu vyake vinapotea na ajui ni nani anachukua ila alikua ana muhisi jamaa ni jiran yetu.kuna siku alifua boksa zake akaanika nje c huyo muhuni akapita nayo alafu alivyo fala akaenda nayo location kupiga picha...sasa jamaa alimuona fb huyo msela kapiga picha kifua wazi ko boksa ikawa inaonekana ( ndo maana alikua anamtuhumu huyo msela kuwa ndo mwizi wake)

Siku hyo nilimsikiliza na ushauri nikatoa wa kinafki dhen nikasepa kulala.Nilimwambia dogo langu asiingie kuiba asubiri kwanza jamaa hofu imuishe..

Huyo Mtoto wa mwenye nyumba licha ya kuwa mkubwa kwetu ( Ana miaka 40+ ) ila jamaa ni muoga hatare yan hata panya alikua hawez kuua..afu kingine licha ya kuwa na pisi kali kali lakin alikua ana matatizo ya nguvu za kiume maansa kuna siku aliniomba ushaur atumie madawa gani, nikamuuzia yale madawa niliyokua nauza kule kisiwa ( kuna mengine nilimuibia dokta home kwake ).

Ko jamaa alikua ananikubali sana ila alikua anadharau sana..alitudharau sana kwasababu mzee alikua halipi kodi kwa wakati basi ataenda kuwaambia sisi ni nothing pale kwao.hicho kitu kiliniuma sana.sasa ndo nikaamua nimuibie kisawa sawa ili kumkomoa...lakin nilikuta zile hela za kwenye kapu hazipo kaziamisha.

Nilitafuta sana ni wapi alipozitunza lkn siku fanikiwa kuzipata..Mdogo wangu cjui alikua na madawa gani aisee siku aliinita na kunionesha kimfuko hivi kilikua chini ya sofa lake huyo jamaa.

Huo mfuko ulikua na hela nyingi ckujua ni shngap...nilitaka kuzibeba zote sema dogo alinizuia nikachukua 400k nikasepa zangu.kesho nilirud nikakuta hazipo hela cjui alizificha nilitafuta kila kona ckupata...nikaona ili nichukue tu Baritika zero kwenye fridge yake nikaonge demu.

Huyo manzi angu ( Yule wa mwanzoni tumuite Lizy maana alikua ana nguo yake imeandikwa Lizzy ndo me nilikua hivyo ) Manzi ilifaidi sana hela za wizi japokuwa hakuwa mwaminifu kwangu.

Kuna kipindi nilikua chumban humo nakosa hela kabisa yaan nilikua naambulia 5k mpk buku....nilikasirikia balaa nikawa najiuliza jamaa anatunza wap hela zake ama anaweka benki..Siku moja ilikua jumamosi sikwenda kanisani nilikuepo home tu nachek movie.Siku hyo jamaa nae hakwenda kazini maana alikua ni zamu yake Jumuia kufanyikia hapo kwao.ko waumini wa kanisani kwao walikuja wakafanya ibada pmj pale kwao.

Me nilikua nawachora tu dirishani jinsi wanavyo abudu..niliona wanatoa SADAKA kwenye kisonzo alafu wakamkabidhi yule jamaa walivyoondoka nilimuona jamaa amezibeba akaingia nazo chumbani..nilikua namchora nikajisemea tu Mungu anisamehe kwa tabia hyo.

Nili subiria jamaa akaondoka cjui alienda hyk ikawa nafasi yangu niliingia chumban kwake kasi ya ajabu mpk kwenye hilo li briefcase lake..nilifungua nikazikuta zile sadaka mule..Nilizichukua zote nikaacha tu kile kisonzo na kaunta book.

Kipindi hicho sina roho ya huruma kabisa tena nilikua nikiingia kwake nabeba kisu kabisa ili nikishikwa tu nijitete na kisu.Jamaa siku alinihisi kabisa kuwa mimi ndo mwizi.

Jamaa wasiwasi wake wa kupotelewa na hela vilimfanya akaamin kuwa kuna chuma ulete kwake.Siku moja alirudi na kajamaa flani hivi kalikua kamebeba begi...akaingia nae chumbani kwake, Mara jamaa akatoka na kutuita me na wadogo zangu.

Kumbe kale kajamaa kalikua ni kaganga kalituita akatwambia yukae chini tumsikilize aliyo tuitia

*Nitarudi tena *
 
nilifurahi sana kusikia hivo mpk nikawa natetemeka kwa furaha )

Daah nimechekaaaa hatari, nimetengeneza kaclip kichwani, namuona, Yule mbilikimo wa aki Na ukwa,
 
Nimecheka sana, maana wenyewe wanataka dawa we huna, unapiga sounds unauza zilizopo hapo nakupa kongolee.
Kuna kipindi jamaa niko kitengoni wamepiga sana nyagi badala ya Gordon gin,Valeur badala ya Remy Martin na mnaenda sawa tu.πŸ€£πŸ€—πŸ€£
Kuna maskini mkenya ndo alituumbua, akaja na mchupa wa Gordons kaagiza kwetu tukampa za uso nyagi akapiga makelele tukamtoa kwenye game akafie mbele
 
Alielewa hapa anieleweshe
 
Kantalamba sumbawanga hahah

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Huu ndo ukweli kuhusu Musoma niliishi huko kwa zaidi ya miaka 6 lakin sina ninacho kimiss hata kimoja ambacho kinanifanya nitamani kurudi kuishi huko, mwaka juzi nilikuja huko kusalimia baadh ya jamaa zangu ilikua nimepanga nikae siku mbili lakin nilikaa siku 1 tu nikasepa maana sipakubali tu **** ushamba ni mwng mno huko baadh ya marafik zangu wa miaka hiyo tukiwa bado wadogo, walikua na tabia ya kupora icecream za wanafunzi shulen na kukimbia nazo lakin sahiv ni waizi kamili na wamekaa gerezan sana tu kila mwaka anachezea miez 6 ndan miez 6 nje

Kwakweli huko ukiwa na familia yako inatakiwa uiweke chin ya uangalizi mkubwa laa sivyo wanaweza kuiga tabia za baadhi ya vijana wengi wa huko ambao wanaamini kuwa na makundi ya kihuni ndo ujanja
 
Inaendelea


Kama nilivyosema siku hyo huyo jamaa alikuja na huyo mtu ajiiatae Mganga..Tuliitwa mimi na wadogo zangu wawili pamoja na Jamaa mmoja muhuni muhuni nae walimuhisi ni mwizi.

Basi tuliingia chumbani kwa huyo jamaa tukakuta Mganga kashaanda mambo yake tayar kwa kazi iliyomleta.

Nahisi ilikua ni mind game ya huyo jamaa na huyo Mganga wake.niliuliza kuna nini kwani jama ndo akaanza kutiririka kwann tumeitwa pale me nilikataa sihusikii na wizi pamoja na wenzangu pia walikataa kata.nilikua na mwangalia dogo kama ana wasi wasi lakni alikua mweupe hata wasiwasi hana.

Baafmda ya kila mtu kukana kuwa hausiki na wizi Mganga alimuomba ruhusa huyo jamaa aanze uganguzi wake..πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚ ila kuna watu wana visa dunia hii acha mganga awashe kamshumaa kekundu na aliletewa sufuria la maji akawekapo vidawa fulan,na kidude fulan hivi kama sabuni pamoja na sindano rungu.niliwaza kuwa naumbuka siku ile ila nikakaza nilisema hata kama nashikwa ni fresh tu kwanza uzur sina urithi kwa Mzee sio mbaya nikikamatwa ( nilikumbuka ile kauli ya mzee wangu hapo nyuma ).

Mganga alisema tu " kama kuna mtu anajua kabisa hausiki na wizi achome hicho kipande na anawe mikono kwenye sufuria alafu aondoke "...niliogopa kiasi chake ila sikutaka nionekane kama na hofu...unajua kipindi cha nyuma bado nasoma kuna jamaa nilimuibia dictionary class alinihisi me ndo nimemuibia ko aliamua kunipiga mikwara mizito ya kijini jini ila ndo sikuogopa ( kisa chake nilisahau kukielezea )sasa hyo mganga nilimuona ni kama tu yule jamaa wa dictionary.

Alianza mdogo wangu ( sio mwizi ) kuchoma kile kidude kwa sindano Rungu aka fuata yule muhuni kisha dogo alafu me kidume ndo nikamalizia..wakati naondoka nilimwambia yule Jamaa kama nisipokuwa kitu utanilipa fidia ( nilikua nimemkazia sura utadhani me sio mwizi )

Usiku wake siku lala vizur kiukweli nilkua nasubiri tu matokeo ya ile dawa ya mganga ( tapeli tu ) nilikua najishika viungo vyangu nione kama kuna mabadiliko yoyote lakin sikuona, usingi cjui ulinipitia sangap

Asubui yake niliamka nikawai chumban kwa madogo nione kawaje na yeye lakin sikumkuta dogo niliogopa kuangalia chooni na bafuni hayupo nikawa najiuliza kaenda wapi tena?...kumbe dogo alikua anamlia target yule jamaa asepe ampige tukio ( mdogo wangu kunakipindi niliamini karogwa )....siku hyo ilipita fresh tu tuko vizur na siku iliyofuata pia nikasema kumbe jamaa wamempiga hela za bure na Mganga wake.

Dogo langu alikua anaiba mpk to much aisee...sio tu kwa huyo msela mpk kwa baadhi ya majirani alikua anawacheza...nilimkanya kama Kaka aache kupiga matukio kwa watu mwishoe azoee sikupenda kwa kweli dogo apite njia zangu..

Bahat nzur aliacha kuiba kwa majirani ila akawa anampiga tu huyo jamaa...


Me kipindi hicho mapenzi yangu na Lizzy yameshika kasi kinoma kumuhudimia kama kote..ila Mapenzi ni mapenzi tu Lizy alianza kuniletea mambo ya kifala sana alikua anani cheat me najua lakin namkaushia tu maana bado nilikua sina demu mwingine ( yule Ney alikua kashasepa Musoma ko lizy ndo aminio langu alafu ndo alikua Moyoni mwangu ko sikutaka kumuacha ghalfa nilikua namtafutia mbadala wake πŸ˜‰πŸ˜‚πŸ˜‚ )

Kuna siku moja Huyo Lizy aliniomba 10k ya chips nikamwambia sina alinuna akidai simjali..alafu alikua ananituhumu kuwa natembea na demu mmoja hivi mwimba kwaya ko alianza kuleta visa vya kifala...siku hyo alinuna balaa hata akutaka tuonane siku hyo jioni ( ilikua ni kawaida yetu kuonana jioni )..basi kesho yake jioni baada ya kutoka kwenye mahubiri niliamua kumpelekea 10k yake alio niomba..nilienda mitaa yao majita road ilikua saa moja hivi..nikamtuma mdogo wake aniite na kweli akaja amenuna sio kidogo..nilongea nae nikawa naona hayuko interested na mimi nikamwambia anisindikize basi akakubali...tulipita kiuchochoro flani kili hakina watu sana basi nikamtolea noti ya 10k..acha demu anirukie na kuanza kuninyonya mate πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ me nae nikayapokea na kunyonya yake pia 😘😘.

Alianza kujibebisha sasa na kutaka nimnunulie Sendo nilimwambia nitampa hela lakin alikataa akidai nimnunulie..kidume ilibid nikubali na kwa vile hela ilikuepo ya wizi sikuona uchungu kupotea...kesho nilienda town nikamchukulia sendo nzur tu za wadada kumpelekea jioni akizipima na kuzivua na kunitupia..akaanza kulalamika kuwa ina maana me cjui size ya miguu yake yani size za mademu wengine najua ila size yake sijui...nilikua kimya tu niaviokota na kurudi home nikampa dogo langu ( wa kike ) kesho yake nikarudi town tena kuchukua sendo nyingine siku hyo alifurahi akanipa mate nikala kona kwenda home...nacho mkubali huyu demu alikua anibanii nikimuomba show alikua yupo free sana.....

Nitarudi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…