Hadithi ya kweli ya maisha yangu

Kweli mganga hajigangi ukaogopa kaswende na dawa unazo...ila umenichekesha sana ulivoweka begi mapajani asione ulivokiwasha... Ila hiyo tour ilikua babkubwa navuta picha kama sio bongo yan ni mwendo wa boat na mitumbwi tu
Hizo area anazosema ni nzur kwakweli...yaan mm naendaga nakaa wiki nikiamka naona maji ..yaan kuzuriii..unataman kuhamia mazima
 
Mnamtania Mungu,mnaokota madada poa halafu mnaenda kwenye ibada
 
Kweli mkuu. Hizi ni laana kabisa, ningejua story ipo hivi nisingeisoma kabisa ila basi tu najikuta naendelea na uzi

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Dah hiii habari kutaka dawa ya kuacha pombe alaf unapewa yakutibu kichocho ni hatari sana nimecheka kinoma[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] alaf hii itakuwa inafanyika hata huku mtaani kwetu hawa wamasai hawa siwaelewi elewi
 
Nimetembea sana visiwa vya ukara sema nimeshavisahau..halafu hyo guest ya GREEN PARACHICHI KAMA NIMESHAIONA. Halafu mbona kama Bwisya ni Ukara kabisa na hyo guest ipo ukara? au nimesoma vibaya unasema ipo UK.
 
Inaendelea

Turudi kisiwani......

Siku hyo ziwani mawimbi yalikua ni makubwa kwa sababu ya upepo kitendo kilicho fanya hata sikuweza kutoa simu yangu mfukoni kwa hofu ya kudondoka ziwani kama ya rafiki angu.

Safar ilikua ni ndefu kimtindo ila japo mawimbi yalikua ni makali lakin ile injini ya mtumbwi ilikua iko imara kuyakata...nilijikuta. natamn tusiwai kufika kakukuru maana niliipenda ile hali ya kwenye boti ingawa nilikua naogopa.


Tulifika ng'ambo tukachukua teksi iliyotupeleka mpk Bwisya ambapo napo tukachukua teksi ya kwenda Nansio tulifika Nansio Kwa madereva teksi wa kwenda Kisorya feli kwa ajili ya kwenda Bunda kisha turudi Musoma......Dokta alitutaka tutoe sh 7k kila mmoja kwa ajili ya Nauli tukakubali

Dereva taksi alijikosea siku hyo alitutoza nauli tofaut na tuliyokubaliana nae ko Dokta alimpiga mpk akatoa chenji ( alikua kagoma kutoa )


Tulifika Musoma saa 4 za usiku nilikua na hela zile ambazo nilikua nikiziuza kimagendo bila dokta kujua.

Kesho yake nikiwa home niliamua kumtafuta yule manzi wa kule Ilugwa ili tufahamiane vizur maana muda kufahamiana ulikua haupo.Alinambia kuwa yeye ni Mwenyeji wa Shinyanga na alikua anasoma chuo cha buhare CDTI ( ngoja nimruke tena nitamzungumzia baadae tena huyu manzi )

Mwaka Mpya wa 2017 nilipataa majanga balaa...tareh 31 kabla ya kuingia mwaka moya kuna demu mmoja hivi nilikuwa na mihadi nae Usiku nilimuomba show akasema saa nne nimfuatee mitaa yao NYAMATARE.


Basi midaa ya saa tatu nilienda mtaani kwao ila akanambia ni subir mpk Wazazi wake walale..( niliudhika ila sikua na namna )...Ilibidi niende kwao na rafiki angu ni hapo hapo nyamatare nimsikilizie Manzi mpk anistue ni mchukue....

Kipindi cha kuukaribisha mwaka mpya hua vijana wanafanya fujo ( kuchoma matairi barabarani,Kupiga mabaruti na kero nyingine nyingi )....Sehemu zenye hizo fujo sana ni mitaa ya Nyakato, Iringo, Majita road mpaka huko Nyamatare kuelekea buhare

Police hua inadhibiti sana hyo mitaa wakati wa Mwaka mpya....Basi siku nilimsubir huyo demu ani text wapi nikajua tu kanirusha, niliamua kukaa pale kwao na rafiki ili baadae twende kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Nikiwa hapo sina hili wala lile tulishangaa tu vijana kama wawili waingia ndani na mbio...hatukuwajua sisi tulikua bado tunajiuliza kuna nn mara police watatu wakaingia na wenyewe na marungu yao bila hata kuuliza wakatushika me na rafiki pamoja na huyo kijana mmoja, mwingine cjui walimsahau....

Nilikua nawaambia maafande kuwa sisi tulikua ndani tumetulia lakin wapi....Maafande ni Nyoko yaan hawana huruma mdaa huo wametutoa nje kulikua na maafande wengine acha waanze kutupiga na Marungu yao pamoja na vitako vya bunduki....Walikua wanafoka kisenge eti tunafanya fujo...ilikua hawakurusu ujitete...nilipigwa rungu za kwenye goti na ugoko huku tunaburuzwa kwenda kwenye Fenda ( walikua wameibaki pale Nyamatare Sheli )

Narudia kusema tena police ni sio wana kabisa walinipiga mpk simu yangu ilipasuka na kilikua ki Aitel cha batani.....Tulifikishwa kwenye fenda walivyoturusha sasa [emoji1787][emoji1787][emoji1787] ndani ya fenda utadhani sisi ni gunia...Walituambia tulalie tumbo wakati huo tumebanana ( tuliwakuta wengine waliokamatwa kama sisi wapo kwenye Fenda ).

Police wanamatusi mwingine alikua anasema ngoja ni mnukuu maana maneno nayakumbuka " yani nyie badala mlale mnasumbua watu na mabaruti yenu leo tunaenda kuwafira kumamae zenu"...nilivyosika hvyo na kosa sijalifanya nilitaman nisimame niruke nikimbie lakin ningewezaje na hku tulikua tumebanana kisawasawa...na police walivyo wakuda walikua wamesimama kwenye migongo yetu [emoji23][emoji23][emoji23]...ila siku hyo sitoisahau nilijilaumu kwann nilienda huko nilimchukia yule demu kwa kuni chomesha mahindi.

Kama utani vile Fenda ilifika Central tukatolewa huku bado tunapigwa virungu....kumbe police unaingia bila hata kutenda kosa...tuliambiwa tuvue viatu ma mikanda kama kuna mtu mwenye hela akabidhi pale mapokezi...me muda huo na kasimu kangu tu niko peku nilikabidhi wakaandika kisha moja kwa moja mpk Sero...

Kwa mara ya kwanza ndo naingia Sero toka nizaliwe nilikua napasikia tu...watu walikua wengi siku hyo hasa vijana...kuna jamaa mmoja tulie ingia nae nilikuja kumjua kwa jina la Athumani baadae sana....Alikua analia vibaya mno " yara yara yara Yaalabi niokoe mimi mwanao" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila nani alie mjali sasa kwa muda ule alilia mpk akanyamaza mwenyewe..

Asubui ilifika maumivu yalikua ni makali kisenge mpk kunyosha goti la kushoto ilikua ni Tabu kwangu yani ilikua siku mbaya kwangu...pona pona ilikua ni afande mmoja hivi tulkua ni majirani ndo aliwajulisha home....Ili nitoke walidai watoe 250k na kweli Mzee alizitoa nikatoa walinambia niwe narudi kituoni kwa ajili ya upelelez, nilirud siku moja tu nyingine nikakausha...

Nitarudi baadae tena.....
 
YAAAANI MWANANGU STORY YAKO NAIFATILIA KAMA VILE NILIVYOKUWA NAFATILIA UCHAGUZI WA OCT 2020
 
Lete ndefu kidogo maana weekend Ni ndefu wakati hatuna kitu mfukoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…