Hadithi ya kweli: Mama wa kambo

Hadithi ya kweli: Mama wa kambo

Sehemu ya pili


Safari ilikuwa ya siku nzima mpaka majira ya saa sita usiku tukaingia jijini Dar es Salaam na mvua kubwa ikinyesha siyo ya kitoto, nilishuka kwenye basi stendi ikiwa ni Ubungo wakati huo na kutazama tazama huku na kule nikiwa sina hata mwamvuli

"Frank!" mara nikasikia ninaitwa kutazama pembeni alikuwa ni mwanamama mmoja nisiyemfahamu akinifuata

"naam!"
"karibu Dar!"
"asante shikamoo!" nilimsalimia, mtu mzima kiasi ila miaka arobaini mpaka arobaini na tano hivi kwa kumtazama haraka haraka

"unanifahamu?" aliniuliza akitabasamu bila kuitikia salamu yangu ya shikamoo'

"hapana bila shaka ni mama md...."
"ndiye mimi!" aliniambia mvua ikiwa kubwa kwelikweli

"ooh sawa!" nilitabasamu nikimpa mkono
"sasa hapa nyumbani kwenda saa hizi na mvua hii changamoto kwakweli na baba yako wala hayupo hapa tukachukue tu vyumba gesti mpaka kesho asubuhi sawa?!"
"sawa mama!" nilitikisa kichwa na kuongozana na mwanamama huyo mpaka kwenye gesti moja tukaulizia vyumba tukaambiwa kimebaki kimoja tu

"tutalala hicho hicho pamoja!" mwanamama huyo alimwambia mtu wa mapokezi ikabidi nishangae kidogo

"mama kula...!" kabla sijamalizia kauli yangu yule jamaa wa mapokezi akanikatisha
"mbona kijana kama ana wasiwasi hivi?" jamaa alimwuliza mwanamama huyo

"ni mwanangu huyu!" mwanamama huyo alijibu akipewa funguo ya chumba na kutangulia mbele nami nikiwa nimebaki nimesimama sielewi elewi......

Mwanamama huyo mke wa baba yaani mchepuko wake alitangulia mbele yangu nami nikiwa nipo nyuma yake, alikuwa kajazia kwelikweli yaani nyama nyama, na nyuma kafungashia matak** makubwa mpaka nikashikwa na hasira kutokana na kitendo anachokifanya baba

"baba amepata wapi ujasiri wa kumtuma huyu mama aje anipokee?!" nilijiuliza mwenyewe huku nikiwa nimejishika kiuno

"karibu!" mwanamama huyo aliniambia huku akiufungua mlango wa chumba tulichochukua ndani ya nyumba hiyo ya wageni (guest house)

"asante!" nilimwitikia tukaingia ndani ya chumba hicho mvua ikinyesha kweli kweli nje tena ya upepo


"utaoga?"
"hapana siogi na baridi hili!"
"mh hapana lazima ukaoge bila hivyo hautalala vizuri wala!" mwanamama huyo aliniambia akinishika mkono kuniinua akiwa hajui hasira nilizonazo juu yake nikabaki namtazama tu na kumwonyesha tabasamu kwa nje nikitikisa kichwa kukubaliana na suala lake hilo la kuoga ingawa sikuwa tayari kabisa, nilitembea kwenda kwenye bafu hilo la ndani kwa ndani lakini kabla sijaingia bafuni simu ya mwanamama huyo iliita akaipokea nami nikasimama nikijibanza ukutani kumsikiliza anazungumza na nani

"halow!" nilisikia sauti ambayo moja kwa moja niliitambua kuwa ni ya baba
"halow darling za kazi?" mwanamama huyo aliitikia kwa mahaba

"upo wapi?"
"Ubungo"
"kufanya nini saa hizi?"
"kumpokea mtoto!"
"mtoto?"
"eeh si mwanao Frank jamani umesahau kama amekuja leo?"

"sasa nani kakutuma kazi hiyo na nimekwambia saa ngapi kama anakuja leo Dar umejuaje??!"

"si nimeangalia tu kwenye simu yako nikasoma meseji?"
"unataka kuniudhi sasa Penina mambo ya familia yangu yanakuhusu nini, nilishamtuma ndugu yake akampokee sababu sikutaka Frank aje nyumbani agundue kama ninaishi na mwanamke mimi nitajibu nini kwa mama yake??!"

"samahani baba jamani mimi nimetamani tu kumfahamu kijana wako huyu nisamehe baba kama nimeingilia maswala yako ya kifamilia!"

"umeniudhi sana umejitambulishaje sasa?"
"nimemwambia tu mimi ni mama yako sasa nimfiche nini nitamficha mpaka lini yaani ina maana unataka iwe siri kati yangu na wewe tu ndo mapenzi gani hayo?"

"umeniudhi sana Penina aah!"
"samahani jamani!"
"umeniudhi nitajibu nini mimi kwa mke wangu??!!" baba alijibu na kumkatia simu mwanamke wake huyo mchepuko nami nikaingia bafuni kuoga lakini nikashindwa kuoga kwanza nikaegemea ukutani nikitafakari ninayoyaona

Nikae hapa ili nipate moraly wa kutafuta hela na kutunza watoto na kutooa tena
 
Duh poleni ase ujue story zipo nyingi mpaka natamani niziunganishe thread zote iwe moja tu yaan iwe special ya hadith zangu pekee
Hapana usiunge kwa sie wavivu itachosha kusoma mkuu ! Tupeleke hivii hiviii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom