Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 33,487
- 65,822
- Thread starter
- #121
"nimevunjiwa nyumba yangu kuna mradi wa serikali unakatiza karibu na kwangu pale pale, tuliahidiwa kuwa tutapewa stahiki zetu kama mimi niliahidiwa kuwa nitapewa milioni mia moja kama fidia kwa sababu pia eneo langu lilikuwa kubwa kubwa, tukasainishana kwenye makaratasi na tukavunjiwa nyumba lakini baadae tunakuja kuambiwa hatutalipwa chochote kwa sababu eti hata eneo tulilokuwa tunaishi halikuwa la kwetu lilikuwa sijui la mwekezaji gani wa Kiarabu, hapo ndo tulipochoka sasa tukaamua kwenda mahakamani lakini nako hatuelewi sijui hakimu anapewa hongo na matajiri ambao wanatalitaka eneo lile halafu kumbe wala siyo serikali kama tulivyodanganywa awali, anayelitaka eneo letu ni mtu tu mwenye pesa zake, basi vuta nikuvute ikaanzia hapo, nyumba yenyewe ndo hiyohiyo moja nayoitegemea nilioachiwa urithi na baba na mama kabla hawajafariki, ninayowasomeshea wadogo zangu mpaka mmoja amefika chuo kikuu sasa nimeipangisha wapangaji na mimi mwenyewe na wadogo zangu wawili tunaishi kwenye chumba na sebule..."
Alimeza mate kidogo kisha akaendelea....
"basi ndo vuta nikuvute sasa na ubaya wenyewe sisi tunaopigania haki yetu hatuna hata pesa ya kumpa wakili anayetutetea, tulichangishana changishana hivyo hivyo kesi ikasogea sogea lakini baadae wakili akaonekana kutoridhishwa na malipo tunayomlipa, kwanza ni madogo na pili ya kudunduliza dunduliza wakati mwingine tunamcheleweshea pesa zake mpaka tukusanye kwa watu wote, wakili mwishowe akanyoosha mikono na kuachana na kesi yetu sasa hivi hatuna wakili tena nitaishije mimi, ndo kila siku nimekuwa mtu wa kukopa kopa mpaka mtaani naaibika nimetungwa majina kibao nimehama mitaa kama saba hivi kila mtaa naacha madeni nakimbia" aliongea huku kwikwi ya kilio ikimshika
"duh kweli mambo makubwa pole sana ndo maisha kuna siku utasahau!" nilimwambia nikimpiga piga mgongoni kumbembeleza
"ndohivyo" aliongea nikachukua kitambaa na kumfuta futa machozi na wakati huo simu yake ndogo 'kiswaswadu' iliyokuwa kitandani iliita nikaichukua
"simu yako hii pokea!"
"iache tu madeni ya watu tu hayo!"
"huwezi jua ungeisikiliza kwanza weka na laudi spika" nilimshawishi akaipokea kiunyonge na kuiweka sikioni mwake
"halow!"
"halow Hawa mimi jirani yako mama Khamisi hapa!" sauti ya mwanamke ilisikika ikiwa imejawa furaha
"za leo mama Khamisi?"
"nzuri tu umeingia mtandaoni?"
"sina simu ya mtandaoni!"
"kesi yetu ya fidia tumeshinda na mahakama imeamuru tulipwe wiki hii watu wameshaanza kulipwa pesa zao tangu juzi nakutafuta we sikupati kwenye simu sijakupata!"
"unasema kweli mama Khamisi?" mwanamama Hawa aliuliza huku akisimama
"eeh wewe jina lako ni kesho mimi ndo nimetoka huko wilayani pesa zangu zimeshawekwa benki kwahiyo fanya kesho uende mapema!" mwanamke huyo aliongea, mwanamama Hawa akabaki amesimama ametoa macho na simu mkononi
"siaminiiii!!!" aliruka na kunirukia mimi kitandani tukaanguka kitandani mimi nikiwa nimelala chali nae akiwa amenilalia kwa juu....
Inaendelea

Soma kama burudani tu ya kusisimua mwili na akili ila usiyatendee kazi yaliyoandikwa