Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Hadithi ya kusisimua- Mimba ya Jini

Mzizi mkavu Mpaka apigiwe magoti

Pole.
Uki google "global publishers mikasa" huo mzigo utaukuta huko.
Mimi nimeanza kusoma hadithi au riwaya za kiswahili hasa zile za zamani. Ni burudani sana.Natafuta vitabu ya Elvis Musiba sivipati.Muuzaji vitabu mmoja aliniambia eti vimepigwa marufuku na serikali. Nilishangaa sana.
 
Last edited by a moderator:
HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-46

IILIPOISHIA:

Muda wote John alikuwa ametulia
akimuangalia bosi wake aliyekuwa
ameinama.
“John,” Mustafa alimwita huku akinyanyua
kichwa kumtazama.
“Naam.”
“Kuna kitu kinanichanganya sana.”
“Kitu gani bosi?”
“Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya
ndotoni au kweli?”
“Mambo gani?”
“Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja
hapa?”
“Ndiyo.”
“Unamuonaje?”
“Kivipi?”
SASA ENDELEA...
“Unamuona yupo kama wanawake wengine?”
“Ndiyo, kwani vipi?”
“Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama
yule?”
“Mmh! Sijawahi wewe umemtoa wapi, kwa
kweli ni mzuri sana tena sana ajabu kila
nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya
moyo hunienda mbio.”
“Unajua kwa nini?”
“Hata sijui.”
“Mimi nawasiwasi na yule mwanamke ni ji....”
Mustafa alinyamaza ghafla baada ya
kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi
John bali Shehna akiwa anamtazama uso
wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka
sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John
aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka
kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.
Alimuokota na kumkalisha chini kisha
alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini
ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John
alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa
ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini
sauti haikutoka. Alimpigia simu mkewe
ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka
kumkuta mumewe kwenye hali.
“Vipi ilikuwaje?” alimuuliza mlinzi.
“Tulikuwa tukizungumza ghafla nilimuona
mwenzangu akishtuka na kuanguka chini.
Nilipomuinua kila alipotaka kusema sauti
ilipotea.”
“Sasa kipi kimempata jamani mume wangu?”
Husna aliuliza.
“Hata mi nashangaa, kwa kweli siku ya leo
simuelewielewi kabisa bosi.”
“Inawezekana ni malaria tumuwahishe
hospitali.”
Mustafa kila alipojaribu kuzungumza sauti
haikutoka, alikwishajua makosa yake kwa
kutaka kutoa siri ya Shehna ambaye
alifahamu kuwa si kiumbe cha kawaida
kutokana na matukio yaliyokuwa ya kimtokea
japo awali hakutaka kukubaliana na akili yake
kuwa Shehna si kiumbe cha kawaida.
Aliamini yote yaliyotokea haikuwa ndoto bali
kweli baada ya kuupata ukweli wa wasiwasi
wake wa tumbo la Shehna. Vyote alivyoviona
na kujikuta amelala katika ya bahari aliamini
moja kwa moja mpenzi wake si mtu wa
kawaida bali jini japokuwa hakuwahi kumuona.
Alijiuliza nini hatima yake baada ya kutaka
kuitoa siri ya Shehna ambayo hakutaka
kiumbe chochote akijue. Aliwasikia
aliyopanga jinsi ya kumpeleka hospitali,
aliwakatalia kwa kutikisa kichwa na kuomba
kurudishwa nyumbani kwa kuwaandikia
kwenye kalatasi.
“Sasa mume wangu utaponaje?”
“Nirudisheni nyumbani,” aliwaandikia
kuwasisitiza wasimpeleke hospitali. Lakini
alipoulizwa anaumwa nini aliwambia hajui ila
wamrudishe nyumbani. Mkewe alikubaliana na
mumewe na kumrudisha nyumbani.
Mustafa alitegemea kupata simu kutokwa
kwa Shehna naye apate nafasi ya kuomba
msamaha. Lakini wiki ilikatika bila dalili
zozote za simu kutoka kwa Shehna, kazini
hakuweza kwenda kwa wiki nzima ilibidi
apewe mtu mwingine nafasi ile huku kampuni
ikijitolea kumtafutia matibabu.
Hospitali zote alizokwenda halikuonekana na
tatizo lolote, Mustafa aliogopa kuwaeleza
sababu ya yeye kuwa vile kwa kuhofia adhabu
zaidi toka kwa Shehna. Baada ya tiba ya
hospitali kushindwa, watu walimshauri Husna
kuangalia upande wa pili labda mumewe
kachezewa. Mustafa pia hakutaka kwenda
kwa mganga kwa kuhofia kukatazwa kwa
mkewe kwenda kwa mganga na Shehna wakati
wa matatizo. Lakini ilibidi akubali kwa vile
ndugu zake wasinge muelewa.
Ilipelekwa kwa mganga mmoja Vingunguti,
alipofika walisubiri kwa muda ndipo
walipopata nafasi ya kuonana na mganga.
Alikuwa mganga kijana lakini alikuwa mtu
aliyejijengea sifa kutokana na kuwasaidia
watu matatizo yao. Baada ya kukaa mganga
alitaka kujua wateja wake wana tatizo gani.
Husna mkewe alimuhadithia mganga toka siku
ya kwanza kutokewa na tatizo lile kutokana
na maelezo ya mlinzi na hatua walizochukua
mpaka siku ile waliyompeleka mbele yake.
Baada ya kuwasikiliza alishika mkono wa kulia
kwenye paji la uso, baada ya muda akitikisa
kichwa kama amesisimka na kuanza kutua
mbwewe mfurulizo kisha aliweka mkono
sikioni kama anasikiliza simu na kuwa kama
anakubaliana alichokisikia kupitia kiganja
chake cha mkono na yeye alijibu kwa kusema:
“Eeh... ndiyo... ndiyo...ndiyo...
sawasawa...sawasawa... hapana...eeh...ndiyo...
hapana...sawa..sawa nimekuelewa.”
Baada ya kuzungumza vile kwa zaidi ya robo
saa alitoa mkono sikioni na kuwatazama
wateja wake kwa kutembeza macho kwa kila
mmoja huku macho yake yakionekana
kumeremeta kama ya simba na kuwatisha
wateja wake. Wote walikuwa kimya
wakimsikiliza kwa sauti kama mtu anayevuta
moshi wa kitu ndani alisema:
“Tatizo nimeliona, lakini linaonesha mwenyewe
analijua tatizo.”
“Kwa hiyo unatusaidia vipi?”
“Dawa yake hakuna ila naomba wote mtoke
abakie mgonjwa,” mganga aliomba kuachwa
peke yake na mgonjwa.
“Mmh! Kwa hiyo ndiyo atapona?” Husna
aliuliza.
“Naomba kwanza mtoke.”
Walitoka nje na kumuacha Mustafa na
mganga, baada ya kutoka mganga alitulia kwa
muda kisha alimwita Mustafa kwa jina lake.
“Mustafa.”
“Naam,” sauti ilitoka.
“Unajua tatizo lako?”
“Ndiyo.”
“Kwa nini ulifanya vile?”
“Nilikuwa na wasiwasi na mpenzi wangu
kutokana na mimba yake, ndiyo maana
nilikiuka masharti yake ili nione gizani kuna
nini.”
“Unajua kilichompata msaidizi wako?”
“Sijui.”
“Ubishi kama wako, sasa hivi ni mbwa.”
“Mungu wangu!” Mustafa alishtuka na kushika
mdomo.
“Baada ya kufanya kosa la kwanza bado
umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka
kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi
mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo
ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri
nje.”
“Jini?” Mustafa alishtuka.
“Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa
si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri,
mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa
jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba
yake.”
“Sasa nitafanyaje?”
“Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati
unataka kutoa siri nje, amesababisha
maumivu makali ya tumbo sasa hivi yupo hoi.
Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili
ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa
lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kuvuli
chako kimo ndani ya damu yako ambayo wale
wanao walio tumboni katika ujauzito ile.
“Hukutakiwa kuuona tumbo akiwa katika
umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule,
lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana.
Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukutaka
kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu
ambayo itaisha mpaka ajifungue.”
“Lini?”
“Baada ya miaka miwili.”
“Miaka miwili niwe hivihivi?” Mustafa
alishtuka.


ITAENDELEA...
 
HADITHI YA KUSISIMUWA MIMBA YA JINI-47

ILIPOISHIA:
Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta mwanaye jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini.
"Vipi?"
Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.
SASA ENDELEA...


"Shehna nani kawasha taa?" mama yake alishtuka kuiona hali ile.
"Sijui mama, labda Mustafa."
"Ina maana hukumueleza taratibu zetu?"
"Nilimueleza hata sijui likuwaje mpaka akawasha taa?"
"Ina maana alifanya kiburi cha kibinadamu?" Bi Zaldau aliuliza kwa hasira.
"Mama yaani sijui nimechanganyikiwa, jinsi ya kumuamsha na kumuuliza, lakini naogopa kumueleza mimi ni jini."
"Hivi vitu vyote unavyomfanyia hajashtuka na kukuona kiumbe wa ajabu."
"Huwa anashtuka lakini akili yake ilionekana ngumu kukubaliana kuwa mimi jini."
"Akijua jini?"
"Anaweza kuniacha nami nampenda sana."
"Basi tumfanye hamnazo."
"Hapana mama sitaki awe hivyo, ana familia inamtegemea unafikiri akiwa hivyo atafanyaje kazi?, Lazima atafukuzwa."
"Kila kitu tutaipa familia yake na wewe kuwaeleza masharti ya kukaa naye, hatakiwi kwenda kwa mganga mpaka ujifungue."
"Mamaa, umesahau mimi sitakiwi kutoka huku kipindi hiki."
"Mmh! Hapo ndipo penye tatizo."
"Au nimrudishe kwao."
"Kumrudisha umechelewa, fanya hivi, mtume jini mmoja akachukue nguo zake kwake kisha tumrudishe ofisini ili akishtuka aamini alikuwa amelala na kuota akiwa ofisini."
"Labda tufanye hivyo."
Walimchukua na kumrudishia fahamu kabla hajajitambua walimpuliza na kumfanya apitiwe na usingizi. Waliwatuma vibaraka kwenda kuchukua nguo za Mustafa nyumbani kwake na kuzipeleka haraka kisha walimvisha na kumpeleka ofisini kwake.
Kama kawaida ulifanyika kwanza usafi kisha walimweka kwenye kiti chake na kumuacha amelalia meza na kuondoka.
Mlio wa simu ulimshtua Mustafa kwenye usingizi mzito, alijishangaa kulala ofisini kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kumtokea hata siku moja.
Alipiga miayo na kuangalia saa yake, ilimuonesha ni saa tatu asubuhi. Simu iliyokuwa pembeni yake iliendelea kuita, aliichukua na kukuta inatoka kwa mkewe, alipokea mara moja.
"Haloo mke wangu."
"Mpenzi, vipi leo?"
"Kivipi mke wangu?"
"Imekuwaje leo umeondoka bila kuniaga?"
Swali hilo lilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza aliwezaje kuondoka bila kumuaga mkewe, kila alivyojiuliza alikosa jibu. Ukimya wa kujiuliza maswali ulimfanya mkewe kumuuliza.
"Mume wangu."
"Naam."
"Mbona hunijibu, au ulikuwa na kazi muhimu ofisini?"
"Ndiyo," Mustafa alikubali ili kuepusha maswali asiyoyaelewa kwa wakati ule.
"Hata kama hivyo, basi ungenipigia simu kunijulisha maana nimeshtuka kuamka asubuhi bila kukuona kitandani."
"Yaani simu yako ndiyo iliyonishtua na kuachana na kompyuta toka nilipoingia," alitengeneza uongo unaofanana na kweli japokuwa bado alikuwa hajielewi kwa vile alikuwa hakumbuki kama asubuhi alitokea nyumbani kwake.
"Pole mume wangu, lakini upo salama?"
"Asante nipo sawa sijui wewe mpenzi wangu niliyeondoka bila kukuaga."
"Mi sijambo, hujambo imeongezeka baada ya kuishusha presha yangu."
"Pole sana mke wangu."
"Asante, basi nikuache ufanye kazi."
"Asante mke wangu."
Baada ya kukata simu alijikuta mtu mwenye mawazo mengi sana baada ya kujikuta amelala ofisini bila kukumbuka alifika pale muda gani mpaka kumfanya alale ofisini tena kwa muda mrefu.
Alinyanyuka kitini na kujinyoosha mwili uliokuwa umechoka sana.
Baada ya kujinyoosha na kutengeneza nguo zake vizuri, alitoka nje ili kuzungumza na mlinzi kutaka kujua amefika saa ngapi mpaka kujikuta muda ule amelala. Alikwenda hadi getini, mlinzi alipomuona alimshangaa na kumuuliza kwa sauti ya juu.
"Bosi leo umelala ofisini?"
"Kwa nini?"
"Sijakuona kupita pia macho yamevimba kwa usingizi."
"John, jana nilipotoka hukuniona?"
"Nilikuona, ajabu sijakuona kupita kuingia lakini unatokea ndani ya ofisi."
"Una uhakika hujaniona napita kuingia ofisini?"
"Sijakuona ndiyo maana nakushangaa."
"Mmh! Ipo kazi."
"Kwani vipi, mbona kama huelewi?"
"John hebu njoo ofisini."
Mustafa aliongozana na mlinzi hadi ofisini ili wazungumze vizuri kwani muda ule alikuwa hajielewi. Baada ya kufika ofisini, Mustafa alimweleza mlinzi.
"Kaa chini."
John alikaa kwenye kiti kumsikiliza bosi wake, Mustafa baada ya kukaa alitulia kwa muda kuvuta kumbukumbu kwa yote yaliyomtokea na kutaka ushauri kwa mlinzi kwani alianza kuchanganyikiwa baada ya baadhi ya mambo kuyaona kama mauzauza. Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama.
"John," Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama.
"Naam."
"Kuna kitu kinanichanganya sana."
"Kitu gani bosi?"
"Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?"
"Mambo gani?"
"Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?"
"Ndiyo."
"Unamuonaje?"
"Kivipi?"
Itaendelea Jumatano wiki ijayo.
"Unamuona yupo kama wanawake wengine?"
"Ndiyo, kwani vipi?"
"Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama yule?"
"Mmh! Sijawahi, wewe umemtoa wapi? Kwa kweli ni mzuri sana tena sana, ajabu kila nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya moyo hunienda mbio."
"Unajua kwa nini?"
"Hata sijui."
"Mimi nina wasiwasi na yule mwanamke ni ji...."
Mustafa alinyamaza ghafla baada ya kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi John bali Shehna akiwa anamtazama uso wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.
Alimuokota na kumkalisha chini kisha alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini sauti haikutoka.
Alimpigia simu mkewe ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka kumkuta mumewe kwenye hali ile.

Itaendelea jumatatu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom