Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

duh! nilichelewa kusoma aisee hadithi mnzuri yaani naisoma huku moyo unanipiga, ila kesho hainikosi
ila sasa nikuhulize babu sorry nimekwita babu hisia zangu ndio zimenituma je kuna vitabu vyako vya hadithi? na wapi vinapatikana? maana hii presha ya kusoma kweye internet ni ngumu wakati mwingine net inazingua na hadithi imekolea unatamani uipige ngumi pc
 
HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-54-

ILIPOISHIA:
Taarifa ile haikuwa ngeni kwa Mustafa alijua mtoto kishachukuliwa na mama yake. Alirudi nyumbani haraka ili kumtuliza mkewe ambaye muda ule alikuwa amepagawa. Alipofika

alimkuta amechanganyikiwa akilia ovyo mikono kichwani. Husna alipomuona mumewe alimkimbilia na kumkumbatia na kuendeleza kilio.
“Mume wangu mwanangu ameibiwa!”


SASA ENDELEA...

Alijitahidi kumbembeleza na kumueleza watamtafuta, walipeleka taarifa polisi na kwenye vyombo vya habari lakini ajabu walipotafuta picha za mtoto hawakuziona. Taarifa ilitawanyika kila kona ambayo siri yake alikuwa akiijua Mustafa. Familia ya mume nayo iliungana na Husna katika tukio lile.
Japokuwa mtoto alikuwa amepotea lakini hali ya amani ilikuwepo kwenye ndoa na wazazi kuamini mkwe wao siyo mgumba. Walimpa moyo kuwa awe makini na watu wasiojulikana kutokana na tabia za watu kuiba watoto wachanga. Mustafa alitengeneza uongo kwa kumueleza kuwa Shehna amesema asilie kwa vile mtoto wao atarudi na kumfanya aishi kwa matumaini.
Kupotea kwa mtoto kulifanya wazazi wa Mustafa waendelee kumpa moyo Husna kwa kuhofia kumuumiza kwa kumkumbusha maumivu ya kuibiwa mtoto wake. Baada ya miezi saba kukatika, usiku mmoja Mustafa aliota akizungumza na Shehna akimueleza kuwa ni muda muafaka mkewe kushika ujauzito wa kweli.
Shehna aliendelea kumueleza mtoto yule atakuwa chini ya ulinzi wa majini mpaka atakapokuwa ndipo atarudishwa chini ya wazazi wake. Lakini wakati huo ndugu zake watakuwa wamekua, wataendelea kumlinda siku zote za uhai wake.
Baada ya wiki moja akiwa kazini mkewe alimpigia simu kumweleza mumewe hali aliyohisi, Mustafa alijua dalili zile zilikuwa majibu ya ndoto aliyoota, walipokwenda hospitali vipimo vilionesha ujauzito wa mwezi mmoja. Ujauzito ule ulikuja kawaida wa miezi tisa tofauti na mimba ya ajabu iliyotangulia ya miezi miwili tu mtoto kuzaliwa.
Ujauzito ulikwenda vizuri ulipotimiza miezi tisa alijifungua salama mtoto wa kiume, Husna baada ya kujifungua alimlinda sana mwanaye ili asirudie kosa la awali. Mtoto alikuwa katika malezi mazuri, Mustafa na Sara waliendelea na kazi zao huku Sara akiwa na somo kubwa maishani mwake kuwa mwanadamu anaweza kuwa mbaya kuliko jini pia kutofuatilia lisilokuhusu. Hakuamini kama majini wana roho nzuri siku zote aliamini ni viumbe wabaya kumbe wapo wazuri na wabaya kama wanadamu.
Mustafa alisubiri miaka mitatu ili aende kwa Shehna kwa njia ya ndoto kuwaona watoto wake japo wa kiume alimuona.
Mtoto wao naye alikuwa vizuri bila kujua akiwa mkubwa atakuwa na tabia gani?

Mwisho.
 
Wow! Kumbe kuna majini wazuri?? Mi nilijua waharibifu!!! Hadithi ni mzuri sana na inatufundisha ,ila hujanijibu je kuna vitabu vyako vya hadithi ambavyo viko madukani?
 
Sasa

wewe ulitaka Washiriki wawe akina nani wakristo au wayahudi? Acha kuleta Udini hapa mimi pia Muislam tena Maalim ninaitwa sasa

nimekuzidi hata wewe kielimu usilete Mambo ya Udini hapa kama huna kitu cha kuchangia bora usiandike kitu humu ndani tafadhali

Usiniharibie Hadithi yangu . Unajuwa ni nini maana ya neno hadithi? kama hujuwi nenda shule kwanza kamuulize Mwalimu wako ni nini

Maana ya neno Hadithi kisha ndio uje hapa kuleta ushindani wako wa mambo ya Udini nyamaza nina kuheshimu sana na wewe pia

niheshimu mimi asante.

Duu mkuu kumbe huwa unakasirika
 
Hii hadithi ni nzuri sana na ya kuvutia . Ina mafunzo pia .
Naomba wale watundu na wabunifu waiendeleze. Naona kama mwisho wa hadithi unaashiri kuwapo kwa uwezekano wa kuendelea kwa sababu ya maswali kadhaa yanayojitokeza baada ya kuifunga.
Asante sana mzizi mkavu. Tuletee kisa kingine cha kusisimua.
 
Samahani lakini...ila hii style ya quote episode nzima ya hadithi inachangia kwa kiasi kikubwa kutujazia saver!!
Afu kwa siye wengine tunaotumia simu kuaccess JF tena through JF app inatupa shida sana kufatilia episode mpya..
Nafikiri si vibaya ukareply kwa kutoquote...kama ujumbe wako mzizimkavu ataupata tu.
Asante

Asante ndugu manake Daah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom