KOSA LANGU NI LIPI? Sehemu ya 13
ILIPOISHIA
Joyce alimsikiliza Mama Fredy kwa umakini na
kusema "Lakini mama mbona unafika huko"
Alilalama Joyce Mama Fredy akamjibu kwa
sauti iliyojaa jazba "Huko wapi?Ahera au, tena
sikiliza nikuambie fanya ufanyalo mimi nahitaji
mjukuu. alaah! Hivi unafikiri hili jambo ni dogo
eeh, mimi naondoka lakini tuliyoyazungumza
hapa ukae nayo kichwani na uyafanyie kazi"
Aliongea huku akiondoka na kumuacha Joyce
akiwa ameketi pale sebuleni.
INAPOENDELEA
Hali hiyo ilimuumiza sana Joyce. Baadaye
aliamua kwenda kwa Lina na kumueleza hali
halisi mambo yanavyoendelea. Lina rafiki
yangu nisaidie, naogopa kwenda Hospitali nina
hofu maisha niliyopitia zamani, nadhani hata
wewe unajua kuwa mimi nilikuwa nikitoa sana
mimba.yawezekana ikawa ndiyo sababu.Na
Fredy amenionyesha vipimo vyake yeye hana
tatizo embu nishauri nifanyeje.
Lina aliguna kidogo na kusema Sasa hapo
rafiki mimi nakushauri jaribu kuwa na
mwanamume mwingine uangalie kama
utapata mimba Joyce alishtuka na kusema
Wewe Lina yaani nimsaliti mume wangu?
Hapana haiwezekani na tena yeye hana tatizo
nahisi mimi ndiye mwenye matatizo. Lina
alicheka kidogo kwa dharau nakusema
Unanichekesha wewe, inamaana Joyce
umeshakuwa na wanaume wangapi kipindi cha
nyuma, leo hii unaogopa kujaribu kuwa na
mwanamume mmoja tu. Joyce kwa sauti ya
upole akasema "Usiseme hivyo Lina hayo
mambo yalikuwa zamani nawala sikudhamiria
kutenda zilikuwa ni shida tu, mimi sikupenda
kuwa dada poa. Hata na hivyo nimeolewa na
namuheshimu sana mume wangu" Alisema
Joyce.
"hahahaha unanichekesha wewe Kilikuwa ni
kicheko cha Lina huku akiendelea kusema
Sikiliza nikuambie, kama kweli unataka
kuendelea kuishi na Fredy jaribu kupata
mimba nje kwani kila kitu kinawezekana,
mbona hayo ni mambo ya kawaidia tu,
vinginevyo unataka Fredy achukue mwanamke
mwingine." Aliendelea kumshawishi mwisho
wa siku Joyce alikubali kujaribu kwa shingo
upande.
Akiwa nyumbani Joyce alikuwa akiwaza sana
juu ya uamuzi wake wa kujiingiza katika
mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
mwingine "Hili jambo ninalotaka kulifanya ni
hatari sana, lakini sina namna inabidi nifanye
hivi, ila nafsi yangu inasita, kwani namsaliti
mume wangu ila nikifikiria Fredy anaweza
kutafuta mwanamke mwingine." Alikuwa
akiwaza huku akijiuliza maswali aliyokuwa
akijijibu mwenyewe.
Baada ya wiki moja, Lina alimkutanisha Joyce
na kaka mmoja mfanyabiashara aliyeitwa
Sukari. Baada ya kufahamiana taratibu
walianzisha uhusiano wa siri. Lakini wakati
Joyce akiwa anafanya hivyo hakutaka Sukari
agundue lengo lake kuwa ni kupata mtoto.Kwa
kipindi chote Sukari alikuwa hajui kama Joyce
ni mke wa mtu.
Joyce alifanya mambo yote hayo kwa siri sana.
Kwani kwa wakati huo pia alikuwa akijihusisha
kimapenzi na mume wake kama kawaida.
BAADA YA MIEZI MIWILI
Baada ya miezi miwili kupita hali ya Joyce
ilibadilika alijigundua kuwa ni mjamzito.
Alifurahi sana. Huku moyoni mwake akijua
ujauzito alionao siyo wa mume
wake.Alimfahamisha Fredy siku hiyo walikuwa
pamoja nyumbani Fredy alifurahi sana huku
akimkumbatia Joyce kwa furaha.Wakati huu
mapenzi yaliongezeka maradufu kwa mke
wake kipenzi. Baada ya kupata ujauzito Joyce
alianza kukata mawasiliano na Sukari, hakutaka
kabisa kuonana naye.
Na mara nyingi Sukari alimtuma Lina
akamwambie ni kwa kiasi gani anamuhitaji
lakini Joyce hakutaka kabisa kumsikia.Ilifikia
kipindi Sukari alikata tama ya kuendelea
kumfuatilia Joyce. Maisha yaliendele, Baada ya
miezi tisa kutimia Joyce alijifungua salama
mtoto wa kiume. Alimbatiza jina na kumuita
James. Kwa kipindi kirefu Sukari alikuwa
amesafiri alikuwa Mkoani Mwanza katika
biashara zake. Wakati wote huo hakuwa na
mawasiliano na Joyce.
BAADA YA MIAKA MITATU
Baada ya miaka mitatu kupita Sukari alirudi
Dar es Salaam. Siku moja akiwa katika
mizungunguko ya hapa na pale alikutana na
Lina. Alifurahi sana na kumwambia kuwa
angependa kuonana na Joyce, kwani bado
alikuwa akimpenda."Nimefurahi sana kukutana
na wewe Lina natamani sana kumuona Joyce,
nilimpenda sana natamani angekuwa mke
wangu" Alisema Sukari huku akimtizama Lina.
"Umechelewa sana Sukari Joyce ameolewa na
ana maisha yake na mume wake kwani hawezi
tena kuwa na wewe kwahiyo ni vyema
ukamsahau" lakini aliendelea kumsisitiza
amsaidie huku akimuahidi kumpatia pesa
nyingi endapo atafanikiwa.
Lina kutokana na kuahidiwa fedha nyingi na
Sukari, aliamua siku moja kumfuata Joyce
nyumbani kwake alimkuta anacheza na mtoto
wake Mambo shosti naona unazidi kupendeza
na mwanao hahahaha kilikuwa ni kicheko cha
Joyce mwenzangu nina furaha sana James
ananichekesha hapa na maneno yake na hivi
hajui kuongea vizuri huku akimkaribisha lina
walikaa kibarazani na kuanza kuzungumza Lina
alimuuliza Joyce Vipi shemeji yupo Joyce
akamjibu Hayupo amesafiri kikazi kama baada
ya wikimbili ndiyo atarudi Lina akaonyesha
tabasamu na kusema Afadhali kama hayupo
sasa sikiliza rafiki hapa nilipo nimekuja kwako
jana nilikutana na Sukari anakutafuta yaani
ananisumbua sana Joyce alimwangalia Lina na
kusema sitaki hata kulisikia hilo jina hapa
nyumbani kwangu najuta sana kumsaliti mume
wangu..
..je nini kitaendelea usikose SEHEMU YA 14 hapo Alhamisi!