Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Hadithi ya kweli ya maisha yangu

ulianza matukio ukiwa kijana mdogo but in all mungu akusaidie kama kweli umebadilika
 
"Kesho yake niliwai kumgongea rafiki angu mlango demu wake akasepa kisha tukaenda chumban mwa dokta kufanya ibada.saa moja tukaenda kusubiria boti itupeleke Kisiwa cha Izinga."

Swali, Leo umeenda kufungua sabato Mh. shemasi?
 
Yaani mie kamanda unanifurahisha jinsi mlivyo kua mnatoka kupiga papuchi halafu mnaingia kwenye ibada, au ndio yaleyale kutwanga maji kwenye kinu
 
Mwaka wa jf
Au wa jp..?
Basi mi .........
Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Inaendelea

Niliendelea kuuguza majeraha yangu hasa mguu wa kushoto ambao uliumizwa na maafande kama wiki mbili yaan mpk leo hivi navyoandika hapa jukwaani kiganja changu cha mkono wa kulia bado kina shida...

Nilifikiria sana ni biashara gani nifanye maana nilikua na mawazo mawili nifungue kagoli ka nguo ama nichezeshe *PLAY STATION GAME'S * ( Ps) wazo la kuchezesha Ps likapita na mtaji nilikua sina wakutosha ila nilisaidia na Mama,Mzee na Sister angu, nilkua naitaji 1.5 m.Ambao nilinunua Ps 3 ambazo zimechipiwa kabisa mbili,pad 6,flat screen 2 ( nch 24 ),viti vya plastik 4,benchi moja,Kodi ya Pango ambayo ni 30k kwa mwezi na mazagazaga mengine..

Hela niliyochangiwa na hao nilio waomba jumla nilipewa 900k nyingine niliambiwa nitafute.Sikuwa na sehemu ya kukopa niliwaza sana nitatoa wapi hela niongezee niliyopewa nianze kazi.

Nili plan nianze mwezi wa 4 maana ulikua ni msimu wa pasaka ( cjui pasaka ilikua ni tarh kumi na kitu huko...nimesahau)..hii biashara wadogo zangu niliwaambia lakin bro wangu ( damu ) siku mwambia maana hua siivi japo namuheshimu sana ( kipindi hiki alikua home kamaliza chuo yupo tu na M-Pesa yake )

Kuna siku nimelala asubui dogo langu anae nifuata mara ya pili alikuja chumban kwangu ana hema balaa..akanipa hela nikae nazo alafu yeye akarud kufagia Mji...

Nilihesabu hela zilikua 340k nilizificha chini ya godoro nikaendelea kulala kidogo huku namtafakari dogo...

Mida ya mchana ndo dogo ana nambia kamcheza Mtoto wa mwenye nyumba...kumbe dogo aliniibia zile funguo ambazo na mimi nilimwibia yule mtoto wa mwenye nyumba.

Nilishangaa sana kuwa dogo kaingiaje alinambia kipindi jamaa anaoga yeye aliingia spidi mpk kwenye kabati kulikua na briefcase ilikua na password ( ambazo alinitajia ) akachukua hela bila kuhesabu ndo akanilitea.

Nilipata wasi wasi kuwa jamaa akijua kuwa kapotelewa na hela itakuaje lakin kwa roho nyingine nilifurahi nikampa pole tu huyo jamaa.

Dogo langu ndo kwanza alikua form 3 ckujua huo unyamela alitoa wapi maana me sikumfundisha kabisa...zilipita kama wiki nikaona jamaa yupo kimya nilimgawia dogo 50k ambae na yeye aliwagia ndugu zake wawili ten ten kila mtu.

Nilimtuma dogo tena aende aka mcheze huyo jamaa ( mtoto wa mwenye nyumba ) siku hyo akarud na 70k..kuna Mama mmoja church nilimshirikisha hilo wazo langu alinichangia 50k.ukitoa hyo 50k niliyopewa na huyo Mama na ndugu zangu hela nyingine ilikua ya wizi...baada ya kununua hivyo vitu nilifungua Ps mtaa wa Mwisenge.biashara haikua nzuri kabisa maana hela niliyokua napata ilikua ndogo mno just imagine kwa siku napata 3k ikiwa kubwa sana aizidi 10k ko niliamua niache kwa muda ili nitafute eneo zuri la biashara.

Kipindi hicho nilijiunga kuimba kwaya kanisani ( binafsi napenda sana kuimba ).sikutegemea kama na mimi nitakuja kuimba kwaya maana hazikua ndoto zangu hizo lkn automatic nilijikuta naimba kwaya ( labda nilipita kwenye mfereji wa uimbaji kwanzia mzee wangu,Mama yangu na ndugu zangu kasoro mdogo wangu wa mwisho wa kike wote tumeimba kwaya )

Kipindi naimba kwaya ( hapo nimestop kwanza biashara nipo tu home sina ramani ) kulikua ni msimu wa MAKAMBI yalikua yanafanyika mwezi wa saba.Ko kulikua na sare lazima tununue kwenye kwaya sare zenyewe ni gharama kubwa 70k na waliweka deadline kutoa mchango ( mwezi wa 6 mwishoni ).

Hapa unatikiwa uwe makin sana ili nisikuchanganye maana ndo kwenye point ya kisa changu wahindi wanasemaga Intermission

mwez wa sita ilikua ni tarehe za mwanzoni...Kuna muhuni mmoja alikua home na ka smart phone ka tekno anauuza 50k ila nilimwambia na 30k akakubali kunipa.Nilimwita dogo langu nikamuomba funguo za chumba cha yule jamaa akanipa kisha akanitajia password za kwenye briefcase la hyo kamaa akanambia ( 711) basi nikazama ndani mpk kwenye kabati nikalifungua nikatoa briefcase nakuweka hizo nywira nilikuta kuna kama Laki na kisimu flani hivi cha nokia ya batani..nilichukua 60k nikampa yule muhuni na nyingine nikaenda nayo town kuitengeneza ile simu ( system charge ilikua mbovu ).hapo ndo kwa mara kwanza nikaanza kuiba hela na mimi.

Nilikua nikiiba naumia sana tena pale napomuona huyo jamaa nilkua nakosa kujiamini.kitu cha kushangaa huyo jamaa hata alikua haongelei hilo swala la wizi...mdogo wangu yeye alikua hana majuto kabisa.

Turudi kwenye kwaya..mwisho wa kulipa hela ya sare ilikua imefika na siku hyo ilikua ni Alhamis ndo tulitakiwa tupeleke hela ili watume dar nguo zije.

Kama kawaida niliingia chumbani kwa hyo jamaa siku hyo sikuambulia kitu.Nilichanganyikiwa nikasema sasa leo itakuaje..nilimpigia simu mama kumuomba hela nae akanipanga kuwa atanitumia jumamosi niliwaza sana nitatoa wapi hela.Maana sikutaka kuaibika kwenye kwaya eti mimi niwe miongoni mwa watu waliokosa 70k nilisema kama nikiikosa basi zoezi siendi siku hyo na kwaya naacha kuimba.

Nitarud tena kuendelea.....
 
Back
Top Bottom