Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-47

ILIPOISHIA:
Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta mwanaye jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini.
"Vipi?"
Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.


SASA ENDELEA...

"Shehna nani kawasha taa?" mama yake alishtuka kuiona hali ile.
"Sijui mama, labda Mustafa."
"Ina maana hukumueleza taratibu zetu?"
"Nilimueleza hata sijui likuwaje mpaka akawasha taa?"
"Ina maana alifanya kiburi cha kibinadamu?" Bi Zaldau aliuliza kwa hasira.
"Mama yaani sijui nimechanganyikiwa, jinsi ya kumuamsha na kumuuliza, lakini naogopa kumueleza mimi ni jini."
"Hivi vitu vyote unavyomfanyia hajashtuka na kukuona kiumbe wa ajabu."
"Huwa anashtuka lakini akili yake ilionekana ngumu kukubaliana kuwa mimi jini."
"Akijua jini?"
"Anaweza kuniacha nami nampenda sana."
"Basi tumfanye hamnazo."
"Hapana mama sitaki awe hivyo, ana familia inamtegemea unafikiri akiwa hivyo atafanyaje kazi?, Lazima atafukuzwa."
"Kila kitu tutaipa familia yake na wewe kuwaeleza masharti ya kukaa naye, hatakiwi kwenda kwa mganga mpaka ujifungue."
"Mamaa, umesahau mimi sitakiwi kutoka huku kipindi hiki."
"Mmh! Hapo ndipo penye tatizo."
"Au nimrudishe kwao."
"Kumrudisha umechelewa, fanya hivi, mtume jini mmoja akachukue nguo zake kwake kisha tumrudishe ofisini ili akishtuka aamini alikuwa amelala na kuota akiwa ofisini."
"Labda tufanye hivyo."
Walimchukua na kumrudishia fahamu kabla hajajitambua walimpuliza na kumfanya apitiwe na usingizi. Waliwatuma vibaraka kwenda kuchukua nguo za Mustafa nyumbani kwake na kuzipeleka haraka kisha walimvisha na kumpeleka ofisini kwake.
Kama kawaida ulifanyika kwanza usafi kisha walimweka kwenye kiti chake na kumuacha amelalia meza na kuondoka.
Mlio wa simu ulimshtua Mustafa kwenye usingizi mzito, alijishangaa kulala ofisini kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kumtokea hata siku moja.
Alipiga miayo na kuangalia saa yake, ilimuonesha ni saa tatu asubuhi. Simu iliyokuwa pembeni yake iliendelea kuita, aliichukua na kukuta inatoka kwa mkewe, alipokea mara moja.
"Haloo mke wangu."
"Mpenzi, vipi leo?"
"Kivipi mke wangu?"
"Imekuwaje leo umeondoka bila kuniaga?"
Swali hilo lilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza aliwezaje kuondoka bila kumuaga mkewe, kila alivyojiuliza alikosa jibu. Ukimya wa kujiuliza maswali ulimfanya mkewe kumuuliza.
"Mume wangu."
"Naam."
"Mbona hunijibu, au ulikuwa na kazi muhimu ofisini?"
"Ndiyo," Mustafa alikubali ili kuepusha maswali asiyoyaelewa kwa wakati ule.
"Hata kama hivyo, basi ungenipigia simu kunijulisha maana nimeshtuka kuamka asubuhi bila kukuona kitandani."
"Yaani simu yako ndiyo iliyonishtua na kuachana na kompyuta toka nilipoingia," alitengeneza uongo unaofanana na kweli japokuwa bado alikuwa hajielewi kwa vile alikuwa hakumbuki kama asubuhi alitokea nyumbani kwake.
"Pole mume wangu, lakini upo salama?"
"Asante nipo sawa sijui wewe mpenzi wangu niliyeondoka bila kukuaga."
"Mi sijambo, hujambo imeongezeka baada ya kuishusha presha yangu."
"Pole sana mke wangu."
"Asante, basi nikuache ufanye kazi."
"Asante mke wangu."
Baada ya kukata simu alijikuta mtu mwenye mawazo mengi sana baada ya kujikuta amelala ofisini bila kukumbuka alifika pale muda gani mpaka kumfanya alale ofisini tena kwa muda mrefu.
Alinyanyuka kitini na kujinyoosha mwili uliokuwa umechoka sana.
Baada ya kujinyoosha na kutengeneza nguo zake vizuri, alitoka nje ili kuzungumza na mlinzi kutaka kujua amefika saa ngapi mpaka kujikuta muda ule amelala. Alikwenda hadi getini, mlinzi alipomuona alimshangaa na kumuuliza kwa sauti ya juu.
"Bosi leo umelala ofisini?"
"Kwa nini?"
"Sijakuona kupita pia macho yamevimba kwa usingizi."
"John, jana nilipotoka hukuniona?"
"Nilikuona, ajabu sijakuona kupita kuingia lakini unatokea ndani ya ofisi."
"Una uhakika hujaniona napita kuingia ofisini?"
"Sijakuona ndiyo maana nakushangaa."
"Mmh! Ipo kazi."
"Kwani vipi, mbona kama huelewi?"
"John hebu njoo ofisini."
Mustafa aliongozana na mlinzi hadi ofisini ili wazungumze vizuri kwani muda ule alikuwa hajielewi. Baada ya kufika ofisini, Mustafa alimweleza mlinzi.
"Kaa chini."
John alikaa kwenye kiti kumsikiliza bosi wake, Mustafa baada ya kukaa alitulia kwa muda kuvuta kumbukumbu kwa yote yaliyomtokea na kutaka ushauri kwa mlinzi kwani alianza kuchanganyikiwa baada ya baadhi ya mambo kuyaona kama mauzauza. Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama.
"John," Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama.
"Naam."
"Kuna kitu kinanichanganya sana."
"Kitu gani bosi?"
"Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?"
"Mambo gani?"
"Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?"
"Ndiyo."
"Unamuonaje?"
"Kivipi?"

"Unamuona yupo kama wanawake wengine?"
"Ndiyo, kwani vipi?"
"Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama yule?"
"Mmh! Sijawahi, wewe umemtoa wapi? Kwa kweli ni mzuri sana tena sana, ajabu kila nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya moyo hunienda mbio."
"Unajua kwa nini?"
"Hata sijui."
"Mimi nina wasiwasi na yule mwanamke ni ji...."
Mustafa alinyamaza ghafla baada ya kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi John bali Shehna akiwa anamtazama uso wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.
Alimuokota na kumkalisha chini kisha alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini sauti haikutoka.
Alimpigia simu mkewe ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka kumkuta mumewe kwenye hali ile.


Itaendelea jumatatu....
 
HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-48

IILIPOISHIA:
Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama.
"John," Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama.
"Naam."
"Kuna kitu kinanichanganya sana."
"Kitu gani bosi?"

"Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?"
"Mambo gani?"
"Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?""Ndiyo."
"Unamuonaje?"
"Kivipi?"

SASA ENDELEA...

"Unamuona yupo kama wanawake wengine?"
"Ndiyo, kwani vipi?"
"Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama yule?"
"Mmh! Sijawahi wewe umemtoa wapi, kwa kweli ni mzuri sana tena sana ajabu kila nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya moyo hunienda mbio."

"Unajua kwa nini?"
"Hata sijui."
"Mimi nawasiwasi na yule mwanamke ni ji...."

Mustafa alinyamaza ghafla baada ya kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi John bali Shehna akiwa anamtazama uso wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.Alimuokota na kumkalisha chini kisha alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini sauti haikutoka. Alimpigia simu mkewe ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka kumkuta mumewe kwenye hali."Vipi ilikuwaje?" alimuuliza mlinzi.
"Tulikuwa tukizungumza ghafla nilimuona mwenzangu akishtuka na kuanguka chini. Nilipomuinua kila alipotaka kusema sauti ilipotea."
"Sasa kipi kimempata jamani mume wangu?" Husna aliuliza."Hata mi nashangaa, kwa kweli siku ya leo simuelewielewi kabisa bosi."
"Inawezekana ni malaria tumuwahishe hospitali."
Mustafa kila alipojaribu kuzungumza sauti haikutoka, alikwishajua makosa yake kwa kutaka kutoa siri ya Shehna ambaye alifahamu kuwa si kiumbe cha kawaida kutokana na matukio yaliyokuwa ya kimtokea japo awali hakutaka kukubaliana na akili yake kuwa Shehna si kiumbe cha kawaida.Aliamini yote yaliyotokea haikuwa ndoto bali kweli baada ya kuupata ukweli wa wasiwasi wake wa tumbo la Shehna. Vyote alivyoviona na kujikuta amelala katika ya bahari aliamini moja kwa moja mpenzi wake si mtu wa kawaida bali jini japokuwa hakuwahi kumuona.Alijiuliza nini hatima yake baada ya kutaka kuitoa siri ya Shehna ambayo hakutaka kiumbe chochote akijue. Aliwasikia aliyopanga jinsi ya kumpeleka hospitali, aliwakatalia kwa kutikisa kichwa na kuomba kurudishwa nyumbani kwa kuwaandikia kwenye kalatasi.
"Sasa mume wangu utaponaje?""Nirudisheni nyumbani," aliwaandikia kuwasisitiza wasimpeleke hospitali. Lakini alipoulizwa anaumwa nini aliwambia hajui ila wamrudishe nyumbani. Mkewe alikubaliana na mumewe na kumrudisha nyumbani.
Mustafa alitegemea kupata simu kutokwa kwa Shehna naye apate nafasi ya kuomba msamaha. Lakini wiki ilikatika bila dalili zozote za simu kutoka kwa Shehna, kazini hakuweza kwenda kwa wiki nzima ilibidi apewe mtu mwingine nafasi ile huku kampuni ikijitolea kumtafutia matibabu.Hospitali zote alizokwenda halikuonekana na tatizo lolote, Mustafa aliogopa kuwaeleza sababu ya yeye kuwa vile kwa kuhofia adhabu zaidi toka kwa Shehna. Baada ya tiba ya hospitali kushindwa, watu walimshauri Husna kuangalia upande wa pili labda mumewe kachezewa. Mustafa pia hakutaka kwenda kwa mganga kwa kuhofia kukatazwa kwa mkewe kwenda kwa mganga na Shehna wakati wa matatizo. Lakini ilibidi akubali kwa vile ndugu zake wasinge muelewa.Ilipelekwa kwa mganga mmoja Vingunguti, alipofika walisubiri kwa muda ndipo walipopata nafasi ya kuonana na mganga. Alikuwa mganga kijana lakini alikuwa mtu aliyejijengea sifa kutokana na kuwasaidia watu matatizo yao. Baada ya kukaa mganga alitaka kujua wateja wake wana tatizo gani.
Husna mkewe alimuhadithia mganga toka siku ya kwanza kutokewa na tatizo lile kutokana na maelezo ya mlinzi na hatua walizochukua mpaka siku ile waliyompeleka mbele yake.Baada ya kuwasikiliza alishika mkono wa kulia kwenye paji la uso, baada ya muda akitikisa kichwa kama amesisimka na kuanza kutua mbwewe mfurulizo kisha aliweka mkono sikioni kama anasikiliza simu na kuwa kama anakubaliana alichokisikia kupitia kiganja chake cha mkono na yeye alijibu kwa kusema:
"Eeh... ndiyo... ndiyo...ndiyo... sawasawa...sawasawa... hapana...eeh...ndiyo... hapana...sawa..sawa nimekuelewa."Baada ya kuzungumza vile kwa zaidi ya robo saa alitoa mkono sikioni na kuwatazama wateja wake kwa kutembeza macho kwa kila mmoja huku macho yake yakionekana kumeremeta kama ya simba na kuwatisha wateja wake. Wote walikuwa kimya wakimsikiliza kwa sauti kama mtu anayevuta moshi wa kitu ndani alisema:"Tatizo nimeliona, lakini linaonesha mwenyewe analijua tatizo."

"Kwa hiyo unatusaidia vipi?"
"Dawa yake hakuna ila naomba wote mtoke abakie mgonjwa," mganga aliomba kuachwa peke yake na mgonjwa.

"Mmh! Kwa hiyo ndiyo atapona?" Husna aliuliza."Naomba kwanza mtoke."
Walitoka nje na kumuacha Mustafa na mganga, baada ya kutoka mganga alitulia kwa muda kisha alimwita Mustafa kwa jina lake.
"Mustafa."
"Naam," sauti ilitoka.

"Unajua tatizo lako?""Ndiyo."
"Kwa nini ulifanya vile?"
"Nilikuwa na wasiwasi na mpenzi wangu kutokana na mimba yake, ndiyo maana nilikiuka masharti yake ili nione gizani kuna nini."
"Unajua kilichompata msaidizi wako?"

"Sijui.""Ubishi kama wako, sasa hivi ni mbwa."
"Mungu wangu!" Mustafa alishtuka na kushika mdomo.
"Baada ya kufanya kosa la kwanza bado umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri nje.""Jini?" Mustafa alishtuka.
"Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri, mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba yake."
"Sasa nitafanyaje?""Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati unataka kutoa siri nje, amesababisha maumivu makali ya tumbo sasa hivi yupo hoi. Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kuvuli chako kimo ndani ya damu yako ambayo wale wanao walio tumboni katika ujauzito ile."Hukutakiwa kuuona tumbo akiwa katika umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule, lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana. Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukutaka kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu ambayo itaisha mpaka ajifungue."
"Lini?""Baada ya miaka miwili."

"Miaka miwili niwe hivihivi?" Mustafa alishuka.
"Sasa nitafanyaje?"Itaendelea kwenye
ITAENDELEA TENA
 
Mbona hadithi zako za majini hawaendi kuombewa kanisani?Dawa ya majini ni Jina la Yesu tu..waganga wote wanazingua sanasana wanakuongezea lingine
 
HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-49

ILIPOISHIA:
"Baada ya kufanya kosa la kwanza bado umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri nje."
"Jini?" Mustafa alishtuka.
"Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri, mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba yake."
"Sasa nitafanyaje?"
SASA ENDELEA...

"Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati unataka kutoa siri nje, amesababisha maumivu makali ya tumbo kwa vile alikurupuka sasa hivi yupo hoi. Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kivuli chako kimo ndani ya damu yako ambayo ni wale wanao walio tumboni katika ujauzito ule.
"Hukutakiwa kuona tumbo akiwa katika umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule, lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana kwako. Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukataka kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu ambayo haitaisha mpaka ajifungue."
"Lini?"
"

Baada ya miezi saba atakapojifungua."
"Mmh! Miezi saba niwe hivihivi?" Mustafa alishuka.
"Hiyo ndiyo faida ya kiburi chako na adhabu hiyo ni ndogo kuliko zote ambazo amezitoa mama yake baada ya Shehna kuingilia kati kitendo chako kile kimemuumiza sana mama yake. Bila hivyo ulitaka kugeuzwa hamnazo."
"Mungu wangu, sasa utanisaidia vipi?"
"Sina msaada wowote zaidi ya kuitumikia adhabu yako, zaidi ya hapo ukitaka chokochoko utapotea wewe na waliokuzunguka."
"Siwezi kuonana na Shehna nimuombe msamaha?"
"Yupo katika uangalizi mkali baada ya kutoka ujinini bila idhini ya wazazi wake ili kukuzuia usiitoe siri yake na kumsababishia matatizo makubwa sasa hivi hana kauli, hajiwezi kwa lolote."
"Kwa hiyo utakuwaje?" Mustafa alishtuka.
"Adhabu yako ni kuitunza siri hii kwa miezi saba, cha kuomba Shehna apone upesi ili uweze kukupunguzia adhabu au kukuondolea ububu."
"Kwa hiyo baada ya mazungumzo narudia katika hali ya ububu?"
"Ndiyo usalama wako."
"Itanibidi nikubali sina jinsi," Mustafa alikubali kwa shingo upande.
Baada ya makubaliano aliitwa Husna mke wa Mustafa na mtu aliyemsindikiza ambao waliamini watakuta mabadiliko ya kukuta akizungumza. Lakini ilikuwa tofauti na mawazo yao, Mustafa alikuwa bado yupo katika hali ya ububu.
"Umefika wapi?" Husna aliuliza.
"Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu imeonesha ugonjwa huu utatoka taratibu bila kutumia dawa yoyote."
"Itachukua muda gani?"
"Sijajua, ila msirogwe kwenda kwa mganga yeyote eti amponye, dawa atakayompa ndiyo itakayomfanya awe bubu milele."
"Kwa hiyo hata panadol tusimpe akiumwa?" Husna aliuliza.
"Dawa zote mpeni, ila si za kutibu ugonjwa huu, msikubali kumpeleka kwenye maombi ya aina yoyote au kwa mganga yeyote. Ukifanya hivyo mtanikumbuka."
"Sawa tunashukuru."
Baada ya kukubaliana na mganga walimchukua mgonjwa wao ambaye ilikuwa vigumu kuamini anaumwa kwani alikuwa kwenye hali ya kawaida na kurudi naye nyumbani.

***
Siku zilizidi kukatika huku Mustafa akiwa katika hali ya ububu na Sara akiwa katika umbile la mbwa. Mateso makubwa yalikuwa kwa Sara ambaye aliendelea kuishi maisha ya kujificha kukimbia watoto kumpiga mawe na kulala kwenye majumba mabovu.
Chini ya bahari, Shehna alipata nafuu haraka sana na kuweza kukaa hata kula mwenyewe baada ya kupoteza fahamu kwa miezi mitatu iliyotishia uhai wake. Kukubali kwa Mustafa kuendelea kuwa katika hali ya ububu na kuyakubali maelekezo ya mganga, ile ilimsaidia sana kuwahi kupata nafuu.
Kama mkewe Mustafa angekuwa mbishi lazima angewapoteza mumewe na Shehna pamoja na watoto waliokuwa tumboni. Baada ya kupata nafuu alitaka kujua Mustafa yupo katika hali gani kwani aliamini hasira za mama yake lazima angemfanya kitu kibaya.
Katika vitu vyote alimkataza mama yake kumuua hata kumpa adhabu kali mpenzi wake.
"Mama mpenzi wangu yupo katika hali gani?"
"Nilimgeuza bubu ili asitoe siri mpaka muongee wenyewe na kukubaliana."
"Nimepona, vipi hali yake kwa sasa?"
"Bado sijamtoa ububu lakini niliyaangalia maisha yake ya siku zote, ila amenifurahisha kutotafuta dawa kwa ajili ya kutibu ububu. Kitendo kile kimesaidia wewe kupata nafuu upesi."
"Mustafa ni msikivu sijui kwa nini siku ile hakutaka kunielewa mpaka akawasha taa."
"Wewe ndiye mwenye makosa, ulitakiwa kujitambulisha mapema kwa vile alikuwa akikupenda sana, angekuelewa."
"Mama nilihofia kumueleza mimi jini, angenikimbia."
"Ona sasa alikuwa anatoa siri nje kwa vile alikuwa hakuelewi, kila kitu kingekuwa wazi, ububu na uelewa wake ndiyo nafuu yako, bila hivyo ungekufa, hali ilikuwa mbaya."
&[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Sasa nifanye nini?"
"Aletwe leo aambiwe ukweli lazima atakuelewa tu."
"Sawa mama."
Malkia Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu mama wa Shehna walikubaliana na mwanaye usiku wa siku ile Mustafa apelekwe chini ya bahari.
***
Mustafa alishituka usingizini na kujikuta akiwa pembeni ya Shehna ambaye tumbo lake lilikuwa limeongezeka katika umbile la kibinadamu lililokuwa ndani vazi la kulalia. Shehna alikuwa akimtazama huku macho yakiwa yamejaa machozi na kuongeza uzuri wake.
"Shehna."
"A..abeee," aliitikia kwa sauti ya kilio.
"Nisamehe mpenzi wangu."
"Huna kosa, nisamehe mimi."
"Kwa kosa gani mpenzi?"
"Nimekutia kwenye mateso bila kosa."
"Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza."
"Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema."


Itaendelea siku ya Alkhamisi ijayo.....
 
Ahsnte mimi nasubiri ya 52 kuna mahala nimebamba mpaka 51kuweka si.vizuri ntakua nimemuingilia mzizi ila anaetaka anipm nitamwelekeza zilipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom