Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Kaka mzizi mkavu fanya mambo saa hii kiongozi niko macho kama kawaida nakusubiria sijui tuko wangapi
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-25-

ILIPOISHIAJANA :
Vijakazi na watwana waliingia katika kazi ya usafi iliyochukua dakika tano kila kitu kilikuwa safi ndani. Kilibadilishwa kila kitu na kuwekwa pazia nzuri la halili na kuifanya ofisi ipendeze mara dufu. Baada ya kufanya usafi walipiga magoti mbele ya Shehna na kusema.
SASA ENDELEA…


“Mtukufu mwana wa Mfalme wa jini la bahari ya dhahabu tumemaliza kazi, kama kuna kasoro tupo tayari kwa adhabu yoyote kutoka kwako.”

“Hapana nawamini.”
“Asante mwana wa mfalme.”
Shehna hakuwa na shida ya kukagua kwa kuamini majini walikuwa wakijua usafi kuliko mwanadamu.
“Nimefurahi kwa yenu nzuri, mnaweza kuondoka.”

Kufumba na kufumbua vijakazi na watwana walitoweka na kumuacha Shehna alifurahia hali nzuri ya kupendeza ya ofisi. Alitoka nje na kumwita Mustafa aliyekuwa akizungumza na mlinzi. Alikwenda ndani na kuishangaa ofisi ilivyopendeza tofauti na siku zote.
“Duh! Kazi hii imeifanya peke yako?”
“Umemuona nani akinisaidia?”

“Hongera sana.”
“Asante, ila kama Sara hatatokea na kesho funguo iache mlangoni, nitakuwa nawahi mapema kufanya usafi kabla hujafika mpaka atakaporudi kazini .”
“Nitafanya hivyo.”

“Mustafa mimi si mkaaji ilikuja kukushukuru wa mapenzi yako matamu, hakika leo nimefaidi usichana wangu kwa kupata penzi lililokamilika. Nakuahidi baada ya kushika ujauzito nitakupatia zawadi kubwa sana.”
“Wala usihofu, lakini nina wasiwasi wa kuharibu masharti yako.”
“Wala usiwe na wasiwasi, asubuhi umenilaisishia kufanya mambo yetu bila mkeo kukusumbua. La muhimu kufanya yote kama niliyokuelekeza.”

“Nitafanya hivyo.”
“Basi nikuache uendelee na kazi.”
“Nashukuru.”
Walikumbatiana kisha Shehna aliondoka na kumuacha Mustafa alimsindiza kwa macho.
***
Wiki nzima ilikatika bila kuonekana kwa Sara huku Shehna akiendelea kufanya usafi kila siku na kuifanya ofisi izidi kupendeza. Kwa hali ile ilifikia hatua ya Mustafa kuomba Sara isirudi tena kutokana na usafi uliokuwa ukifanywa na Shehna uliifanya ofisi yake isifikiwe kwa kila aliyeingia na kutaka kupatiwa mtu mwenye uwezo wa kufanya usafi kama wa ofisini kwake.

Wakati wote huo kila siku Shehna alikwenda nyumbani kwa Mustafa na kufanya naye mapenzi kitandani kwake huku mkewe akiwa amepitiwa usingizi. Siku zote alifuata masharti aliyopewa kuyafanya kabla ya kulala. Zoezi kubwa kwake lilikuwa kumpaka mafuta mkewe ambayo humfanya alale mpaka asubuhi bila kugeuka na kuacha wafanye mambo yao bila yeye kujua kinachoendelea.
Mustafa alifanya vitu vyake siku zote kwa umakini mkubwa kwa vile mkewe hakuweza kukutana naye tena kimwili baada ya kuelezwa na Shehna ili aweze kupata mtoto huku akiendelea kutumia dawa alizopewa. Hata kulala sehemu ya ukutani hakulazimishwa kwa vile lilikuwa moja ya masharti ya dawa.
Siku zote alifanya kama alivyoelekezwa, lakini siku moja alirudi nyumbani akiwa amechoka sana na kusahau kumpaka mafuta mkewe kwa kuamini aliisha mpaka. Usiku kama kawaida Shehna aliingia ndani na kunyanyua Mustafa na kwenda naye bafuni kuoga baada ya kuoga alirudi kitandani na kuanza kuandaana kisha waliingia kwenye tendo.
Hatua ya awali iliisha kila mmoja alifurahia penzi la mwenzake kisha walipumzika kwa muda ili kujiandaa kwa hatua nyingine. Shehna kama kawaida alimpa Mustafa maji ya kunywa yaliyomrudishia nguvu na kurudi tena bafuni kuoga na kuingia hatua ya pili. Mapenzi yalipopamba moto Shehna aligugumia kimapenzi kwa kuusifia uwezo wa Mustafa kimapenzi.
Kwa vile mke wa Mustafa hakupakwa mafuta ya kumlaza, sauti ya kulalamika kimapenzi ilimshtuka usingizini.

Itaendelea Kesho Wakati kama huu

Mmmh, mbona majanga sasa haya
 
Hadithi ya kusisimuwa mimba ya jini-28-

ILIPOISHIA:
“Basi nikuache ufanye kazi.”
“Nashukuru.”
Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akijiandaa kuanza kazi ya siku ile.
SASA ENDELEA...

Msichana mmoja alionekana amelala chini ya mti mkubwa pembeni ya barabara kuu ya kutoka Dodoma kwenda Mpwapwa akiwa amejifunga kipande kichafu cha khanga kwa chini na juu matiti yalikuwa wazi.

Miguu ilikuwa pekupeku, ilijaa tope lililokauka na kujaa vumbi. Wasamaria wema waliopita njia ile waliamini yule ni mwendawazimu, lakini ilikuwa ajabu kwa eneo lile hakuna hata mmoja aliyekuwa akimfahamu.
Toka watu walipomuona amelala chini ya mti, ilipita zaidi ya saa sita bila kugeuka kitu kilichowatisha na kufikiria labda amefariki.
Walimsogelea na kumtikisa, alifumbua macho kuwatazama lakini alikuwa amechoka kwa njaa na uchovu. Walimchukua na kumpeleka kwenye makazi ya watu na kumpatia chakula baada ya kushiba, walimpatia maji ya kuoga na nguo. Alionekana ni mtu mwenye akili zake timamu wala si kichaa kama walivyomfikiria.

Baada ya kutulia, walimuuliza maswali kutaka kujua ametoka wapi na amefikaje pale.
“Unaitwa nani?”
“Sara.”
“Umetokea wapi?”
“Dar es salaam.”
“Umefikaje huku?”
“Kwani huku wapi?” aliuliza huku akipepesa macho kuishangaa sehemu ile ambayo ilikuwa ngeni kwake.
“Hapa ni Kongwa njia ielekeayo Mpwapwa.”
“Kongwa si Dodoma?” Sara alishtuka.
“Ndiyo.”
“Waongo!” Sara alibisha haku haamini kufika Dodoma kwa kutembea usiku mmoja tena kwa miguu.
“Dada kwani sehemu hii unaijua?”
“Mmh! Hapana.”
“Duh! Uliondoka kwako lini?”
“Jana usiku?”
“Mmh! Upo sawa kiakili?” mmoja alimshangaa majibu ya Sara.
“Na wala sijawahi kuugua ugonjwa wa akili.”
“Basi hapa ni Kongwa.”
“Mungu wangu, nimefikaje huku?” Sara alishtuka huku macho yakimtoka pima.
“Kwani ilikuwaje?”
Sara aliwaeleza jinsi alivyopotea baada ya kutoka kwake kuelekea kwenye banda la chipsi kununua chakula cha usiku na kujikuta akipotea njia na kushangaa kujiona yupo katikati ya pori na kutembea bila kufika mpaka alipofika chini ya mti ule alfajiri, akiwa amechoka sana na kuamua kupumzika kwa vile hakujua anapoelekea.
“Haiwezekani utoke Dar kwa miguu jana usiku ufike Dodoma alfajiri!” mtu mmoja alipingana na maelezo ya Sara.
“Basi hapa ni Kongwa mkoa wa Dodoma ndiyo maana tuna wasiwasi na maelezo yako huenda akili yako haipo sawa.”
“Akili yangu iko sawa, kwani leo ni siku gani?” aliuliza baada ya kumuona watu wakipita kuelekea kanisani.
“Jumapili.”
“Mungu wangu! Haiwezekani nitoke nyumbani Jumatatu mpaka leo Jumapili, haiwezekani nitembee kwa miguu wiki nzima, nimewakosea nini kunitesa hivi,” Sara alilalamika huku akitokwa machozi.
“Kina nani?”
“Hata najua, Mungu atanilipia.”
Sara alianza kulia na kuwafanya wasamaria wema kumbembeleza, baada ya kunyamaza. Aliwaomba msaada wa kumrudisha Dar kwa vile muda ulikuwa umekwenda, walimpa hifadhi ya kulala pale ili siku ya pili alfajiri wampandishe basi mpaka njia panda kisha apande basi kurudi Dar.
Usiku kucha hakulala kuwaza yaliyomtokea, kwake hakuamini, aliamini tukio lile ni la ndotoni halina ukweli wowote. Siku ya pili aliamshwa alfajiri na wenyeji wake na kupandishwa mabasi yanayokwenda njia panda ili apande yanayokwenda Dar es Salaam.

Baada ya kupanda haisi iliyompeleka njia panda ambapo alipanda basi la Shabib na kutulia kwenye siti, basi likiwa linakwenda aliangalia mapori ya njiani ambayo yalimfahamisha yupo safarini lakini bado hakuamini njia nzima alikuwa akijiuliza nini kilichomfanya afike mkoani Dodoma kwa miguu bila kuchoka wala kudhurika na wanyama wakali.
Pamoja na kuamini yumo ndani ya basi, bado hakuamini tukio lililomtokea ni la kweli. Kwake aliamini ile ni ndoto iliyomchanganya na akiamka asubuhi atajikuta yupo kitandani amelala. Basi lilingia Dar majira ya saa sita na nusu mchana, bado Sara hakuamini. Aliteremka kwenye basi baada ya abiria kuanza kuteremka.


Itaendelea Kesho Wakati kama huu...........
 
Mmmh, mbona majanga sasa haya

Samahani lakini...ila hii style ya quote episode nzima ya hadithi inachangia kwa kiasi kikubwa kutujazia saver!!
Afu kwa siye wengine tunaotumia simu kuaccess JF tena through JF app inatupa shida sana kufatilia episode mpya..
Nafikiri si vibaya ukareply kwa kutoquote...kama ujumbe wako mzizimkavu ataupata tu.
Asante
 
Samahani lakini...ila hii style ya quote episode nzima ya hadithi inachangia kwa kiasi kikubwa kutujazia saver!!
Afu kwa siye wengine tunaotumia simu kuaccess JF tena through JF app inatupa shida sana kufatilia episode mpya..
Nafikiri si vibaya ukareply kwa kutoquote...kama ujumbe wako mzizimkavu ataupata tu.
Asante

Mkuu, sometimes sie wengine tunapenda kuonesha from exactly where I quoted, ili hata mtu akitaka kujua nimequote from section ipi iwe rahisi kuliko ku-cut off whole part of the story na kubakiza kasehemu kidogo.
By the way, brother do not ever expect for those mobile users to enjoy JF like those who are using PC, kuna baadhi ya vitu utamiss tu or kukereka kama hiyo big quote yangu.
Asante.
 
Mkuu MziziMkavu muda tunaomba leo uwahi kidogo tunapata taabu kuamka asubuhi kuwahi kazini.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom