Phenomenon Lady
JF-Expert Member
- Nov 19, 2013
- 407
- 246
Mmmh marafiki hawa!!
KOSA LANGU NI LIPI? Joyce alimwangalia Lina na
kusema sitaki hata kulisikia hilo jina hapa
nyumbani kwangu najuta sana kumsaliti mume
wangu..
..je nini kitaendelea usikose SEHEMU YA 14 hapo Alhamisi!
ameline
Mbona umetukatisha mwisho wa Mama Joyce imekuwa vipi kule Hospitali????????
Je, alipona?????
Je alifariki???
Je, Joyce anajua kuhusu alipo mama yake???
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
KOSA LANGU NI LIPI? Sehemu ya 17
ILIPOISHIA
Fredy alishangaa kusikia hivyo na kusema
Embu mkaribishe ndani Sukari ambaye
muda wote alikuwa amenyamaza kimya
aliingia ndani Fredy alimtizama huku akijiuliza
maswali na nafsi yake "Mbona mimi huyu mtu
simfahamu, na anamfahamu vipi mke wangu."
Aliwaza na kumsalimia Sukari "Habari yako,
karibu sana, sijui ulikuwa na shida gani"
Aliuliza Fredy huku Sukari akiwa anamtizama
bila ya kuzungumza chochote. Je nini
kitaendelea usikose ...SEHEMU ....YA 17.....
INAPOENDELEA
Fredy kuona Sukari amenyamaza kimya,
aliamua kuuliza tena Vipi ndugu ulikuwa na
shida gani? Sukari alimtazama Fredy huku
akionyesha tabasamu la kinafki Sijui nianzie
wapi ili unielewe nadhani Joyce angekuwepo
ingekuwa vizuri zaidi, nafikiri wewe utakuwa ni
mume wake." Aliuliza Sukari Ndiyo, Unaweza
kuongea tu mimi ni mume wa Joyce, kwani
ulikuwa unashida gani?Mbona unazungusha
maneno, kama kuna jambo lolote unaweza
kuniambia bila tatizo, karibu sana, tunaweza
kusogea na kwenda kuketi sebuleni"
Waliongozana na Fredy alimkaribisha vizuri
Sukari.
Wakiwa pale sebuleni walianza mazungumzo
"Karibu sana kaka, sijui nikusaidie kinywagi
aina gani kuna soda, maji na juisi" Alisema
Fredy huku akiwa anamtizama Sukari "Asante
sana, ila sihitaji kinywaji chochote, jambo
kubwa lililonileta hapa, ni kuonana na Joyce,
ili..." Kabla hajamaliza kuzungumza Fredy
alimkatisha na kusema "Joyce hayupo, lakini
kama nilivyokueleza, mimi ni mume wake
unaweza kunieleza jambo lolote na akirudi
nitamfikishia ujumbe, kwani wewe ulikuwa na
shida gani na mke wangu?".
Aliuliza Fredy huku akimtizama kwa kumkazia
macho, Sukari akamjibu Kwasababu
umenisisitiza nitakueleza, mimi naitwa Sukari,
nimefahamiana na mke wako miaka mitatu
iliyopita, na alikuwa ni mpenzi wangu...."Fredy
aliguna kidogo na kusema "Ati unasema miaka
mitatu iliyopita Mama James alikuwa mpenzi
wako? Una uhakika na unachokizungumza
wewe, unajua huyo unayemzungumzia hiyo
miaka mitatu iliyopita tayari alikuwa ni mke
wangu" Alihamaki Fredy huku akimshangaa
Sukari ambaye hakujali kumuona katika hali ile
na kuendelea kusema "Sikiliza nikuambie kaka
mimi sikuwahi kujua kama Joyce alikuwa ni
mke wa mtu, na pia nimekuja hapa kwa lengo
moja tu nahitaji mtoto wangu.
Fredy akamjibu kana kwamba alikuwa
hajamsikia vizuri Eti umesema nini wewe,
unahitaji mtoto wako?au sijakuelewa vizuri
Sukari akamwambia Katika kipindi ambacho
nilikuwa na Joyce alifanikiwa kupata ujauzito
lakini alinificha, sikufahamu lolote kwa kipindi
hicho.Kumbe Joyce alikuwa na nia ya kuwa na
mimi ili abebe ujauzito.Kwani baada ya
kujigundua kuwa ni mjamzito alianza
kunionyesha vituko, na tuliachana bila sababu
yoyote ya msingi, na kwa wakati wote huo
sikujua yeye alikuwa na lengo gani."
Lakini namshukuru sana Lina rafiki yake
kipenzi na Joyce, ambaye mwanzoni ndiye
aliyetukutanisha ameniambia kila kitu. kuwa
Joyce anaye mtoto na ni wakwangu na
vilevile... Kabla hajamaliza kuzungumza Fredy
aliyekuwa akimsikiliza kwa umakini
alimkatisha na kusema Hivi wewe una kichaa,
au umetumwa, nahisi wewe ni
mwendawazimu. Hivii unamzungumzia mke
wangu huyuhuyu Joyce au umekosea njia?
Sukari akahamaki Samahani sana mimi siyo
kichaa nina akili zangu zote timamu. Sasa ni
vyema huyo mkeo angekuwepo ili
azungumze ukweli mimi ninachotaka ni mtoto
wangu. Mimi baba yake nipo hawezi kulelewa
na mwanamume mwingine.
Fredy alikuwa kama haamini anayosikia
alizunguka pale sebuleni bila kujua wapi
anaelekea huku akijisemea Inamaana James si
mtoto wangu? Joyce alikuwa na mwanamume
mwingine siamini kwakweli Sukari akajibu
Wewe uamini usiamini hiyo ndiyo hali halisi
Wakiwa wanaendelea kuzungumza ghafla Joyce
aliingia akiwa hana wazo lolote nini
kinaendelea ghafla alishtuka kumuona Sukari
alishindwa hata kutoa salamu akabaki
ameduwaa , Fredy alimuangalia na kusema
Habari za kazi mke wangu Joyce huku
akitetemeka mithili ya mtu aliyeona kitu cha
kutisha akasema Ni kwema na za hapa.
Fredy akaguna na kusema Mgeni wako huyo
hapo huku akimuangalia Sukari Joyce
alinyamaza kimya huku akiwa ameinama chini
Sukari akasema Nimekuja kumchukua mtoto
wangu mueleze kila kitu mume wako
kwasababu ananiona mimi ni kichaa
Joyce alianza kulia huku akimungalia Fredy na
kusema Nisamemehe mume wangu nimekosa
nisamehe sikudhamiria kutenda yote haya
Fredy kuona vile alisogea karibu na
kumsukuma Joyce kwa nguvu huku akimpiga
na kutoa maneno makali Yaani nilifikiri haya
maneno hayana ukweli kumbe wewe
mwanamke ni muuaji kweli unaamua
kunifanyia mimi yote haya. Aibu gani hii
jamani sikutaki tena Joyce, mchukue na mtoto
wako muondoke na huyo baba yake.
Nakuambia ondoka sitaki kukuona.
Joyce alilia sana huku akijaribu kuomba
msamaha bila ya mafanikio. baadaye msichana
wa Kazi alikuja akiwa na mtoto James. Sukari
alimchukua mtoto akambeba, Jame alikuwa ni
mtoto asiyeogopa watu.Sukari alimwacha
Joyce na kuondoka na mtoto. Joyce alikuwa
akilia huku akiomba msamaha lakini Fredy
hakutaka kumsikiliza na kusema Toka mjinga
mkubwa wewe, Nafikiri hata hiyo mimba
uliyonayo siyo yangu. Kahaba mkubwa wewe
toka nakwambia sitaki kukuona Yaani ilikuwa
ni purukushani ya patashika nguo kuchanika.
Fredy alimtupia Joyce baadhi ya vitu vyake nje
ambapo ilimbidi Joyce aondoke na kuelekea
katika hoteli. Huku mtoto akiwa amechukuliwa
na Sukari . James alikuwa hana tabia ya
kuogopa watu, kwani alikuwa akipendelea sana
michezo. Hivyo ilikuwa ni rahisi kwa sukari
kuishi naye.
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana,
akiwa Hoteli aliwaza sana Eeeh Mungu
naomba unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui
nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa,
nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama
watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa
Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy,
yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya
yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na
hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy
hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura
yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza
Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI
KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA 18.
KOSA LANGU NI LIPI?Sehemu ya 18
ILIPOISHIA
Joyce alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwa
Hoteli aliwaza sana Eeeh Mungu naomba
unisaidie, nisamehe kosa langu, sijui
nitafanyaje, yaani nahisi kuchanganyikiwa,
nyumbani wakigundua baba mkubwa na mama
watanifikiriaje najuta sana kukubali ushauri wa
Lina. Hapa nilipo nina nina ujauzito wa Fredy,
yalaiti ningevuta subira kipindi kile yote haya
yasingetokea.Sasa maji yameshamwagika na
hayazoleki. nimeharibu kila kitu na Fredy
hanitaki tena. Sijui nitaificha wapi sura
yangu.eeh Mungu nisaidie" aliendelea kuwaza
Joyce huku machozi yakimtoka.JE NINI
KITAENDELEA...USIKOSE... SEHEMU YA 18.
INAPOENDELEA
Fredy aliamua kwenda nyumbani kwa walezi
wa Joyce na kuwaeleza hali halisi kuhusiana na
yaliyotokea . Alikuwa akiendesha gari huku
akiwa na mawazo mengi Huyu mwanamke
ameniaibisha sana sikuwahi kutegemea kama
ana tabia mbaya kiasi hiki. Ni vyema
nikawafahamishe na wazazi wake. Ili wajue
nimemfukuza binti yao.
Alikuwa akiwaza huku akiwa anaendesha gari
kwa kasi sana. Kutokana na mwendokasi
aliokuwa nao kidogo asababishe ajali. Ni
baada ya kumkosakosa jamaa mmoja dereva
taksi Wewe kijana -------- sana, mlevi nini
wewe unaendesha gari ovyo. yaani
ungenigonga leo ungenilipa gari jipya
Aliongea dereva taksi kwa ukali huku Fredy
akijifanya kama hajamuona na kuendelea na
safari yake.
Alipofika nyumbani kwa walezi wa Joyce kwa
bahati nzuri aliwakuta wote wapo nyumbani.
Walimkaribisha Shikamoo Mama habari za
hapa Marahaba Karibu mwanangu habari za
nyumbani jamani mbona mmekuwa kimya
sana yaani mnashindwa kabisa kuja
kutusalimia.
Alilalamika Mama Robert Asante Mama
majukumu tu ndiyo yanasabisha kimya
kinakuwa kingi alisema Fredy huku Mama
Robert akiwa anaketi katika sofa lilokuwa
pembeni yake Jamani wanangu haiwezekani
mkapotea kwa kiasi hicho sisi ni wazazi wenu
mnatakiwa kuja kutujulia hali mara kwa
mara.Haya na huyo mwenzio yuko wapi mbona
hamjaongozana Aliuliza Mama Robert .
Fredy alyekuwa amejiinamia kana kwamba
kuna kitu anatafakari akasema Mama kuna
jambo ambalo limenifanya nije hapa leo ni
vyema na Baba angekuwepo ili niweze
kuzungumza nanyi wote. Jambo lenyewe
linamuhusu Joyce Mama Robert alikuwa
anamtazama kwa umakini sana Fredy
nakusema Mbona unanitisha mwanangu kuna
nini kimetokea mwenzio anaumwa au ni nini
tena jamani? Hapana Joyce siyo mgonjwa ila
kuna mambo yametokea nadhani ni vyema
ukamuita na Baba Alisisitiza Fredy. Baba
Robert ametoka hayupo hapa nyumbani wewe
zungumza tu mwanangu hakuna tatizo Fredy
alivuta pumzi na kuanza kumueleza Mama
mlezi wa Joyce kila kitu kuhusu Joyce na
mambo yote yaliyotokea.
Wakati wote akiwa anaelezea Mama Robert
alikuwa akimtazama kwa umakini huku akiwa
ameweka mkono wake wa upande wa kulia
shavuni, Mungu wangu kweli Joyce anaweza
kufanya mambo ya aibu hivyo. Amepatwa na
nini huyu mtoto sasa yuko wapi na mbona
hapa nyumbani hajafika. Jamani balaa gani
tena hili Alizungumza mama Robert huku
akionyesha kupatwa na hasira kwa kile
kilichotokea.
Fredy akamjibuMama binafsi haya mambo
yananiumiza sana akili .Mimi mwenyewe
sikutarajia kama Joyce angeweza kunifanyia
mambo yote haya na ukiniuliza ameenda wapi
mimi siwezi kujua labda atakuwa amemfuata
huyo mwanaume aliyezaa naye. Inaniuma sana
mimi sina lakuongeza nimekuja kutoa taarifa
tu kuwa binti yenu sipo naye tena
ameniaibisha sana.
Mama Robert akainama chini na kuinua uso
wake huku akimtazama Fredy Yaani unajua
siamini ninayosikia inamaana ..... Kabla
hajamaliza kuzungumza mlangoni kulisikika
mtu anabisha hodi Nani tena huyu muda huu
karibu ingia mlango uko wazi Aliyekuwa
amekuja kwa wakati huo alikuwa ni Joyce.
Alifungua mlango na kuingia alishtuka sana
baada ya kumuona Fredy ameketi pale
sebuleni. Alisogea taratibu huku akiwa amejaa
wasiwasi mwingi.Fredy alimtizama kwa hasira
na kunyanyuaka huku akiaga Mama mimi
naondoka nafikiri utakuwa umenielewa.
Joyce alipoona Fredy anataka kuondoka alisoge
na kusema "Fredy naomba usiondoke Mume
wangu, naomba unisikilize mwenzako
sikukusudia kukutendea hivyo nakuomba
unisikilize Aliongea Joyce huku akipiga magoti
na mchozi yakiwa yanamtoka Nikusikilize kitu
gani Joyce, sidhani kama mimi na wewe tuna
lakuzungumza hata kidogo.Mimi siwezi
kukusamehe hata kidogo, wewe endelea na
maisha yako Fredy alifungua mlango na
kuondoka bila ya kusikiliza chochote na sasa
alibaki Joyce na Mama yake mlezi.
Ni aibu gani hii wewe Joyce unajua nashindwa
hata kuelewa kwa yote haya yaliyotokea.
Kwanini umeamua kutuaibisha kiasi hiki. Kweli
wewe ni mtu wa kumsaliti mume wako, tena
umezaa nje ya ndoa? Halafu unadiriki
kumdanganya mume wako kuwa mtoto ni wa
kwake na ni kwa muda mrefu ukiwa umeficha
siri. Wewe mtoto si muuaji wewe ni upumbavu
gani huu Joyce?.
Mama Robert alizungumza kwa hasira Joyce
akiwa amepiga magoti huku mikono yake ikiwa
kichwani Akasema Mama naomba unisamehe
sikukusudia kufanya hivi ni shetani tu alinipitia
na ushauri mbaya wa rafiki yangu nisamehe
mama nampenda sana mume wangu. Funga
bakuli lako eti shetani alinipitia na rafiki
alikudanganya inamaana wewe hauna akili
udanganyike kirahisirahisi tu mjinga sana
wewe tena subiri Baba Robert arudi sijui
atakufanya nini wewe. JE NINI
KITAENDELEA ...USIKOSE...SEHEMU YA ....19...hapo Ijumaa!